ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI MHE. ANGELINE MABULA MKOANI TANGA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati akikagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Wilayani Mkinga wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki (mwenye tai) na Meneja NHC Tanga Issaya Mshamba.
2
3
Baadhi ya Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Wilayani Mkinga ambazo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameamuru watumishi wa wilaya hiyo waamie ifikapo tarehe 1 Agosti 2016.
4
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe (mwenye tai nyekundu) mara baada ya kujadili changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.
5
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na wananchi wa Hale wilayani Korogwe mkoani Tanga na kutolea ufumbuzi migogoro ya Ardhi inayowakabili.
6
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Tanga. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA ARDHI.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula ametoa Siku kumi na mbili kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuhama Tanga Mjini na kuhamia Wilayani Mkinga mahali zilipo nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizojengwa kwa ajili yao.
Naibu Waziri Mabula ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake wilayani Mkinga ambapo pamoja na mambo mengine alipata nafasi ya kutembelea eneo zilipojengwa nyumba hizo na kumuagiza Meneja wa NHC mkoa wa Tanga kuhakikisha tarehe 1 mwezi wa Agosti 2016 watumishi hao wanahamia katika nyumba hizo.
kwa sasa watumishi hao wamekuwa wakiishi Tanga mjini na kufanya kazi wilayani mkinga, hali inayowalazimu kusafiri zaidi ya kilometa 50 kilasiku kwenda na kurudi.
Mheshimiwa Mabula yupo katika ziara ya siku nne mkoani Tanga ambapo anatembelea Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya za Tanga mjini, Korogwe pamoja na kuzindua baraza jipya la Wilaya ya Kilindi. Hata hivyo mbali na mabaraza ya Ardhi mheshimiwa Naibu Waziri anatembelea miradi ya NHC pamoja na kutatua kero za migogoro ya Ardhi na changamoto za watumishi wa sekta za Ardhi mkoani Tanga.na Mjengwa blog.
ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI MHE. ANGELINE MABULA MKOANI TANGA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI MHE. ANGELINE MABULA MKOANI TANGA Reviewed by Unknown on 00:33:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.