MIRIAM CHIRWA AFANYA KOLABO NA KALA JEREMIAH

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah anaendelea na nyimbo zake za kiuwanaharakati ambapo anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘Wana Ndoto’ aliomshirikisha mwanadada Mirium Chirwa.

Rapper huyo alisema wimbo huo unazungumzia maisha ya jamii pamoja na watoto wadogo ambao wana ndoto za kufanya mambo fulani katika maisha yao.

wiki hii, Kala ameamua kuweka wazi uwezo na binti huyo ambaye amemshirikisha katika wimbo huo.“Nimewahi kukutana na watoto wengi wenye vipaji lakini sijawahi kukutana na mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu kama huyu mtoto,” aliandika Kala kupitia instagram.

Aliongeza, “Anauwezo mkubwa sana wa kuimba na ana akili nyingi sana. Mungu kambariki sana. Ukitaka kuamini hayo subiri tarehe 26/7 /2016 siku ambayo ‪#‎wanandoto‬ inatoka. huyu ndiye kaimba kiitikio. wakati unaendelea kusubiri Wana Ndoto unaweza kwenda youtube na kuandika miriam chirwa utaona mambo yake. na utaamini ninachokisema,”
MIRIAM CHIRWA AFANYA KOLABO NA KALA JEREMIAH MIRIAM CHIRWA AFANYA KOLABO NA KALA JEREMIAH Reviewed by WANGOFIRA on 20:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.