Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi.

 
Mahakama kuu kanda maalumu ya Iringa leo imesendelea na kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha cha Channel Ten mkoani Iringa, Daud Mwangosi, inayomkabili askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573

Hukumu ya kesi hiyo awali ilipangwa kutolewa July 21 mwaka huu, iliahirishwa hadi leo kutokana na jaji anayesikiliza kesi hiyo kuwa nje ya mkoa kikazi.

Leo July 25 2016 taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV  ni kwamba mahakama kuu Iringa imemtia hatiani kwa kuua bila kukusudia askari huyo na hivyo hukumu rasmi itatolewa siku ya jumatano.



Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauwaji  kufikishwa
Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo
Mtuhumiwa wa  mauwaji  ya  Mwangosi  akipakiwa  kwenye  gari  za  FFU
Msafala  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiz askari  mwenzao anayekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia  leo
Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo
Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo

wakili
kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za
binadamu (
(THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo

wakili
kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za
binadamu (
(THRDC)Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo
 Siku ambayo  mwanahabari  Daudi  Mwangosi  alipouwawa
 Askari  hao   wakimtoa mahakamani  hapo  leo  mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi
                             
Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi. Taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa juu ya mauaji ya Daudi Mwangosi. Reviewed by WANGOFIRA on 20:09:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.