Paul Mkonda awahimiza Viongozi kuwa wazalendo katika Maadhimisho ya Miaka 37 ya Mashujaa

Screen Shot 2016-07-25 at 4.09.19 PM
Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Mkonda amewataka wananchi wa Mkoa wa DSM,watumishi wa Umma na Serikali kuwa wazalendo katika kutekeleza majukumu yao huku wakitanguliza Utanzania kwanza ili kuwaenzi mashujaa walipigana Vita kuu ya Dunia .

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Maadhimisho ya Miaka 37 ya Mashujaa waliopigana Vita dhidi ya wakoloni maadhimisho yaliyofanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja jijini Dsm.

Amesema baadhi ya wananchi,hususan watumishi wa serikali na Umma wameacha Uzalendo na kutanguliza maslahi yao mbele na kutahadharisha kuwa Serikali ya awamu ya Tano Chini ya Dr.Magufuri haitowafumbua macho watumishi wa Umma au serikali wanaotanguliza maslahi yao mbele .

Akisoma Dua kwa niaba ya Kamati ya Amani ya Mkoa wa DSM M/kiti wa kamati hiyo Sheikh Alhad Mussa Salum amewataka wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dr.Magufuri katika kuhakikisha kuwa watumishi wa Umma wanawajibika kwa wananchi pamoja na kuwa na maadili ktik kuwatumikia wananchi.
Paul Mkonda awahimiza Viongozi kuwa wazalendo katika Maadhimisho ya Miaka 37 ya Mashujaa Paul Mkonda awahimiza Viongozi kuwa wazalendo katika Maadhimisho ya Miaka 37 ya Mashujaa Reviewed by WANGOFIRA on 20:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.