Donald Trump akubali uteuzi wake

Donald Trump ameahidi kukomesha matukio ya uhalifu na vurugu nchini Marekani endapo atafanikiwa kuwa rais mteule wa taifa hilo, ahadi hii ameitoa kwatika hotuba yake wakati alipokuwa anathibitisha ukubalifu wake wa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
 
Maneno ama ahadi hiyo imo katika moja ya kifungu cha hotuba yake hii ni baada ya kuvuja kwa hotuba hiyo na kudakuliwa na wataalamu wa udakuzi na kueleza kuwa hotuba hiyo imesheheni ahadi tele za ya kurejesha utawala wa sheria , ikiwemo suala la kukabiliana na uhamiaji haramu na kwamba suala hilo ataliingiza katika sera za kigeni za Marekani.

Pamoja na hayo Trump anatarajiwa kutoa tamko kuwa mara moja atahakikisha anasimamia suala la wahamiaji haramu kutokana na mataifa kuathiriwa na wimbi la masuala ya ugaidi na kusisitiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka baina ya Marekani n a nchi ya Mexico ili kuondokana na suala la wahamiaji.

Naye mpinzani wa Donald Trump bibi Hillary Clinton, atathibitishwa juma lijalo kupitia chama chake cha Democrats ambapo chama hicho kitakuwa mkutano mkubwa katika jimbo la Philadelphia.

BBC
Donald Trump akubali uteuzi wake Donald Trump akubali uteuzi wake Reviewed by WANGOFIRA on 20:54:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.