NDOA YA SIKU 7 YAVUNJIKA KWA PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA MIAKA 7 ILIYOPITA NA EX BOYFRIEND WAKE


Kuna picha zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mwanamke akifanya mapenzi na mpenzi wake. Yote hayo yalitokea siku chache tu baada ya mwanamke huyo kufunga ndoa na mwanaume mwingine jijini Dar es Salaam.



Mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo alijipiga na mpenzi wake zamani miaka saba iliyopita wakiwa chuoni na zimekuja kusambaa ndani ya wiki baada ya kufunga ndoa. Anadai kuwa ni kisasi cha ex wake aliyedhamiria kuivunja ndoa yake.



Akiongea kwenye Ripoti ya Siku ya kipindi cha Ubaoni cha EFM kilichoruka Ijumaa iliyopita, mwanamke huyo amedai kuwa picha hizo zimedhamlilisha mno kiasi cha kuiharibu ndoa yake, kuwaumiza ndugu zake na kuwakosea heshima wakwe zake na kwamba anajuta kupita kiasi.


“Ni kweli ni mimi ndiye niliyepiga hizo picha lakini ni muda mrefu tangu kipindi nikiwa chuo, yaani hata huyo mtu mwenyewe sijui yuko wapi sina mawasiliano naye tena, sikutegemea kiukweli,” anasema mwanamke huyo.


“Ni kitu ambacho kinaniuma na kimeniharibia mlolongo mzima wa maisha yangu, mpaka sasa hivi sielewi, mume wangu hawezi kunielewa tena na yeye ndio nimemwekea kama nguzo, ndio kila kitu kwasababu hata familia yangu hainielewi ,” ameongeza.

“Mpaka sasa hivi sijui nafanya nini.”


Kwa upande wa mume wake, alidai kuwa picha hizo zimeuvunja moyo wake.

Wakifurahia Ndoa yao kabla ya mambo kuharibikaBOFYA <<<HAPA>> KUONA PICHA NYINGI ZAIDI
“Tulikuwa tumeshaenda kwenye honey moon tumerudi, sikuamini macho yangu baada ya kuona hizo picha na huyu mwanamke, rafiki zangu walikuwepo wengi sana, best man wangu pia ni vitu ambavyo kuvizungumza mimi nashindwa, naanzia wapi, lakini mapenzi huwa yako hivyo, inawezekana iko hivyo lakini sasa kama mazingira kama yale hata kama ukiwa ni wewe lazima utaumia, familia yangu ntaiambia nini mimi, imenigharamia harusi kubwa,” alisema mwanaume huyo.


Amedai kuwa haoni kama inawezekana tena kukaa chini na mke wake huyo kwa kile kilichotokea.


“Nikae chini ili iweje?” alihoji kwa jazba. “Imeniuma, imeniumiza sana hii kitu haki ya Mungu, hata kama miaka kumi imepita kwanini imekuja kwenye harusi yangu, zawadi zimekuja kwaajili ya harusi yetu kwanini aletewe picha za aina hiyo? Angeniambia before kwamba nilikuwa na moja mbili, ningekuwa najua, lakini amenificha. Imenicost kwa kiasi kikubwa sana, nitaiambiaje familia yangu kwa mfano? Nitasema nini.”


“Sitokuja kupenda tena mwanamke wa aina yoyote ile, mpaka nakuja kuingia kaburini, I swear to God, imetosha kabisa.”
Wawili hao walifunga ndoa tarehe April 23 mwaka huu.


Kwa mujibu wa best man wa harusi hiyo, waliziona picha hizo siku nne baada ya harusi wakati wanafungua zawadi walizopewa na kuzikuta zikiwa kwenye bahasha na kusababisha vita kubwa kwenye familia yao.


Anadai kuwa rafiki yake hataki kusikia chochote kuhusiana na kumsamehe mke wake na jitihada za ndugu kuwasuluhisha zimegonga mwamba. 

“Yaani hapo alipo nakuambia haelewi, mtu anayenisikiliza ni mimi tu, hasikilizi mtu yeyote. Huyo mwanamke ndio analia muda wote, jamaa haelewi,” amesema best man huyo aliyejitambulisha kwa jina la Geofrey Nicholas.





NDOA YA SIKU 7 YAVUNJIKA KWA PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA MIAKA 7 ILIYOPITA NA EX BOYFRIEND WAKE NDOA YA SIKU 7 YAVUNJIKA KWA PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA MIAKA 7 ILIYOPITA NA EX BOYFRIEND WAKE Reviewed by WANGOFIRA on 00:02:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.