RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 5 & 6 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi: EDDAZARIA G.MSULWA


ILIPOISHIA
 “Samahani kaka sijui wewe ni nani mwenzangu?”
“Unaniuliza mimi ni nani ndani ya nyumba yangu?”
Moyo ukanipiga paaaa kama jiwe lililotua juu ya bati tena la nyumba ya uswahilini.Nikajua jamaa anaweza akawa mume wa Madam Mery mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio pale jamaa alipoanza kupiga hatua za kwenda chumbani kwa Madam Mery kwani boxer na tisheti ya shule vyote vipo ndani ya chumba hicho na vipo sehemu ya wazi kwa mtu yoyote anayeingia lazima ataviona,na kingine kilichozidi kunipagawisha ni kitanda nilivyo kiacha kimevurugika kwani kinaonyesha hivi hivi kilikuwa ni kiwanja cha mechi za wakubwa

ENDELEA
    Jamaa kabla hajafunua pazia ili aingie ndani simu yake ikaita.Akaitoa kwenye mfuko wa suruali kisha akaipokea na kuanza kuzungumza mazungumzo ambayo yalianza na ndio bosi.Jamaa akanitazama kisha akatoka nje nikahisi mazungumzo yake ni muhimu sana na ya siri sana ndio maana akatoka nje huku begi lake akilivua na kuliweka pembeni ya mlango wa kuingilia chumbani kwa Madam Mery.

Ikawa nafasi kwangu kuingia chumbani nikachukua kila kilicho changu huku shuka lililo changungaka nikilitoa na kulisokomeza mvunguni mwa kitanda na kuliacha godoro likiwa na foronya yake tu pasipo kuwa na shuka,Nikarudi hadi sebleni na kumuona jamaa akirudi ndani kwani mlango aliuacha wazi kidogo.Ikanibidi boxer yangu niiweke mfukoni mwa suruali yangu huku tishet yangu nikiwa nimeishika mkononi huku nikitaka kuivaa
 
“Dogo unakwenda wapi?”
“Ehee”
”Hujasikia…! Unakwenda wapi?”
“Kununua vitafunio vya chai”
“Dogo mbona unajifanya mjanja sana?”
Maswali ya jamaa yakazidi kunichanganya akili na kunizidisia presha ambayo sikuelewa kama inapanda au inashuka.
“Mjanja wa nini brother?”
“Huendi kununua vitafunio ila sema ninakwenda kununua vitafunwa kwani vitafunio ni hayo meno yako”
“Sawa bro nimekuelewa”
“Ehee kwanza hujaniambia wewe ni nani? Nakuona upo upo tu humu ndani?”
 
“Mimi ninaitwa Eddy”
“Yuko wapi Mery?”
Nkaanza kufikiria cha kumjibu huku maswali mengine nikijiuliza mwenyewe na kujijibu mwenyewe ndani ya moyo wangu hadi nikapata muafaka wa nijibu nini
“Amelazwa kwenye hospitali ya shule”
“Lini?”
“Leo asubuhi”
Lengo la kumjibu jamaa kiufasaha kila swali analo niuliza ni ili akienda kumuangalia Madam Mery iwe nafasi ya mimi kuondoka katika nyumba hiyo ili nikatafute hata sehemu ya kuishi nikisubiria siku zangu za kusimamishwa masomo ziishe
 
“Powa dogo vaa tisheti yako unipeleke huku alipolazwa”
Sikuwa na ujanja zaidi ya kuivaa tisheti yangu na kumalizia kuvaa viatu vyangu na kitu kilichozidi kuniweka mpole mbele ya jamaa ni pale alipoitoa bastola yake na kutazama kama inarisasi za kutosha kwenye magazine yake na kuirudisha kiunoni bastola yake huku akionekena kuridhika na risasi zilizomo.

Safari ikaanza huku sote tukiwa kimya ila mimi nimetangulia mbele kama hatua moja huku yeye akifwatia kwa nyuma.Akili yangu ikawa inanituma nipige hatua za haraka haraka na kama kuna uwezekano nikimbie kwani vichochoro vyote ninavijua katika mji huu wa Arusha
“Dogo nasikia kuna majambazi sana wamezuka kipindi cha hivi karibuni?”
 
“Kusema ukweli bro mimi mwenyewe ninasikia sikia ila sina uhakika kivile.Ila ni juzi kuna benki pale mbele ilivamiwa na pesa zote zikaibiwa”
“Dogo subiri ninunue P.K hapa dukani si utakula?”
“Ndio”
 
Jamaa akaingia kwenye moja ya duka,nikamchungulia kwenye duka hilo nikamuona yupo bize na muuza duka.Nikaanza kupiga hatua za taratibu huku nikizuga zuga watu waliopo katika eneo hilo wasistukie kitu chochote ili nikifika mbali na duka hilo nianze kukimbia.Kabla sijafika mbali kidogo gafla nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma.Nikageuka na kukutana na muuza mahindi
“Oya broo yule jamaa pale mjeda ameniambia nikuletee maindi uchague”
 
Nikatamani nimtukane muuzaji wa watu ila nikaona hana kosa taratibu nikaanza kuyatazama mahindi yaliyo chomekwa kwenye spoke za baiskeli zipatazo kumi na kuunganishwa katika mti mmoja.Nikachagua muhindi laini laini kwani sikuwa nimekula kitu cha aina yoyote tangu asubuhi.Jamaa akaja hadi tulipo akatoa noti ya elfu kumi na kumpa muuza maindi na kumuambia chenchi akae nayo
“Aisee kamanda wangu Mungu akubariki sana”
 
Muuza maidi alizungumza kwa lafudhi ya kichaga huku akipiga saluti na kumfanya jamaa acheke ila mimi sikuwa na hata hamu ya kuyakenua meno yangu.Tukaendelea na safari ya kwenda katika hospitali ya shule ambayo haikuwa mbali sana na shule kwani ilikuwa pia inatoa msaada wa kuwahudumia wananchi wa kawaida tofauti na wanafunzi
 
Tukafika hospitalini na tukakutana na Madam Rukia akiwa nje ya wodi ya wagonjwa,nikamsalimia nikabaki nikiwatazama jinsi  anavyo salimiana na jamaa huku wakicheka kwa furaha na kuonekana wakifahamiana kwa muda mrefu
“Huyo mwenzako anaendeleaje?”
“Kidogo joto lake limeshuka kwani asubuhi hali yake haikuwa nzuri kivile”
“Tatizo lake ni nini haswa?”
 
“Maleria alikutwa na vidudu sita ndio vimemlaza.”
“Sasa mbona umekaa huku nje?”
“Nilitoka mara moja kupunga punga hewa ila twende ukamuone”
Wakati wote wanazungumza nilikuwa kimya nimetulia kama maji ya mtungini huku moyoni nikifurahia jamaa aingie ndani na mimi niondoke .Jamaa na Madam Rukia wakaanza kuingia ila jamaa akasimama na kuniangalia
“Oya dogo twende ukamuangalie mgonjwa”
 
“Huyu mwalifu umemtoa wapi?”
Madam Rukia alimuuliza jamaa na kumfanya atabasamu ila kwangu nikazidi kuogopa,cha kumshukuru Mungu jamaa hakulijibu swali la Madam Rukia kwani tayari tulishafika ndani ya chumba alicholazwa Madam Mery.Jamaa akakaa kitandani na kumkumbatia madam na wote kwa pamoja wakawa wanatokwa na machozi ya furaha,sikujua kinacho waliza ni nini
 
Wakaachiana huku jamaa akianza kumfuta Madam Mery machozi kwa kutumia kitambaa chake na kunifanya roho yangu kuanza kuhisi maumivu ya wivu
“Lucka mdongo wangu ni wewe?”
 
“Ehee….!”
Nikajikuta nikihamaki hata kabla jamaa hajamjibu Madam Mery nikamfanya Madam Rukia kunitazama kwa jicho kali lililoashiria kunionya nifunge domo langu
“Ndio dada yangu ni mimi kwanza pole kwa kuumwa”
“Asante za huko Pakistani?”
“Dada huko kusema kweli si kwema ni kudra za mwenyezi Mungu miaka yote saba tuliyokuwepo kule ni kwa rehema za Mungu”
 
“Kweli hilo ni la kumshukuru Mungu mdogo wagu kwani kila siku nilikuwa nafuatilia taarifa ya habari kujua mnaendeleaje ila sikuwa ninapata majibu kamili”
“Yaani dada maisha ya kule ni bunduki mkononi wakati wote.Kuisikia milio ya risasi ni kitu cha kawaida”
“Sasa mbona walikuongezea miaka miwili ya kuishi?”
“Dada jeshini ni kufwata amri tuu huwezi kujiamulia kuwa nataka hichi hichi sitaki”
 
“Basi miaka mitano ilipoisha nikawa kila mara ninakwenda makao makuu yenu.Basi wakawa wananizingua hadi baba yake huyo kijana (Eddy ) ndio alinisaidia katika kujua taarifa zenu kidogo matumaini ya kukuona yakarudi upya kwani nilidhani umefariki ndio maana wakawa wanakataa kuniweka bayana”
“Baba yake Eddy ni nani pale makao makuu?”
 
“Ndio mkubwa wa sasa hivi katika makao makuu yenu,Baada yule mliye muacha si aliugua kansa ya damu na kufariki”
“Ahaa sasa Napata picha unajua nilipomkuta Eddy kule kwako sura yake nikwa ninaifananisha na sura ya Mzee Godwin yaani hadi ongea zao zinafanana”
 
“Tena wamefanana sana.Eddy huyo ni mdogo wangu wa damu baba mmoja mama moja na tupo wawili tu kwetu”
 
Hadi wakati huo sikuwa ninaamini kama jamaa ni mdogo wake Madam Mery mawazo na fikra zangu zote zilipelekea mimi kujua ni mume wake na kwajinsi alivyokuwa akini hoji hoji maswali yake yaliyokuwa yakinichanganya

“Nashukuru kukufahamu bro Lucka”
“Alafu mzee wako alinipigia ule muda niliokuwa ninazungumza naye akaniambia nimuandalie mazingira kwani kesho au kesho kutwa anaweza kuja kukutembelea”
 
Mawazo yakarudi upya,Tena ya safari hii yakazidi kunichanganya kabisa kwani mziki wa mzee ninaujua mimi mwenyewe na hapa nilipo ndio kwanza nina siku moja tangu nisimamishwe shule kwa wiki moja
 
“Alafu Madam Rukia uliniambia Eddy ni mualifu?”
“Tena mualifu sana mwambie mwenyewe akusimulie”
Madam Rukia kama kawaida yake ya kuwachochea wanafunzi ndivyo alivyofanya kwa Lucka.Ikanilazimu nimuhadisie mkasa mzima kuanzia wakati wa sherehe hadi waliponipa barau ya kusimamishwa wiki moja
 
“Huyo mwalimu aliye kuchapa fala kweli kwani mtu ni lazima kukaa hadi mwisho wa sherehe?”
 
Kauli ya Lucka ikamfanya Madam Rukia kunyamaza  huku akionekna kutopendezwa na Lucka kunitetea mimi
 
“Hata mimi nashangaa yule Sir sijui anakisa gani na mimi”
“Haya Eddy amka twende nikupeleke shuleni.Dada zangu jamani nitakuja muda si mrefu ndoja huyu raia nikamkabidhi kwa waalimu wake waliomsimamisha.Alafu Rukia vipi lile ombi langu la kukuoa?”
 
“Nilikuwa nakusubiri ni wewe tu kupeleka posa kwetu”
Wote wakacheka natukatoka nje ya hospitali na kuelekea hadi shuleni.

Moja kwa moja jamaa akanipeleka katika ofisi za mkuu wa shule hii ni baada ya kumuonyesha zilipo ofisi hiyo.Kwa bahati nzuri tukamkuta mkuu wa shule tena akiwa pamoja na mwalimu Kikole katika ofisi yake,akasalimiana nao kisha wakamkaribisha kukaa katika kiti ila kaka Lucka akasimama na kuniomba mimi nikae katika kiti hicho
 
“Samahani mzazi wa Eddy hatutoweza kuizungumzia kesi ya mwanao kwani muda wake wa kutumikia adhabu yake haujapita”
 
Head master alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Lucka ambaye kwa jinsi sura yake alivyoiweka katika hali ya umakini nikahisi mkuu wa shule pamoja na Mr Kikole waliogopa
 
“Sikuja kusikiliza kesi yake ila nimemleta aendelee na masomo sawa”
 
“Ila kijana wako ni mkorofi”
Mr Kikole alidakia na kumfanya kaka Lucka kumtazama kwa jicho la hasira
“Siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa kwahiyo funga bakuli lako”
 
Jibu la Kaka Lucka alilomjibu Mr Kikole likanifanya nicheke na waalimu wote wakanitazama huku mwalimu mkuu akionekana kuto kupendezwa na jibu la Kaka Lucka
 
“Nimetoka jeshini nimeacha shughuli muhimu za kufanya na sijaja kupoteza muda cha msingi ni kumrudisha dogo darasani sawa”
 
Head master akatingisha kichwa akionekana kukubaliana na kaka Lucka japo Mr Kikole alionekana kukasirika
“Eddy yule mwalimu aliyekuchapa ni yupi?.Nionyeshe ili niondoke naye nikamuhoji kambini?”
 
Moyo wangu ukaingia furaha huku nikimtazama Mr Kikole nikamuona jinsi anavyohaha haha huku akiwa anatamani kuondoka katika ofisi hiyo.Mr Kikole akaanza kunikonyeza pasipo Kaka Lucka kumuona  ili nisimtaje
“Bro achana naye bwana”
 
“Si alikuzalilisha mbele ya wanafunzi wezako ngoja na mimi nikamzalilishe kambini”
 
Kusema kweli mwalimu Kikole anatetemeka hadi nikahisi kaka Lucka anaweza kumgundua ni yeye.Nikamtazama katika suruali yake nikaona jinsi inavyoanza kuchora ua lisilo na umbo maalumu kwani haja ndogo inaanza kumtoka hadi nikajikuta nikimuonea huruma.Kaka Lucka akatoa simu yake na kuiminya minya na kuiweka sikioni
 
“Ndio mkuu”
“Nimemfikisha dogo hapa shule hapa nasubiri anitajie huyo mwalimu aliyemdhalilisha na pia ningekuomba uwasiliane na mkuu wa hapaArusha ili aniletee vijana wawili na defender moja”
 
Mazungungumzo ya kaka Lucka yakazidi kumchanganya Mr Kikole hadi nikashuhudia haja ndogo ikianza kuchuruzika kwenye kapeti lililopo katika ofisi ya mkuu wa shule
“Eddy nionyeshe fasta fasta niondoke naye si unajua nipo kwa muda maalumu hapa”
 
“Kaka hebu tufanye kama umemsaehe kwani mmmmmm”
Nilizungumza huku nikicheka na kumfanya kaka Lucka kunitazama huku akinishangaa
“Dogo unacheka ?.Alafu mbona mzee unatetemeka kiasi hicho ni wewe nini?”
 
Kaka Lucka alizungumza huku akimpiga piga Mr Kikole kwenye bega lake cha kumshukuru Mungu hakumuangalia chini kwani Mr Kikole alikuwa amekaa kwenye kiti ambacho kinatazamana na mimi na hali yake ya hewa ilisha haribika muda mrefu.Nikamshika mkono Kaka Lucka na kutoka naye nje ya ofisi huku nikiendelea kucheka
 
“Eddy mbona unacheka kiasi hicho”
“Kaka ticha mwenyewe ni yule mzee pale uliyekuwa unampiga piga bega”
“Haaa sasa mbona hukuniambia nikamnyanyua nimchangamshe damu kwa kichura chura?”
“Ohhh mwenzako pale alipo kojo nje nje”
“Amejikojolea?”
 
“Ndio”
“Masikini mzee wa watu,nilikuwa nawachimba biti kumbe muhusika yupo  pale?”
“Ndio”
Sote tukajikuta tunacheka ila mimi nilizidi kucheka hadi machozi yakaanza kunimwagika.tukaagana na kaka Lucka akurudi zake hospitali kisha mimi nikaelekea darasani.Kabla sijafika darasani kuna mwanzafunzi akaja kuniita
“Head master anakuita”
 
“Yupo wapi?”
“Ofisini kwake”
Sikuwa na wasi wasi,nikaanza kwenda ofisni kwa mkuu wa shule nikamkuta yupo peke yake huku Mr Kikole akiwa hayupo,Nikakaa atika kiti ambacho nilikuwa nimekalia hapo awali na kutazamana na mkuu wa shule huku miwani yake akiiweka vizuri
 
“Kijana nataka kukuambia kitu kimoja tu na ukiweke akilini na ukishike……..Usione kuwa tumekukubalia urudi shule kabla ya muda wa adhabu yako kuisha ukadhani tumekuogopa.Sasa ni hivi utafanya kazi ya kuchimba mashimo 15 ya taka hadi jumamosi adhabu yako itakapokwisha na utafyeka kila eneo la shule lenye nyasi ndefu.SAWA”
 
Nikamtazama mkuu wa shule kwa macho ya dharau huku nikiwa ninajiamini na kumfanya mkuu wa shule kuikunja sura yake huku akianza kuhema kwa hasira.Nikajikuta ninamuuliza mkuu wa shule swali
“Mbona hukuzungumza hivyo wakati kaka yangu yupo hapa?”
 
Mkuu wa shule akasimama kwa hasira huku akiuvua mkanda wa suruali yake akitaka kunichapa
“Wewe ni mshenzi kweli lala chini”
 
Ikanibidi kuwa mnyonge nikamuomba msamahaa mkuu wa shule hadi akanielewa na tukakubaliana adhabu ya kuchimba mashimo ianze kesho asubuhi.Nikafika darasani na kuwakuta wezangu wakijisomea.Wakanishangaa kuniona ninaingia darasani
 
“Oya Eddy si tumetangaziwa una Sas P ya wiki moja?”
John aliniuliza huku akinipisha kwenye kiti changu ninacho kalia darasani huku yeye akihamia kwenye kiti kingine
“Kesi imeisha juu kwa juu ila nimepewa adhabu ya kuchimba mashimo……Ehee nipe stori vipi yule Salome umebonga(Zungumza naye) naye?”
“Yule dogo anajisikia sana kama vipi kamdai zile pesa zako ulizo mpa”
 
“Hebu acha masihara ndugu vipi aliniulizia?”
“Akuulizie wewe ni nani?,Mbaya zaidi dogo nasikia anapigwa na yule jamaa aliye cheza naye ila sasa hii dogo tunapishana kama magari mabovu NO salamu”
“Nikumbushe baadaye nikusimulie kilicho mkuta Mr Kikole”
“Huyo msen** leo pia kanichapa zamu si yake ila ana kihere here kama amenyimwa penzi na mkewe”
“Yule si kiherehere ngoja nitakuambia wewe mwenyewe utacheka hadi mbavu zikuume”
 
Tukaendelea kuzungumza na John hadi muda wa kutoka darasani mchana ukafika.Kendele ya chakula ikagongwa ikiashiria kidato cha tano wote tukachukue chakula.Tukaelekea katika sehemu ya kuchukulia chakula na tukapanga foleni kama walivyo panga wanafunzi wengine wa kidato chetu tulio wakuta
 
“Samahani ninaweza kukaa mbele yako?”
Nikageuka na kumkuta ni Salome ndio anaye niongelesha,nikasogea kidogo akapita mbele yangu kwa jinsi mstari wa chakula watu walivyo banana nikajikuta karoti yangu iliyoanza kusimama ikigusa makalio ya Salome na kumfanya ageukegeuke nyuma na kuniangalia usoni huku akitabasamu akionekana akifurahi kwa jinsi ninayomgusagusa na koroti yangu katika makalio yake yaliyo makubwa kiasi

                        ******SORY MADAM******(6)

Mstari wa chakula ukaanza kusogea taratibu kuelekea mbele huku mimi na Salome tukiwa kimya hakuna aliyemsemesha mwenzake.Ikanibidi niukate ukimya
“Salome leo tunaweza kuonana?”
“Saa ngapi?”
“Kabla ya prepo”
“Sawa nitaangalia kama kuna uwezekeno”
“Nitashukuru sana.Ila vipi shemeji hajambo?”
“Hajazaliwa bado”
“Acha kuniongopea”
 
“Kweli shem wako bado hajazaliwa”
Kabla sijazungumza kitu chochote akaja kaka mkuu sehemu tuliyo simama katika mstari na kunifanya nikae kimya
“Ahaa Salome mbona umepanga mstari si ungepita mbele?”
“Naogopo yule prefect(kiongozi) anayesimamia pale mkali kama nini?”
“Twende nikupitishe wewe ni mtu mkubwa bwana hapa shule”
 
Jamaa akamshika mkono Salome na kumtoa kwenye mstari na kuondoka naye kitendo ambacho kimenikera kupita maelezo kwani kaka mkuu kanipeperushia ndege wangu.Nikiwa najifikiria kupita na mimi mbele ili niwahi kuchukua chakula na kumfwata Salome ili tuzungumze vizuri jamaa mmoja wa kidato cha tano akaja sehemu niliyo simama
 
“Oya Eddy unaitwa na mwalimu wa nidhamu”
“Yupo wapi?”
“Ofisini kwake”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kwani katika waalimu ninao waogopa katika shule hii ni mwalimu wa nidhamu ambaye anaonekana kutokuwa na masihara na mwanafunzi wa aina yoyote.Nikampa vyombo vyangu John anishikie huku nikianza kujichunguza kuanzia miguuni hadi kwenye shati.

Sikuwa nimevaa sare za darasani kwani tangu juzi sikwenda bwenini zilipo nguo zangu.Niaanza kuelekea katika ofisi za nidhamu.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio zaidi baada ya kuliona gari la baba aina ya Hammer wanayo tembelea wakuu wa jeshi huku dereva wake akiwa ndani ya gari hilo.Nikaenda kumsalimia dereva kutokana ninajuana naye,
“Shikamoo brother P”
“Marahaba vipi Eddy?”
 
“Safi vipi home munaendeleaja?”
“Tunaendelea vizuri vipi masomo?”
“Safi,vipi mzee mbona kaja fasta fasta kwema”
“Kwema yupo huko ofisini kwenu’’
Nikajaribu kumchunguza dereva kuniambia juu ya mzee kama amekasirika au laa ili niweze kujiandaa kwa chochote kwani mzee(baba) kurusha ngumi kwake ni kitu cha kawaida sana.Nikaachana na dereva na kwenda ofisini.Nikamkuta baba akiwa na Mwalimu wa nidhamu Mr Karata wakiwa wanazungumza maswala yao huku wakicheka .Nikawasalimi kwa pamoja wakaniitikia huku sura zao zikiwa na tabasamu
“Oohh my first born how you?”(Ooh mtoto wangu wa kwanza hujambo?)
 
“Am fine dady”(Nipo sawa baba)
“Why your looking so scare what’s wrong of you?”(Mbona unaonekana kuogopa,Una tatizo gani?)
“Nothing dady”(Hakuna kitu baba)
 
“Ok be happy my son”(Sawa kuwa na furaha mwanangu)
Nikaweka tabasamu usoni mwangu huku nikiwa ninashangaa leo baba anafuraha na mimi wakati katika vipindi vyote alivyokuwa akinitembelea shuleni alikuwa kauzu hadi waalimu wakawa wanashangaa ni maisha gani ambayo tunaishi na baba yangu na sheria nyingine ya baba akianza kuzungumza kingereza ni lazima na mimi nimjibu kwa lugha hiyo hiyo
 
“Hapa nilikuwa nazungumza na mwalimu wako akinielezea kisa chako cha kuvunja fimbo ya mwalimu”
Nikakaa kimya huku nikimtazama mwalimu wa nidhamu huku kimoyo moyo nikimlaani ni kwanini amemuadisia baba yangu juu ya mkasa huo kwani hashindwi kunichapa mikanda mbele yake
 
“Mwanangu usiwe mkorofi sawa first born”
“Sawa baba nimekuelewa”
“Mimi nilikuja kukutembelea mara moja kwani wiki ijayo ninakwenda Iraq kwa ajili ya kazi maalumu huko tunakutana wakuu wa majeshi wa nchi mbalimbali nitakaa mwaka mmoja na nusu”
 
“Sawa na mama anarudi lini?”
“Mama yako anarudi kesho kutwa”
“Atakuja huku kunitembelea?”
“Nitamwambia aje kukutembelea ila cha msingi hakikisha unasoma kwa juhudi matokeo yako mwalimu hapa nimempatia Email yangu kila ripoti yako ya masomo atakuwa ananitupia…Sasa kazana na kusoma sawa?”
“Sawa baba”
 
Baba akatoa pesa na kunipa laki tano za matumizi ya kipindi chote ambacho nitakuwepo shule.Mwalimu wa nidhamu akaomba anishikie laki nne ili kuepuka kuibiwa,Sikuwa na ubishi nikampatia laki nne na nusu nikabakiwa na elfu hamsi nikachanganya na pesa nyingine nilizokuwanazo.Baba akanipa simu mbele ya mwalimu wa nidhamu japo sheria za shule haziruhusu mwanafunzi kuwa na simu
 
“Sasa Eddy uwe makini na simu yako ili waalimu wengine wasiione wakakupokonya kwa mimi ninakuruhusu kuwa nayo”
 
Mwalimu wa nidhamu alizungumza huku akiwa anajichekesha chekesha baada ya kupewa laki moja na baba ila sikujua ni ya nini.Baba akaniombea ruhusa ya kwenda na mimi nje ya shule.Baada ya kuipata ruhusa hiyo tukaondoka shule na kwenda katika hoteli moja iliyopo karibu na shule.Tukanunua chakula tukiwa na dereva wa baba tukaanza kula huku mara kwa mara mzee akinihusia kusoma kwa juhudi huku akinipondeza kwa kumbishia mwalimu
 
“Wale waalimu wenu wanaonekana wana tabu sana.Ila wakikuzingua kwa kosa ambalo utaona hawakutendei haki wewe wazingue.Ila wakiniletea kesi ambayo ni ya kijinga jinga kama umekamatwa na demu sijui umegoma kufanya mtihani jua nikirudi nitakuvunja kiuno tumeelewana?”
“Sawa baba”
 
Baba akaniomba nimpeleke katika hospitali ya shule akamuone Madam Mery.Tukafika katika hospital ya shule tukamkuta Madam Mery akiwa na kaka Lucka ambaye baada ya kumuona mzee akampigia saluti.Wakazungumza na Madam Mery huku mazungumzo yao akimuhimiza anifwatile sana katika masomo yangu huku awe anampa taarifa kwa kila kitu nitakachokuwa ninakifanya
 
Tukatoka hospitalini mida ya saa moja kasoro usiku baba na dereva wakanipeleka nyumbani kwa Madam Mery kuchukua madaftari na vitabu vyangu kisha wakanirudisha shuleni na kuagana nao wakaondoka mimi nikaelekea zangu bwenini.
“Oya Eddy kuna kiji message chako hapa”
“Kimetoka kwa nani?”
“Aliye nipa ameniambia nisikuambie”
Baraka akanipa kikaratasi nikakifungua na kukuta ujumbe ulio andikwa kwa mwandiko wa kike
{Naomba tuonane kabla ya prepo kwenye kordo ya madarasa ya Arts ‘S’}
 
Nikatambua kuwa ni Salome kwani tulipanga tuonane katika muda kama huo.Nikajiandaa haraka haraka na kumpa taarifa John anayeonekana kutokuamini kwa kitu ninacho kizungumza.Tukafika katika madarasa ya Arts tukawakuta Salome na rafiki yake wakiwa wanatusubiria.Tukasogea pembeni na Salome na kuwaacha John akiwa amesimama na Claudia
“Salome nashukuru kwa kukubali ombi langu la kuonana na mimi hapa”
 
“Eddy hauna haja ya kushukuru wakati hata mimi ninapaswa kukushukuru kwa msaada wako wa pesa ulionipatia majuzi kwani bila wewe wala nisingeweza kushiriki mashindano ya umiss na kushinda”
“Hakuna tabu vile ni vitu vya kawaida…..Salome na….”
Kabla sijazungumza kitu nikamuona mwalimu wa zamu akija eneo tulilo simama na ikabidi tubadilishe mada
“G.S(General study) sijaandika naomba uniadhimishe daftari lako”
Salome akafungua begi lake na kujifanya anatoa daftari la somo nililomuomba huku tukimsubiria mwalimu wa zamu apite
“Eddy nenda darasani kwenu muda wa kujisomea sasa acheni stori”
 
“Sawa ticha hapa nimekuja kuazima daftari la G.S”
Mwalimu akapita na kutuacha na kutuacha tumesimama na Salome.
“Salome kama hutojali njoo class kwetu mida ya saa tatu tatu”
“Powa nenda na hili daftari ili nipate kisingizio cha kuja Class kwenu”
Tukaachana na Salome kila mtu akaelekea darasani kwao
“Eddy nimempiga Sound Claudia amenikubalia”
“Wee”
“Chezea mimi,dogo ameniambia kesho tuonane”
“Haya mwaya”
“Vipi na wewe huyo miss wako amekukubalia?”
“Yule kwangu haruki mimi ndio Eddy mwengine photocopy”
“Mmmmm unaweza ukawa unajiproud bure kumbe domo zege”
 
“Haya mimi si domo zege utaona”
“Nitaona nini sasa?”
“Twende darasani tuachane na hizo mada”
Tukaingia darasani na kila mmoja akakaa sehemu yake na tukaanza kusoma huku akili yangu ikihesabu masaa ya Salome kuja darasani kwetu kuchukua daftari alilonipa.Mida ya Saa tatu kasoro Salome akaingia darasani kwetu na kuwafanya watu wengine kushangaa huku wengine wakimpongeza kwa ushindi nikawa najiuliza kwani siku zote hawakumuona ili wampepongezi
 
Salome akafika katika meza yangu,Nikachukua kiti ambacho hakina mtu na kmuwekea pembeni.Salome akakaa na kumfanya John akibaki akisikitika huku akinikonyeza
“Eddy unasoma nini?”
“Nisome wapi hapa nilipo nilikuwa ninahesabu muda wa wewe kuja”
 
“Acha kunichekesha Eddy unataka kuniambia saa zote hujasoma kitu hata kimoja?
“Kweli sijasoma hapa pia nashukuru kukuona hapa”
Salome akaanza kucheka kwa sauti ya chini hapo ndipo nikapata fursa ya kumchunguza vizuri na kukubali kimoyo moyo kwamba Salome ni mzuri kwani kila kitu kilichokaa katika mwili wake kimekaa kwa mpangilio
“Eddy mbona unanitazama sana?”
“Salome sio siri wewe ni mzuri yaani mpaka unafanya moyo wangu unauma”
 
“Eddy wewe muongo”
“Kweli yaani kila nikikuangalia mwili wangu unasisimka”
“Asante ila hata wewe pia ni  mzuri.”
“Mzuri wapi best”
“Wewe hujioni ila sisi tuna kuona ndio tunajua wewe ni mzuri”
“Salome kusema ukweli ninakupenda japo wewe upo na kaka mkuu”
“Hapana yule si mpenzi wangu”
“Ila ni nani yako?”
“Yule jamaa alinitongoza ila kwa muda mrefu sikumpa jibu lake”
 
“Mmmm haya sisi yetu macho”
“Kwa nini yenu ni macho?”
“Sisi tulio wabaya tutaishia kufaidi tu kwa mimacho yetu”
“Ila usijali mbona hata wewe unaweza kuf……”
Kabla Salome hajamaliza kuzungumza kitu chochote gafla umeme ukakatika na watu wakaanza kushangilia.Salome akanisogelea na kunipiga busu la haraka la mdomoni na kunifanya mwili wangu kusisimka kwa raha
“Eddy twende zetu huku”
 
Salome akanishika mkono na kuanza kutoka darasani huku kukiwa na giza totoro ila wenye tochi zao waliombwa kuzizima na watu wenye kufanya yao na mademu zao.Tukafika katika vyoo vya shule na kuingia katika vyoo vipya ambavyo havijaanza kutumika.Tukaanza kunyonyana denda huku kila mmoja akionekana kuwa na humu na mwenzake japo kuna giza ila nikajikuta nikijiamini.Nikaipandisha sketi ya Salome juu na kumvua nguo yake ya ndani huku na yeye akinivua suruali yangu kwa haraka
 
Kidole changu kimoja nikakiingiza katika mgodi wa Salome na kuanza kukichezesha na kumfanya Salome kuanza kutoa miguno ya raha huku naye akijitahidi kuanza kuichua karoti yangu,Sikutaka kupoteza muda nikaunyanyua mguu wake na kuushika na mkono mmoja kisha karoti yangu ikazama ndani ya mgodi na kuanza kuuchimba.Salome akanza kutoa miguno huku mara kwa mara nikimnyonya denda ili kuepuka kelele zake zisikike nje japo vyoo hivyo vipo mbali kidogo na madarasa.Nikazidisha kasi ya kuchimba kisima na kumfanya Salome alie kama mtoto mdogo
 
Gafla tukajikuta tunakatisha zoezi baada ya kusikia mtu akifungua milango ya vyoo vya mwanzo na hapo tulipo ni choo cha tano kutoka choo cha kwanza.Salome akaanza kutetemeka huku akianza kuvaa nguo zake.Nikapandisha suruali yangu haraka haraka na sote tukaanza kuskilizia ni nani anafungua katika vyoo tulivyopo.

Tukaanza kuuona mwanga wa tochi kwa kupitia uwazi wa mlango ukija katika choo tulichopo huku miguu ya mtu huyo ikizidi kusogea karibu na choo tulichopo.Tukasikia mtu huyo akigusa kitasa cha mlango wa choo tulichopo na kuanza kukivuta
 
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio na kujikuta nikianza kuomba sala ya kuniepusha na kukamatwa kwetu kwani ni muda mchache uliopita baba alitoka kunionya kwa ujinga kama huo.Nikamtazama Salome na taratibu nikamuona mwenzangu akilegea kabla hajaanguka nikamuwahi kumkumbatia ili asianguke chini na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.....

ITAENDELEA.....  

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 5 & 6 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 5 & 6 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by Unknown on 20:06:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.