WHITEDENT YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA MAFANIKIO NCHI NZIMA.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa kampuni ya
Whitedent wakisherekea miaka 25 ya kutengeneza bidhaa za meno.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiweka maboksi ya Whitedent wakati wa
kuzindua shindano la whitedent linaloshindanishwa nchi nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiteta jambo na kiongozi wa Kampuni ya Whitedent Mkoani Tabora.
Kampuni
bidhaa za afya ya mdomo Whitedent inasherehekea kuadhimisha miaka 25 ya
biashara kwa kufanya promosheni ya miezi mitatu ambapo watu nchini kote
wananafasi ya kujishindia moja ya magari 25 ya aina ya Suzuki Alto
K10.
Whitedent
inatoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hili kwa
kukisia idadi ya pakiti za whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari
hayo ya Suzuki litakalokuwa linazunguka nchi nzima wakati wa promosheni.
Mteja atatakiwa tu kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha
promosheni na kukisia jibu sahihi ili aweze kuingia katika droo kubwa ya
kujishindia moja ya magari hayo ya Suzuki Alto 10 mwisho wa promosheni
hii Oktoba mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni, Afisa Mkuu wa Chemi & Cotex
Raja Swaminathan alisema, “Katika kusherehekea miaka 25 ya bidhaa hii
tumetaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio yetu. Tunatoa
magari haya ambayo ni mapya kabisa yakiwa yamejaa mafuta kwenye tenki
lake, na yakiwa yamelipiwa ushuru na bima kwa mwaka mzima. Katika
promosheni hii, hakutakuwa na kiingilio cha aina yoyote na wala mshiriki
hatakiwi kutumia hata shilingi moja ili aweze kushiriki na zaidi ya
hapo watu wote wanaweza kushiriki mara nyingi wawezavyo.”
Shindano
hili litakalokuwa chini ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya
Bahati Nasibu Tanzania itachukua miezi mitatu na itashirikisha mikoa
yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.
“Tungependa
kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika shindano hili. Bidhaa ya
Whitedent ni ya kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa
na Watanzania. Safari ya promosheni itapita sio mijini tu bali pia
katika vijiji ili kuhakikisha kila mtu ana nafasi ya kushiriki,”
aliongeza Swaminathan.
Inakadiriwa
kuwa zaidi ya wana Afrika Mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa
kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent. Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa
Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa Whitedent ina asilimia 79 ya soko
nchini na hupatikana katika maduka makubwa ya bidhaa hadi kwenye vioski
vidogo.
WHITEDENT YASHEREHEKEA MIAKA 25 YA MAFANIKIO NCHI NZIMA.
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:15:00
Rating:
No comments: