Michel Jordan alaani mauaji Marekani

Michael Jordan, bingwa wa mpira wa vikapu
Michael Jordan, bingwa wa mpira wa vikapu
Michael Jordan, ambaye ni mmoja wa wachezaji wa zamani wanaofahamika ulimwenguni kote kwa ustadi wa kucheza mchezo wa Kikapu, amevunja kimya chake na kusema kuwa amekuwa akisikitishwa mno na visa vya kuuawa kwa Wamarekani weusi, vinavyotekelezwa na polisi.

Katika ujumbe kwa njia ya barua ya ukurasa mmoja iliyochapishwa na mtandao wa undefeated.com, ambao unamilikiwa na shirika la utangazaji la ESPN leo Jumatatu, Jordan, ambaye pia ni mmiliki wa klabu cha NBA cha Charlotte Hornet, alisema kuwa hawezi kuendelea kunyamaza kuhusiana na swala hilo.

Aidha Jordan ametangaza kupita barua hiyo, kwamba atatoa msaada wa dola milioni mbili, milioni moja ikienda kwa taasisi mpya ya uhusiano wa polisi na raia, iliyoundwa na chama cha kimataifa cha wakuu wa polisi, na milioni moja ikienda kwa idara ya kisheria ya chama cha masilahi ya watu wasio wa rangi nyeupe, NAACP.

Kwa mujibu wa mtandao huo wa undefeated.com, Jordan pia ameelezea kutoridhika kwake na mashambulizi yanayowalenga maafisa wa kulinda usalama. Mchezaji huyo wa zamani amesema kuwa, yeye kama mtu mweusi ambaye anjivunia kuwa Mmarejkani, na kama mtu ambaye alipoteza baba yake kupitia kupigwa risasi na wakora mnamo mwaka wa 1993, amekuwa akihuzunishwa sana na visa hivyo.

Kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kuwa licha ya Jordan kuwa na ushawishi kutokana na umaarufu wake, kabla ya leo, amekuwa mchache wa maneno kuhusiana na maswala yanayokumba jamii ya Wmarekani, jambo ambalo limepelekea baadhi ya wenzake kumkosoa.

Barua hiyo ya Jordan imejiri takriban wiki mbili na nusu baada ya mwanajeshi wa zamani kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watano wa polisi mjini Dalla, Texas, huku akisema kuwa alikuwa na hasira kwa sababu ya polisi kuwawapiga risasi na kuwaua Wamarekani weusi.
Michel Jordan alaani mauaji Marekani Michel Jordan alaani mauaji Marekani Reviewed by WANGOFIRA on 20:17:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.