RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 27 & 28 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi:Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia....
   Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala kwenye mwili wangu hususani kifuani mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi

Endelea...

   Nikastukia baba akitoa ukulele na kuanguka chini na kumuona sheila akiwa ameshika kipande cha mbao kinachoonekana kimechomolewa kwenye benchi huku kikiwa kinavuja damu kwenye sehemu ambayo ilitua kichwani mwa baba.Sheila akaanza kutetemeka baada ya kumuona baba akiwa anavujwa na damu za kichwa,madaktari wakaninyanyua na kunirudisha kwenye kitanda huku hali yangu ikizidi kuwa mbaya na mamcho yangu yakaanza kutawaliwa na ukungu na kwambali nikamuona sheila akishikwa na askari wawili na wakaanza kumtoa enje akiwa ananililia kwa uchungu.Kitanda nilicho kilalia kikaanza kusukumwa taratibu na jinsi ninavyo isililizia hali yangu yenye maumivu makali ya mwili nikajikuta macho yangu yakitawaliwa na ukungu mwingi na sikujua ni kitu gani kinacho endelea.
 
                                                    *****
 
 Baridi kali ikaanza kunisumbua mwili wangu na kujikuta nikianza kufumbua macho yangu na kujikuta nikitazama sehemu ya juu ambayo kwa haraka haraka sikujua nipo wapi.Mwili wangu ukawa umebanwa kidogo na na kwa haraka haraka nikagundua kuwa nipo kama nilivyo zaliwa kwani kiwamgo cha baridi kilitawala mwili wangu mzima,nikajariu kujigeuza ila nikajikuta nikishindwa na nikaanza kujisukuma na kumbukumbu za akili yangu ikagundua kuwa sehemu niliyopo ni katika majokofu ya kuhifadhia miili ya watu walio fariki dunia.

Nikajaribu kuita ila sikusikia msaada wa mtu wa aina yoyote wala kitu kikitembea nje ya majokofu hayo,nikazidi kujitahidi huku miguu yangu nikiigonga gonga kwenye sehemu ya chini ya jokofo ambapo ndipo miguu yangu ilipo elekea na kujikuta sehemu niliyo ilalia ikienda mbele na kufunguka.Nikaendelea kujikaza huku nikizisidi kujitahidi kujitoa ndani ya jokofu hili na chakumshukuru mungu nikafanikiwa kulifunua kwa uwazi mdogo ulio niruhusu kuitoa mikono yangu kwa nje na kujivuta na likafunguka na kupata uwezo wa kukaa na kitako na kuanza kushangaa.
 
Woga ukaanza kunitawala na baada ya kujikuta nikiwa nimeshonwa katikati ya kifua changu na kitu kingine kilichoizidi kuniogopesha ni miili mingi ya watu walio lala chini huku wakiwa wamefunikwa malailoni yanayo waonyesha vizuri huku miili yao ikiwa imeharibiwa sana huku wengine vichwa vyao vikiwa vimepasukwa na kurudishiwa rudishiwa kiasi kwamba wanatisa kwa muonekano wao.Nikashuka kwenye jokofu nililo kuwepo na taratibu nikaanza kuutafuta mlango wa kutokea katika chumba hichi na kabla sijauona nikastukia taa za chumba zikizima na giza kali likazidi kutawala.
 
Nikajikaza na sikutaka kuuruhusu woga kutawala katika mwili wangu kwa wakati huu,nikapapasa papasa ukutani kwa dakika zaidi ya mbili na kufanikiwa kukuta mlango na kabla sijaufungua nikasikia watu wakizunumza kwa nje
“muambie huyo mudi awashe hilo genereta la upande huu kuna maiti tunataka kuziingiza humu”
 
“kwani hao nao wametokea wapi?”
“kuna basi limeanguka na kuua watu ishirini”
“sasa huku ndani si kumejaa hadi maiti nyingine tumeziweka chini tutafuta ustaarabu wa kuwatoa kesho wakazikwe na manispaa kwa maana hata ndugu zao hawajitokezi”
“hawa tutawaweka hivyo hiyo bwana kwani hatuna seemu nyingine ya kwenda kuwaweka na hospitali zote za wilaya mochwari zao ni ndogo”
 
Watu waliopo nje wakaendelea kujibishana nikataka kupiga kelele za kuomba msaada ila roho yangu ikasita na kujua ni lazima watu waliopo nje wataogopa na kukimbia na ningelisitisha zoezi zima la wao kuingiza maiti wanazo zizungumzia,taa zikawaka na mlango nikausikia ukifunguliwa na baada ya dakika kakika moja mlango ukafunguliwa
“hembu shika huko vizuri usije ukamuachia”
 
Gafla umeme ukakatika na kuwafanya watu walio ibeba maiti wanayo taka kuuingiza kuanza kutukana matusi mazito na kwakupitia uwazi mdogo wa mlango nikastukia kuona wakiondoka kwa hasira huku maiti wakiwa wameilaza chini na sikujua ni wapi wanapo elekea,nikachungulia nje na kukuta kuna giza ila mwanga wa mbalamwezi uliweza kunisaidia kuona baadhi ya majengo na kungundua bado nipo sehemu ya muhimbili.Nikaanza kuoiga hatua za haraka na kutoka ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti na nikafika kwenye jengo ambalo nikakuta kamba nyingi zikiwa zimeanikwa makoti meupe ya madaktari.Nikalishusha moja kwenye kamba na kulivaa kwa haraka kisha nikachukua suruali nyepe na kuivaa na muonekanao wangu ukawa kama wauduzi wa kiume kwenye hospitali hii.

Nikaanza kutembea kuelekea getini huku miguuni nikiwa nipo peku peku na nikafanikiwa kutoka pasipo walinzi kunitilia mashaka ya aina yoyote.Nikatafuta sehemu na kukaa huku akili yanu ikianza kufikiria ni kitu gani kilicho wafanya madaktari hadi wakanipeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.Nikajikuta nimejishika tama na kugundua mashavu yangu yamejaa ndevu  nyingi na kwaharaka haraka nikagundua ni kipindi kirefu nimekaa hospitali kwani ndevu zangu huchukua muda mwingi sana katika kuota na kuwa ndefu kama nilivyo zikuta sasa.
 
Nikapata wazo la kwenda nyumbani kwa sheila japo ni mbali sana na sehemu niliyopo nikaona sina budi kufanya hivyo.Nikapiga moyo konde na kunyanyuka sehemu niliyo kaa na kuanza kutembea japo njaa kali inanisumbua tomboni kwangu ila nikajitahidi kwenda kutembea kwa haraka ili niweze kufika.

Nikatumia kama masaa mawili na kufika nyumbani kwake na kukuta ukimya mwingi ukiwa umetawala ila kitu kingine kilicho anza kunipa wasiwasi ni nyasi nyingi na ndefu zilizo oto nje ya geti lake na kwaharaka nikajua sheila hayupo ndani ya nyumba yake kwa maana kama angekuwepo kusingekuwa na nyasi nyingi huku geti lake likiwa lemetawaliwa na vumbi jingi.Ikanibidi kuchungulia kwenye eti lake ili kujionea mwenyewe nikipingana na mawazo yagu ya kusema sheila hayupo ndani ya nyumba yake.Giza lilitawala kwenye nyumba yake na hapakuwa na dalili yoyote ya mtu kushi na jinsi mlango tulivyo ufunga siku ya mwisho ndivyo jini ulivyo kwa sasa.Nikashusha pumzi nyingi huku nikitazama wapi nielekee na mbaya zaidi sikua na jirani yoyote wa sheila ninaye mjua ambaye ninaweza kumuulizia habari za sheila
 
Hali ya uchunu ikaanza kunitawala na kwa mbali machozi yakaanza kunilenga lenga na kujikuta nikitamani utokee muujiza sheila kusimama mbele yangu,wazo la kuwa na mama likaanza kunijia ila kutokana na kuchoka nikashidwa kujua kama nitaweza kwenda nyumbani ambapo tulikuwa tunaishi ila woga ukaanza kunijia kwani kumbukumbu ya baba siku alivyokuwa akinipiga ikanijika kichwani kama mkanda wa video ila ukakata gafla baada ya kusikia mnguruo wa mbwa ukitoka nyuma yangu.

Nikageuka na kukutana na mbwa wakubwa wawili wakiwa wananguruma huku wakinitazama kwa macho yao makali kiasi kwamba nikajikuta nikiaanza kutetemeka.Nikatulia kwa muda huku mwili wangu ukishindwa kukimbia kabisa kutokana na njaa kali iliyopelekea nguvu za mwili wangu kuniiishia.Nikasikia mlunzi wa mtu akiwaita mbwa walio karibu yangu na wakaelekea walipo itwa na kumuona mlinzi wa nyumba ya jirani akiwa amesimama huku mbwa wake wakiwa wamenzunguka na mkononi mwake akiwa ameshika bunduki yake aina ya gobore
 
“samahani kaka”
Nilimuita mlinzi kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku nikianza kupiga hatua za taratibu za kumfwata sehemu alipo na kabla sijamfikia akaikoki bunduki yake na kunielekezea
“usipige atua nyingine ya kunfwata la sivyo nitakulipua”
Nikasimama huku nikiwa ninamwangalia mlinzi na sikua na cha kufanya zaidi ya kuwa mnyonge mbele ya mlinzi huyo
“samahani kaka yangu kuna kitu ninaomba nikuulize”
 
“uliza fasta fasta”
“eti huyu dada aliyekuwa akiishi humu ndani yupo wapi?”
“kwani wewe ni nani yeke?”
“mimi nilikuwa ni mchumba wake?”
“unaudhibitisho gani kwamba wewe ulikuwa ni mchumba wake?”
“ninaweza kukutajia jina lake”
“anaitwa nani?”
“sheila”
“sasa wewe itakuwaje usijue habari za mchumba wako?”
“ni hstoria ndefu ndugu yangu”
“sasa kwa ufupi huyo demu yupo jela”
“jelaa.....!!!?”
“unashangaa nini sasa.........? Wewe si ulitaka kujua ni wapi alipo huyo demu?”
“jela gani?”
 
“sijui yupo gereza gani ila ukweli ni kwamba amefungwa”
“amefungwa kwa kosa gani?”
“kaka mimi sio hakimu bwana kama unataka nenda kisutu kaulizie watakuambia”
Wasiwasi ukaanza kunijaa mwilini mwangu na kujikuta chozi likinitoka na sikutaka nilie mbele ya mlinzi
“kwani leo ni tarehe ngapi?”
“wewe jamaa umevurugwa na nini hata tarehe umesahau?”
“naoma tu nijue ndugu yangu”
“ni terehe 15 mwezi wa sita haya hadi mwezi niemkutajia unaweza ukachapa lapa kwani bosi wanu akitoka hapa akikuta ninazungumza na watu kibarua changu kinaweza kikaota mbawa bure”
 
Nikajikuta nikizidi kufadhaika kwani nimiezi mine imepita tangu nilipo kutana na tatizo la kupigwa na walinzi wa uwanja wa ndage.Nikaondoka kinyone huku nikitazama tazama nyuma nikitamani nimueleze mlinzi njaa ninayo ihisi tumboni kwangu hata kama anaweza kunipatia chakula kidogo ila nikashindwa kwani tayari alishapandwa na hasira.Nikaendelea kutembea huku sijui ninapo elekea kwani mawazo mengi yanakizungusha kichwa changu kiasi kwamba ninajikuta nikiongea ongea mwenyewe.

Nikakuta watu wapatao sita wakiwa wamelala kwenye maboksi nje ya baraza za maduka mengi na kujikuna mimi nikikaa kwenye moja ya baraza ambayo ukuta wake umechorwa picha za wasichana na kugundua ni saloon ya wanawake.Usingizi haukuweza kunijia na kila nilipo jaribu kuutafuta nikajikuta nikijipiga piga mwilini kuwaua mbu wanao ning’ata mwilini mwanu.Hadi kunaanza kupambazuka nikajikuta nikipitiwa a kausingizi kazito na kujikuta nikilala kwenye sakafu pembezoni mwa geti la salooni hii ya kike.
  
Nikastukia mguu ukinigonga gonga begani nikayafumbua macho yangu na kukuta mwanga wa jua ukiwa uemshatawala eneo zima,macho yangu yakakutana na msichana mrembo akiwa amevalia suruali nyeupe iliyo mbana vizuri na kuyafanya makalio yake makubwa kuonekana vizuri huku sura yake akiwa ameipamba kwa vipodozi vinavyo onekana ni vyagharama.Mkononi mwake akawa amezishika funguo nyingi na tukabaki tumetazamana
“unanianaliangalia nini hembu nyanyua mindevu  yako nahitaji kufnugua geti langu”
 
Nikanyanyuka na kusogea na kukaa pembeni kidogo,akafungua geti lake la saloon na kuingia ndani na kuanza kupana vitu vyake.Watu wengi wanapita mbele ya macho yangu huku kila mmoja akionekana kuwa na mihangaiko yake ya kutafuta chochote kwa siku hii.Nikapiga miyayo ya uchovu na kusimama ila nikashindwa kupiga hatau yoyote kutokana na kuchoka sana,nikakaa chini na kuanza kutafakari ni nini nifanye ili kuweza kupata hata kifungua kinywa nikachungulia ndani ya saloon na kumuona dada wa saloon akiendelea kufanya usafi.
 
“samahani dada ninaweza kukusaidia japo kufagia fangia”
“kwani nilikuomba unisaidie?”
“hapana ila nimeomba tuu kama ninaweza kukusaidia”
“usije ukawa kibaka ukaniibia vitu vyangu humu ndani”
“hapana dada mimi sio kibaka”
“haya njoo unipigie deki”
 
Nikanyanyuka huku nikiwa na fauraha kidogo ya kuweza kupata chochote cha kula,akanipa tambara la deki pamoja na kindoo chenye maji kidogo na nikaanza kupiga deki taratibu huku nikijitahidi kusafisha kila sehemu ya salooni hiyo.Nikamaliza na kupiga deki kwenye eneo zima la saloon
“tayari dada yangu”
 
“haya asante”
“dada yangu naomba japo kajipesa nikanunue kifungua kinywa”
“haaa kumbe ulikuwa unapiga deki ili nikulipe.......? Mimi nilidhani umenisaidia bure”
“hapana mimi ninaomba japo kidogo tu niweze kupata kifungua kinywa”
 
Dada akafungua pochi yake na kutoa shilingi mia mbili na kunipa nikabaki nikiitazama kwa sekuende kadhaa pasipo kusema chochote na kwajinsi ya ugumu wa maisha ya dar es saalam yalivyo magumu kwa shilingi mia mbili siwezi kupata chochote nitakacho weza kula.
“dada yagnu huwezi kuniongeza japo mia tatu ili iwe mia tani niweze kupata chochote tuu”
 
“kaka yanu hiyo ndio hela niliyo nayo na kama unataka kifungua kinywa jana niliacha kiporo cha ubwabwa wa mchana unaweza kufungua hilo hotpot hapo juu ya meza utakiona chakula”
 
Sikuwa na jinsi nikalisoelea hotpot alilo nelekeza na kulifungua na kukutana na harufu kali ya ubwabwa ulio chacha ambao umepikwa na nazi huku ukiwa na maharage yake.Nikakitaama kwa muda kisha nikaanza kukila haraka haraka na kunya dada wa saloon akibaki akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao.Ubwabwa ukaanza kuniongea ila nikajikuta ukiwa unaelekea ukingoni kwani niliufakamia fakamia kwa haraka,nikajilamba vidole vyangu kwa utamu nilio upata kisha nikasima na kunawa mikono yangu kwa maji niliyo pigia deki.
 
“asante dada yangu”
Dada wa saloon akabaki akiwa amenitazama huku akikiangalia kifua changu na kugundua kuwa anatakuwa amestushwa na mstari wa oparesheni niliyo fanyiwa
“nakuomba utoke ndani ya saloon yangu kabla sijakuitia polisi kwani unaonekana wewe ni jambazi”
“kwa nini?”
“usitake kujua kwa nini au unataka nikupigie kelele za mwizi?”
 
Sikutaka makuu ya kubisha na dada wa saloon nikaondoka huku nikiwa ninajisikia vibaya kwa jinsi maisha yangu yalivyo badilika.Nikaondokoka na kuelekea nyumbani kwetu huku nikijifariji liwalo na liwe.Nikiwa njiani nikajiku nikisimama na baadhi ya watu wanaosoma magazeti kwenye kibanda kidogo na gazeti moja lina pichwa kubwa ya sheila huku pembeni yake kukiwa na kitanzi na juu yake kukiwa na maandishi makubwa yaliyo nistua na kujikuna nikianza kutetemeka yanayo someka
“muuaji wa mtoto wa waziri ahukumiwa kifungo cha kunyongwa hadi kufa”   
 
                           *****sory madam*****(28) 


“haaa...!!”
Nilishanga kwa sauti ya juu na kuwafanya watu walipo pembeni yangu kunishangaa kiasi kwamba nikajikuta nikitazamana nao huku wakinishangaa,nikataka kuondoka ila dada muuza magazeti akaniita na kunifanya nirudi sehemu alipo.
 
“kaka nahisi nimesha wahi kukuona sehemu?”
“labda utakuwa unanifananisha”
“hapana wewe ndio eddy?”
Moyo ukanistuka na kujikuta nikitaka kukimbia ila miguu ikaishiwa ujasiri wa kufanya hivyo na kujikuta nikianza kutetemeka.
 
“huyu si ndio jamaa aliyesemekana kuwa ameuliwa?”
“ndio huyu”
Watu wakaanza kubishana mmoja baada ya mwengine huku kila mmoja akionekana kunishangaa hadi wakanizunguka
“jamani muacheni kaka wa watu aondoke munamshangaa hadi anajisikia vibaya”
“sasa si tunataka kujua ni nini kilicho mpata”
“jamani hembu acheni wanga mimi ndio nimemuita sasa kila mmoja akiwa anataka kujua ni nini kilicho mpata kaka wa watu ni umbea”
 
Watu wakaendelea kubishana wenyewe kwa wenyewe na dada mwenye kibanda cha kuuza magazeti akanishika mkono na kunivuta pembeni na tukaingia kwenye moja ya duka lililopo pembei ya kibanda hicho na kumuomba muhisika wa duka hilo kutupa nafasi kidogo ya kuzungumza na muuza duka hakuwa na lakupinga akatupatia viti viwili na tukakaa
 
“najua utajiuliza ni kwani ni nimekutoa kule kukuleta huku ila ngoja kwani nijitambulishe....Mimi ninaitwa judith na nimuuza maazeti pale kwenye kibanda ndio ofisini kwangu na mimi nimekuwa ni msomaji mkubwa sana wa stori ianyo endelea sasa kwa huyu dada sheila kumuua mtoto wa waziri hadi jana alipo hukumiwa kunyongwa hadi kufa”
 
“ina maana sheila ndio ameniua mimi?”
“kaka yangu mimi wala sijajua kama huyo dada ndio muhusika ila kwa msaada ngoja nimpiie mchumba wangu ambeye ndio muandishi wa habari yako aje hapa tujuae ukweli”
 
Judidh akatoa simu yake na kumpigia mtu aliye dai ni mpenzi wake na baada ya muda jamaa akafika sehemu tulipo akitumia usafiri wa pipipiki aina ya boxer.Judith akampisha mpenzi wake kwenye kiti alicho kaa na yeye akasimama pembeni na jamaa akanipa mkono huku akionekana kunishangaa kwa jinsi nilivyo
 
“mimi ninaitwa john ni muandishi wa habari wa gazeti”
“nashukuru kukufahamu”
Judidh wakabaki wakiwa wametazamana pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote kisha john akakohoa kidogo huku akiaachia tabasamu pana mdomoni mwake na kuanza kuzungumza
 
“kaka mimi ni miongoni mwa watu walio tokea kuguswa na tukio lako la kusemekana kuwa umekufa ila nikaamua kulifwatilia kina ubaga hadi sasa hivi ninaanza kupata picha ambayo itaweza kumsaidia mpenzi mpenzi wako katika kuachiwa huru.......Nilizungumza na sheila akanielezea kisa kizima na alidai kuwa ameonewa kwa maana tangu siku ambayo wewe ulipelekwa katika chumba cha kufanyiwa oparsheni ndio siku ya yeye alipo kamatwa na polisi kwanza akashikiliwa kwa kosa la kutaka kumuua mkuu wa jeshi ila kutoka na ushaidi kutoka kwa manesi na madaktari ukamsaidia sana sheila kuishinda kesi ya kumjerehi baba yako ambaye alitaka kukuua hadharani”
 
“ina maana baba yangu yupo hai?”
“ndio yupo hai na nimiongoni mwa watu walio nipa vitishi endapo nitaendelea kulifwatilia hili swala.......”
“mama yangu je yupo hai?”
“mama nilipata habari kuwa amelazwa nchini afrika kusini kwani alipata ugonjwa wa mstuko wa moyo na hadi sasa hivi sijajua anaendeleaje”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikijaribau kusubiria  ni nini kilitokea katika maisha yangu ila sikupata pichaya aina yoyote
 
“ishu ilikuwa hivi.......Alitengenezwa mtu anaye fanana na sheila na kwakupitia picha rada zilizopo hospitali alionekana akitoka kwenye chumba ulichokuwa umelazwa huku akiwa ameshika sindano mkononi na kwamadai ya madaktari wakasema kuwa msichana huyo ndio amehusika kwa kukuchoma sindano ya sumu iliyo pelekea maisha yako kuwa mwisho”
 
“ngoja kwanza unataka kuniambia kuwa sheila yeye hakuuhusika na chochote?”
“ndio sheila hajausika na kiyu cha aina yoyote juu ya kukuchoma sindaono kwa maana kipindi tukio la wewe kuchomwa sindano linatokea sheila alikuwa mikononi mwa polisi na hadi sasa hivi ninavyo zungumza sheila ndio huyo siku zake zina hesabika”
“huyo daktari aliye dhibisha kuwa nimechomwa sindano ya sumu ni yupi huyo?”
“ngoja nikuonyeshe”
 
John akatoa simu yake na kuwela upende wa video na nikamuona daktari wa familia akiwa anazungumza kwa masikitiko makubwa na mbele ya waandishi wa habari na kunifanya nibaki mdomo wazi
“sasa huyu mzee ndio mbaya wenu katika hii familia?”
“kwa nini?”
“yeye ndio chanzo kikubwa cha baba yako na mama yako katika kugombana?”
“wewe umejuaje?”
 
“mimi nilimuhoji siku akiwa amelewa sana kwa maana huyu mzee ni mjomba wangu na akanieleza vitu vingi sana juu ya familia yako”
“vitu gani?”
“kwanza yeye ndie aliye muambia baba yako kuwa wewe sio mtoto wake wa kumzaa na kitu kikubwa kilicho msababisha baba yako kuchukua uamuzi wa kutaka kumuua mama yako pamoja na wewe ili kuweza kuzirisi mali zote ambazo mama yako anazo”
 
“mmmm sasa mimi mbona ninafanana sana na baba yangu?”
“ndio kutokana baba yako ana pacha wake ambaye ni doto na yeye ndio baba yako wa damu na wao wanafanana sana kiasi kwamba ni vigumu sana kwa mtu kuweza kutambua kuwa wewe baba yako si huyo mkuu wa jeshi”
 
Ni habari mpya katika maisha yangu kwani mama yangu hakuweza kuniambia siku hata moja kuwa baba yangu ni pacha wa baba yangu wa sasa ambaye amejenga chuki kubwa juu yangu na mama yangu,nikajikuta machozi yakianza kunimwagika
 
“kaka jikaze usilie ila huo ni ukweli ambao mimi ninakuambia na huyu daktari mimi ni mtu wangu wa karibu ukiachilia kuwa ni mjomba wangu ila ni zaidi ya hapo kwani vitu vyake vingi huniambia kiasi kwamba vingine siwezi kuvizungumza hapa........Ila ninakuomba sasa hivi tukajaribu kuyaokoa maisha sheila ambeye niliapa kumsaidi sheila hadi mwisho wa maisha yake tana kuna hii sauti niliirekodi kipindi anazungumza kwa uchungu na mimi”
 
‘ni kweli sijamuua eddy wangu mimi ninampenda sana na yeye ndio mwanaume wa ndoto zangu.....Mimi nipo radhi kufa kwa ajili ya mume wangu eddy nikaonane naye peponi kwa mungu.....John nakuomba usijisumbue sana kwa ajili yangu kwani mimi huu ndio mwisho wa maisha yangu”
“hapana sheila usilie mimi nipo tayari kukusaidia kuuvumbua ukweli juu ya hili kwani siamini kama wewe ndio muuaji”
“hapana john wewe niache tu nikafungwe sina jinsi ya kufanya na huu ndio mwisho wa maisha yangu bai john”
 
John akazima simu yake baada ya kuniona ninazidi kutokwa na mahozi mengi na akaniomba nikaze twende tupate msaada wa mwana sheria wa serikali.Tukasimama na john na kutoka nje ya duka huku sura yangu nikiwa nimeiinamisha chini ili watu wasiyaone machozi yangu,tuakapanda kwenye pikipiki yake na moja kwa moja tukaelekea kwenye mahakama ya kisutu na john akanipeleka kwenye ofisi za mwanasheria wa serikali aliye simamamia kesi ya kuhukumiwa kwa sheila na kitendo cha kuingia kwenye ofisi yake kikamfanya mwana sheria huyu kustuka kiasi kwamba akanyanyuka na kubaki akinitazama.
 
“mkuu samahani kwa kukuingilia ofisini kwako pasipo kuwa na taarifa maalumu ila kama unavyo one mbele yako nimekuja na eddy ambaye inasadikika ni mfu”
Mwanaheria wa serikali akabaki amesimama pasipo kujibu kitu cha aina yoyote na kubaki akibabaika pasipo kujibu kitu cha iana yoyote
“mkuu tunahitaji msaada wako wa hali na mali”
“ehhee umesema amefufuka?”
 
“hilo mimi sijui atasema mwenyewe kwamba amefufuka ila kidhibitisho ni kwamba eddy mwenyewe huyu hapa na hajafa kama mulivyo mdhania ila ninakuomba uweze kutusaidi kuhairisha mauaji ya sheila”
“dooo watakuwa wanakaribia kumua kwani zimebaki dakika 45 tu kabla hajanyongwa”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta nikanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi ya mwanasheria wa serikali na kuwaacha john na mwanasheria wa serikali wakizungumza
 
“tunakuomba sana uweze kutausaidi kama tunaweza kwenda kumuona”
“ahaa sasa hiyo ni ngumu kwa maana amesha kabidhiwa kwa askari maalamu wana shuhulika na hilo swala kwa hiyo mimi siwezi kwenda”
“nipo chini ya miguu yako kiongozi ninakuomba twende au tuambie tu niwapi alipo”
“kwa hilo mimi siwezi kuzungumza chochote juu ya hilo”
 
John akapia maoti huku sura yeke ikiwa ina mwagikwa na machozi na ila mwasheria akaanza kutingisha kichwa cheke akishiria hataki kukubaliana na kile anacho obwa na john.Kwa hasira nikapiga hatua hadi sehemu aliyo simama mwanasheria wa serikali na kumvuta tai yake na kumsogeza karibu na sura yangu iliyo jaa ndavu nyingi na nikamuangalia jocho kali kiasi kwamba akabaki akiwa ananitazama kiwoga
“unakwenda au huendi?”
“mmmmm”
 
Nikaishika shingo ya  mwanasheria mkuu na kuinamisha kwenye meza yake kwa hasira na kwa haraka nikachukua peni iliyopo kwenye meza na kuishusha kwa kasi hadi kwenye shabu lake na kuanza kuigandamiza kwa kwa nguvu huku mwili mzima ukiwa unanitetemeka kwa hasira
“nakwenda nakwenda......”
 
Mwanasheria mkuu alizungumza huku akitoa ukelele wa kulia,nikamnyanyua na kumuamrisha kutangulia mbele huku nikiwa ninamfwata nyumba huku nikiwa karibu yake sana endapo atajaribu kukimbia tu ningemfanya kitu ambacho asinge kisahau kwenye maisha yeke.Kila tulipo pita watu walinishangaa na hatua chache kabla mwanasheria wa serikali hatujafika kwenye maegecho ya magari akachomoka kwa kasi akikimbia kitendo kilichonifanya na mimi kukimbia kwa kasi zaidi yake na uzuri wenyewe yeye ni mnene na anakitambi likubwa
 
Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi mwao huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana yoyote na john akabaki akiwa haamini kitu alicho kiona....
 
Itaendelea....
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 27 & 28 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 27 & 28 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 00:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.