Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton

ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.

Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Demokratiki utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.

Marekani inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 8 Novemba mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kupambana na Donald Trump wa Chama cha Republican.

Maalim Seif na Zitto ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

Abdallah Khamis, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo amesema wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.

Taarifa zinaeleza kuwa, viongozi hao ni wawakilishi wa wanasiasa mahiri kutoka upinzani nchini Tanzania.
Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton Zitto Kabwe na Maalim Seif Kutua Marekani kwa Clinton Reviewed by WANGOFIRA on 20:24:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.