TUNAPOELEKEA WATOTO WA WENYE NAZO NDIYO WATASOMA VYUO VIKUU.



 
Kwa muda mrefu sasa Sekta ya Elimu imekuwa ikilalamikiwa sana na wadau wa elimu kuwa imepoteza mwelekeo kwa kutoa wataalam wengi ambao kiukweli wanakuwa hawajaiva vya kutosha kwenda kutumika katika fani mbalimbali. Ikiwemo kufundisha hata shughuli nyingine nje ya ualimu ambao uandaa vijana hawa kutumika katika ujenzi wa nchi

Wadau wa sekta hii na hata sekta nyingine wamekuwa wakijiuliza maswali mengi ambayo kiujumla hukosa majibu ya kwa nini sekta hii inadolola kila mwaka, huku walimu kila kuchapo huajiliwa na serikali.
 
Hawaishii hapo tu bali huenda mbali zaidi kujiuliza kwa nini kwa sasa Serikali imeamua kuanzisha elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne. Jambo ambalo limepongezwa na wengi lakini swali kubwa likiwa ni kwa nini wakubwa walioanzisha watoto wao hawasomi kwenye shule za bure.

Na wao wanawapeleka watoto wao nje au shule zile ambazo wanaziita wao eti international skuli au private ikiwa na maana ya shule binafsi. Ambazo nyingi umilikiwa na vigogo walio serikalini au nje ya nchi.

Shule hizi za kiinteneshinari ufundisha vizuri na kila mwaka husifika kwa kuwa shule bora na kutoa wanafunzi bora ambao hupewa zawadi na serikali kwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao na shule pia hupewa zawadi kwa kufaulisha wanafunzi. 

Utasikia mwaka kati ya shule 100 bora za sendari zilizofanya vizuri ni 5 au 7 tu ndizo za serikali na nyingine zote zilizosalia ni zile za wenzangu na mimi ambao wamebatizwa jina la vilaza. 

Na sasa hakuna usemi ulio rahisi kwa serikali hii ya awamu ya tano ambapo wizara hii ipo chini nya mikono ya Profesa Joyce Ndalichako ambao wengi humuita na kumtania kuwa ni jembe la kazi. Maana hacheki na ninahisi hatocheka na mtu kwenye maswala ya Elimu ambapo akisimamia msimamo wake anaouamini kuwa ni ukweli hata ufanyaje hawezi kubadilika kamwe labda umuweke pembeni.

Hii imejidhihisha wazi tangu alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, baadaye Baraza la Mitihani Tanzania yaani (BAMITA) au NECTA kwa lugha ya kingereza, alipopinga waziwazi mfumo wa Matokeo makubwa sasa au kwa kingereza Big Result Now (BRN) kutohusika kwenye sekta ya Elimu. Na pale wakubwa walipolazimisha akaamua kujiweka pembeni ili awapishe wenye nguvu wapite. Maana wao wameshika kwenye mpini na makali ameyashikilia hivyo akishindana nao ataumia mwenyewe.

Mfumo huu wa Big Result Now ulipingwa sana na wadau na hata wanasiasa wenyewe walioupitisha kwani waliona ni nkama kupanua goli, ili waongeze idadi ya magoli kwa watu kutojishughulisha ipasavyo katika masuala ya kutafuta Elimu.

Au huenda kulikuwa na watoto wa wanasiasa hao waliopitisha mfumo huu ili na wanao wapite kwa mtelezo kama mtu anayeteleza kwenye ganda la ndizi lililonyeshewa mvua. 

Lakini siku za big result hazikuwa nyingi na Uteuzi ukamwangukia Prof. Ndalichako kuwa waziri mwenye Dhamana ya elimu, sayansi na Teknolojia. Na alipoingia tu akatupilia mbali mfumo wa matokea makubwa sasa akaamua kurudi kule Elimu ilikokuwa zamani.
Jambo ambalo lilipongezwa na wasomi japo wanasiasa wengi hawakulifurahia jambo hili kwani huenda kwa wengine ilikiuwa miradi yao ya upigaji. 

Muda haukuwa mrefu wanafunzi wa Chuo kikuu cha St. Joseph zaidi ya 200 wakafukuzwa kwa kile walichokidai kuwa ni kukosa sifa na vigezo vya kusoma chuo kikuu. Kikafuata Chuo Kikuu cha Dodoma kikafuata ambapo zaidi ya wanafunzi 7000 waliokuwa wanasoma stashahada maalum ya ualimu wakafukuzwa, kwa  kuwa hawana nao vigezo vya kusoma masomo hayo na hivyo wachache wenye sifa ndiyo watarudi chuoni mara baada ya zoezi la uhakiki wa taarifa zao kukamilika.

Kwa hili wanasiasa na hata watanzania wengi walishikwa pabaya maana wazazi na wanafunzi wa Dodoma walikuwa katika hali mbaya na mpaka leo hawajajua hatima yao. Na suala lilipoingia bungeni wakaliweka chini ya kapeti na kuendelea na masula mengine ambayo ni ya muhimu kwa madai yao.

Kwa wanafunzi wengi waliofukuzwa Dodoma ni watoto wa maskini na wakulima ambao kwao asubuhi na mchana ni sawa. Wale wasile, kwao ni kawaida kabisa maana maisha yenyewe waliyoyasomea wanayajua wao maana kila mtu ana hadithi ya maisha yake mwenyewe ya jinsi wazazi wake walivyojikongoja hadi akamaliza kidato cha nne na kubahatika kupata nafasio ambayo naweza kusema wamenyang’anywa Tonge mdomoni.

Kufuatia udahili wao kufutwa zoezi halikuishia kwa wanafunzi tu maana hata waliohusika kudahili yaani Tume ya Vyuo Vikuu nayo iligeuzwa kichwa chini, miguu juu. Nikimaanisha wakurugenzi watano akiwemo Profesa Yunus Mgaya nao walifukuzwa kazi, kwa kosa la kuajili wanafunzi wasio na sifa na kuliingiza taifa hasara kubwa kwani karibu wote waliodahiliwa walikuwa wanapewa mkopo wa serikali.

Sasa sakata lipo kwenye sifa na vigezo za udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka 2016/2017, ambapo wadau wengi wana wasiwasi wa vyuo vingi kukosa wanafunzi kutokana na ufaulu kuwa mkubwa zaidi ya uwezo walionao wanafunzi wengi hususani wale wanaosoma shule za wenzangu na mimi.

Maana wao siku zote ndiyo huwa wahanga wakubwa wa matukio haya maana watoto wa wakubwa hwapati shida, kwani pesa ipo na kama wakifeli upelekwa nje ya nchi kusoma na kutafutiwa au kufanya kazi kwenye makampuni ya wazazi wao au rafiki za wazazi wao. Maana zimwi likujualo halikuli likakwisha. 

Imeandaliwa na Baraka Ngofira

MUNGU IBARIKI TANZANIA, WABARIKI NA VIONGOZI NA WANANCHI WAKE.
MAWASILIANO, barakangofira@gmail.com au 0763580901.




TUNAPOELEKEA WATOTO WA WENYE NAZO NDIYO WATASOMA VYUO VIKUU. TUNAPOELEKEA WATOTO WA WENYE NAZO NDIYO WATASOMA VYUO VIKUU. Reviewed by WANGOFIRA on 04:01:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.