Nane nane inavyonogeshwa na mkongwe Benki ya Posta

 
Sikukuu ya wakulima inayofahamika kuwa Nanenane ina sherekewa nchini kote tarehe 8 Agosti kila mwaka.
Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na Shirika la Chama cha Kilimo Tanzania (TASO)na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo. Miaka iliyopita sherehe hizi zilikuwazikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.

Sherehe hizo zilifanywa Julai Saba ya kila mwaka , kuchukua nafasi ya sikukuu ya sabasaba iliyokuwa ikiadhimishwa kusherehekea siku ya Tanu, chama kilicholketa uhuru wa Tanganyika. Kwa hiyo utaona kwamba kwa miaka takriban 15 (1961 – 1976) Watanzania Bara walikuwa wakiendelea kusherehekea kuzaliwa kwa TANU kila tarehe saba ya mwezi Julai, lakini mara tu baada ya kuzaliwa kwa CCM ikabidi sherehe za Saba Saba zibadilishwe na kuitwa ‘Sikukuu ya Wakulima’, lengo likiwa ni kuhimiza sera ya serikali kwa wakati huo ya ‘Siasa ni Kilimo’.

CCM ilizaliwa Februari 5, 1977 vilipounganishwa vyama vya Afro- Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar n tanu cha Tanzania Bara na kuzaliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili Tanzania itawaliwe na chama kimoja tu cha siasa baada ya nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar) kuwa zimeungana Aprili 26, 1964. Ikumbukwe kwamba ASP nayo ilizaliwa Februari 5, 1957 kama ilivyokuwa kwa Azimio la Arusha lililohimiza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambalo lilizaliwa Februari 5, 1967.

TANU ndicho chama kilichotawala nchi baada ya uhuru wa Desemba 9, 1961 Saba Saba ya miaka hiyo ilikuwa na maana halisi ya kuhimiza ‘Siasa ni Kilimo’, kwa sababu katika maonyesho ya kiwilaya, kimkoa na kitaifa, wakulima walionyesha mazao halisi ya kilimo, wakaonyeshwa pembejeo za kilimo ‘cha kisasa’ na kufundishwa namna ya kutumia pembejeo hizo kwa ustawi wa kilimo na taifa kwa ujumla.

Mjini Dar es Salaam sikukuu hii ilitengewa eneo lake maalum katika Barabara ya Kilwa, ambalo lipo mpaka leo, na huko mikoani kulijengwa viwanja maalum kwa ajili ya maonyesho hayo, watu wakiingia bure kuangalia bidhaa na mazao ya kilimo pamoja na kuangalia pembejeo na kujifunza matumizi yake. Kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele, dhana ya ‘Siasa ni Kilimo’ kilibadilika na kuwa ‘Siasa ya Kilimo’ na wengine wakaitafsiri kama ‘Kilimo cha Siasa’, kwa sababu sikukuu hiyo ilionekana kujaa siasa zaidi, huku watu wakilenga kuitumia kibiashara kuliko maazimio ya awali.

Haikushangaza hata hivyo katikati ya miaka ya 1990 wakati serikali ilipoamua kuwahamisha wakulima kutoka ‘Saba Saba’ na kuwapeleka katika siku nyingine ya ‘Nane Nane’. Lengo la serikali sasa likawa kuitumia Saba Saba kama siku ya maonyesho ya biashara ya kimataifa, ambapo wafanyabiashara wengi walijitokeza ama hujitokeza kuonyesha bidhaa zao wanazozalisha na siyo kuwafundisha Watanzania mbinu za kuzalisha biadhaa hizo.

Kama ‘Siasa ni Kilimo’ ilibadilishwa na kuwa ‘Kilimo cha Siasa’ au ‘Siasa ya Kilimo’, nadhani kuna haja kwa serikali na wadau wote kuketi chini kutafakari wapi tulipojikwaa kabla ya kuanza utekelezaji wa ‘Kilimo Kwanza’, vinginevyo tutaletewa msamiati mwingine wa ‘Siasa Kwanza, ndipo Kilimo’! Awali sikukuu ya Nane Nane ilianza kwa kupooza katika maonyesho ya kwanza yaliyofanyika mjini Morogoro katika eneo la Nane Nane, lakini sasa hali inaonekana kuwa tofauti kidogo.

Kwa sasa Maadhimisho haya husherehekewa katika ngazi ya kanda ambapo kanda ya nyanda za juu za kusini ni katika viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya, Kwa kanda ya Kaskazini, sherehe hufanyika viwanja vya Themi, Arusha , wakati kanda ya Mashariki ni katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Morogoro na Kanda ya Ziwa, zinafanyika Mwanza, Viwanja vya Nyamhongolo na Kanda ya mwisho ni kusini, zinafanyika Ngongo.

Mwaka huu sherehe hizi za nane nane zinafanyika kanda ya Kusini katika viwanja vya Ngongo wakati kukiwa na mabadiliko makubwa katika siasa za Tanzania kuhusu viwanda, nchi ikiwa inaelekea katika kutegemea uchumi wa viwanda kwa lengo la kuongeza thamani katika mnyororo wa bidhaa za kilimo ambazo zinaoneshwa katika maonesho haya. Kuna mabadiliko makubwa katika uendeshaji wa kilimo kwa sasa huku kukiwa na sheria za kuwalinda wakulima dhidi ya mbegu na pembejeo feki, Vipimo feki kwa lengo la kumfanya mkulima kunufaika na kazi zake.

Aidha kwa kauli zake rais John Magufuli kwa watendaji wa halmashauri ya kuwataka wakulima wasimenyeke kisha wanawawekewa tozo ambazo hazijaenda shule, maana yake hazina maana kwa kuendeleza kilimo. Ni dhana sahihi kuwapo kwa maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa lengo la kubadili kilimo kwa kuwapa elimu wakulima na kuwakutanisha wakulima na watu wanaowezesha kilimo kama taasisi za kifedha na masoko .

Moja ya tasisi ambayo inashiriki moja kwa moja ni Benki ya Posta ambayo ina historia kubwa katika taifa hili na sasa inaingia katika kusaidia wajasirimali wanaofanya uchakataji wa mazao ya mashambani. Uwapo wa Benki ya Posta ni sehemu ya mabadiliko yaliyopo hasa ya kuanzishwa kwa taasisi za kufanya uwezekano wa kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.

Benki ya Posta tawi lake la Lindi imepokea kwa mikono miwili dhamira ya serikali ya kuwainua kiuchumi wananchi wake kwa kutoa mikopo yenye mashariti nafuu kwa baadhi ya vikundi vya wajariamali vilivyopo katika manispaa ya Lindi hasa vinavyoshughulika na mnyororo wa thamani katika kilimo. Wakulima wa korosho katika mkoa huu wana nafasi kubwa sana ya kutumia benki hii kuendeleza kilimo hicho hasa kwa kuhakikisha kwamba wanauza korosho iliyomenmywa badala ya ghafi.

Moja ya kundi litakaloshiriki maonesho ya Nanenane la Tujiamini Woman Chashewnut Group kimepata uwezo wa kunua korosho ghafi na kuziongeza thamani kutoka katika mikopo inayotolewa kwa wajasirimali ya Posta.

Kwa maneno mengine benki hii inashiriki moja kw amoja kuwezesha kupatikana kwa kitu tayari kw amlaji badala ya mkulima,kuuza ghafi. Kikundi hiki chenye wanachama 17 kilichoanzishwa mwaka 2014,kinachoendesha shughuli zake za uuzaji wa korosho katika kituo kikuu cha mabasi cha Lindi kimefanikiwa kutokana na Benki ya Posta kuwapatia mitaji wanakikundi kwa riba nafuu.

Katibu wa Kikundi hiki Salma Mmoleambao huuza korosho zilizobanguliwa,anasema mikopo ya fedha inayokopeshwa kwa kila mwanakikundi imeanza kubadilisha maisha yao na kuanza kuwa na malengo na ndoto za kufanya mambo makubwa siku zijazo. Alisema licha yayeye mwenyewe kupandisha mtaji wake kutoka shilingi 500,000.00 hadi kufikia 1,500,000.00 ambazo alikopeshwa na benki hiyo,lakini pia wameweza kukodi banda ambalo muda si mrefu watahamia na kuendeshea shughuli zao.

Alisema mafanikio hayo yametokana na masharti nafuu ya mikopo wanayokopeshwa inayoendana na shughuli za ujasiriamali kutokana na mazao ya mashambani yaani kilimo.Annasema kiwango kidogo cha riba, cha 3% ya kiasi wanachokopeshwa na kuwa hata muda wa kurejesha mikopo ni rafiki.

“Posta wanajali wateja wao wamekuwa wakitutembelea mara kwa mara kwa mara kutupatia ushauri,kila mmoja wetu ana matarajio ya kuwa mfanyabiashara mkubwa na muda si mrefu kila mmoja atasimama na kukopa mwenyewe bila kudhaminiwa,” alisema Salma. Kuna uhusiano mkubwa kati ya kilimo kuwa uti wa mgongo na Benki ya Posta ambayo imekuwa nchini tangu nyakati za wakoloni ikiwahudumia watu wa vijijini.
Zena Hamisi mwenye ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa wa mazao ya kilimo katika mahojiano alisema kikwazo kikubwa wanachokutananacho wajasirimali wadogo ni masharti magumu ya mikopo. Aidha Bakari Hamisi katibu wa kikundi cha NOSTRESS cha Mnazi mmoja manispaa ya Lindi alisema kuwa mikopo ya Benki ya Posta imewasaidia wanakikundi kuboresha na kuongeza mitaji ya biashara zao.

Jamila yusuph alisema mikopo ya bank ya posta inapatikana kwa inamasharti nafuu na marejesho yake yanafanywa bila presha jambo ambalo linamfanya mjasiriamali kufanya biashara kwa amani na utulivu. Jamila alisema kikundi chao cha Busara kilianzishwa na watu wa Benki ya Posta walipowatembelea na kuwapa elimu ya mikopo ndipo walipoamua kujipanga na kuomba mikopo.

Meneja wa Benki ya posta tawi la Lindi Frumence Mushin alisema benki hiyo iliyoanza shughuli zake mkoa wa Lindi mwaka 2007, imekuwa ikitoa mikopo yenye lengo la kuwasaidia wajasirimali kupiga hatua zaidi. Alisema kuna mikopo midogo amabayo inawalenga wajasirimali wadogo na imekuwa na wateja wengi tofauti na awali kutoka ana kuwa na huduma iliyolenga kuhudumia wajasirimali wadogo ambao wanawezeshwa na wakulima kwa kutumia raslimali zinazopatikana mkoani humo.
Nane nane inavyonogeshwa na mkongwe Benki ya Posta Nane nane inavyonogeshwa na mkongwe Benki ya Posta Reviewed by WANGOFIRA on 20:52:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.