LISHE BORA ITASAIDIA KUPUNGUZA UDUMAVU KWA WATOTO IFIKAPO 2025





Kila kuchapo serikali na mashirika mbalimbali uangaika kutafuta suluhu juu ya majanga mbalimbali ya udumavu wa watoto unaochangiwa na lishe duni wanazozipata watoto katika umri chini ya miaka mitano.

Vikundi mbalimbali na watu binafsi nao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamashisha afya bora kwa kila mtu, juhudi hizi pia zinaungwa mkono na dini zote ambazo usisitiza ulaji wa vyakula vinavyojenga na kuimalisha afya za waumini wao.

Lakini bado hali ni tete hasa kwa watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili ambapo udumavu na ukondefu unaosababishwa na kukosa lishe bora uchangia kwa kiasi kikubwa kuwaathiri.
Takwimu za shirika la Afya Duniani WHO, zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 270 walio chini ya umri wa miaka mitano nchini Tanzania hupoteza maisha kwa lishe duni, huku zaidi ya watoto milioni mbili na laki saba wakikabiliwa na udumavu unaotokana na utapiamlo.
 
Hali ni mbaya zaidi kwa kutokana na zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo hutokea katika mwezi wa kwanza wa maisha ya watoto hao. Pia kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani UNICEF, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote wa Tanzania waliochini ya umri wa miaka mitano wamedumaa kutokana na lishe bora.

Katika makala hii tutaangazia jinsi udumavu unavyochangia kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa afya za watoto hali inayopelekea watoto kuwa na afya duni na utapiamlo.

Udumavu hutokana na utapiamlo unaosabibishwa na lishe duni kwa mtoto ambapo huchangia mtoto kuwa na kimo au urefu mfupi usioendana na umri wake.

Takwimu hizo zinaonyesha kupungua kwa kiwango cha udumavu nchini kwa asilimia 30, kati ya mwaka 1994 hadi 2014 japo idadi ya watoto waliodumaa ikiwa imeongezeka kutoka milioni 2.4 hadi 2.7 katika kipindi hicho.

Wataalam wa afya wametaja sababu kadhaa zinazochangia udumavu wa watoto nchini ambapo lishe duni na kuugua mara kwa mara katika miaka mitatu ya mwanzo ya maisha ya mtoto uchangia mtoto huyu kudumaa kimwili na kiakili pia.

Pia, afya na lishe duni kwa wanawake kabla ya ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Wanawake kuwa na kimo kifupi, kutopangilia uzazi na hivyo kuzaa karibu karibu na tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa katika umri mdogo nalo linatajwa kuwa tazizo lingine linalosababisha na kuchangia udumavu nchini.
 
Taratibu duni za ulishaji watoto wachanga na wadogo, ikiwemo watoto kutonyeshwa maziwa ya mama kwa pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa, na kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji yao ya kilishe pale wanapotimiza umri wa miezi sita.

Kwa kufanya hivyo na kupewa kiasi kidogo cha chakula, kupewa chakula kisichokuwa na ubora na kutopewa chakula chenye mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya chakula napo uchochea udumavu kwa mtoto ambapo kwa kiasi kikubwa mwili wake na umri wake hudumaa jambo linalochangia udumavu wa akili pia kwa mtoto huyo.

Athari za udumavu

Udumavu kwa mtoto huchangia kupata athari zisizoweza kurekebishwa katika maisha yake na daima atadumu nazo katika maisha yake yote hata kama kwa hapo baadaye hatapata lishe bora lakini mwili wake tayari ushadumaa na hivyo ni vigumu kukubali marekebisho.

Pia udumavu kwa kiasi kikubwa husababisha kupungua kwa kasi ya maendeleo ya ukuaji wa akili ya mtoto hali inayosababisha watoto kupata matokeo duni kielemu kutokana na lishe bora waliyoipata wakiwa wadogo.

Lakini pia kuongezeka kwa uwezekano wa watoto waliodumaa kuwa na uzito uliowazidi au kiribatumbo, na kuugua magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo moyo, kiharusi, shinikizo kubwa la damu, na kisukali wakati wanapofikia umri wa utu uzima nalo utokana na ukosefu wa lishe duni walioipata wakiwa wadogo.

Maendeleo ya ukuaji wa mtoto kimwili  nao kuwa dhaifu uchangiwa na upatikanaji wa lishe duni hali inayosababisha mtoto kuwa na afya duni na mwonekano mbaya (body structure) ya mtoto hivyo mtoto kuwa na mwili afya duni kutokana na mwili wake kutokuwa nguvu ya kupambana na magonjwa nyemelevu ikiwemo minyoo, kuhara, typhod na mengine mengi.

Nini kifanyike ili kuzuia udumavu nchini?

Lengo kuu la Shirika la Afya duniani kwa Tanzania ni ifikapo mwaka 2025 walau idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa iwe imepungua kwa walau kwa asilimia 40. Hivyo ni muhimu kwa jamii ya watanzania kuzingatia lishe bora kwa watoto na mama mjamzito na kulinda afya yake katika kipindi chocho cha mimba hadi katika kipindi cha unyonyeshaji.

Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa wanawakuwa katika hali nzuri ya lishe wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha baada ya kujifungua hii itasaidia kupunguza au kuondoa kabisa kero hii ya udumavu kwa watoto wa kitanzania ambao ni taifa la kesho naa hapo baadaye watakuwa viongozi bora katika nchi hii na duniani kiujumla.

Ni muhimu kwa wakina mama kunyonyesha watoto wao maziwa hadi watakapofikia miaka miwili, hapa wanaawake wajitahidi na waache uzembe wa kuwaachisha watoto wao mapema kwa kisingizio au kuona aibu kunyonyesha. Ni muhimu kwa kila mzazi kwa kushirikiana na familia yake kuwa mtoto ananyonya kwa kipindi cha miaka miwili bila kuachishwa.

Pia ni muhimu kuhakikisha kuwa watoto wananyonyeshwa maziwa ya mama pekee, bila kupewa, vinywaji, au vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa. Ni muhimu kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 23 kupewa chakula cha nyongeza vilivyo na ubora wa lishe.
Pia ni lazima jamii ione umuhimu wa kuwakinga watoto na maradhi pamoja na kupatiwa tiba ya magonjwa ya kuambukiza mapema mara tu, wauguapo maana jukumu la ulinzi dhidi ya mtoto ni jukumu letu sote kama jamii na umma wote kiujumla.

Hivyo, basi tuone umuhimu wa kujenga taifa letu kwa kuzingatia lishe bora ili ifikapo mwaka 2025, tuwe tumepunguza idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa kwa asilimia 40 na hii itawezekana ikiwa tu kila mtu atafanya kwa upande wake.

Kwa mawasiliano wasiliana nami kwa simu namba 0763580901 au barua pepe ya barakangofira@gmail.com






LISHE BORA ITASAIDIA KUPUNGUZA UDUMAVU KWA WATOTO IFIKAPO 2025 LISHE BORA ITASAIDIA KUPUNGUZA UDUMAVU KWA WATOTO IFIKAPO 2025 Reviewed by WANGOFIRA on 04:30:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.