Riyama Ally Awafunga Midomo Mashabiki wanaomsema yeye na Mumewe
STAA wa filamu za Kibongo, Riyama Ally amewafunga midomo wote waliokuwa
wakibeza uhusiano wake na msanii chipukizi wa muziki wa Bongo Fleva,
Haji Mwalimu Mzee ‘Leo Mysterio’, baada ya kufunga naye ndoa hivi
karibuni.
Minong’ono ilikuwa mingi mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa
Riyama yupo kwenye uhusiano na Serengeti Boy kwa vile kijana huyo ni
mdogo wake kiumri kwa miaka saba zaidi.
Akiondoa utata, Riyama alisema wanaojua kusugua midomo waendelee
lakini wao tayari wameshakuwa mwili mmoja, yeye akiwa mali halali ya Leo
Mysterio.
“Wamesema sana, lakini sasa limewashuka shuuu! Wengine walisema sijui
tunatafuta kiki, mara ooh! Sijui nimemzidi umri… inawahusu nini? Tayari
tumeshafunga ndoa, sasa watuache tulale. Kama vilimilimi tushawakata,”
anasema Riyama.
Mysterio ana umri wa miaka 26 huku Riyama akiwa na miaka 33, miaka
saba zaidi ya mume wake huyo anayetamba kupendana mpaka kifo
kitakapowatenganisha.
Riyama anasema: “Mimi najiheshimu sana, ndiyo maana huwezi kunikuta
kwenye skendo yoyote. Hata mavazi yangu siku zote huwa ya heshima.
Najitambua sana.
“Sasa kama kupenda au kupendwa na mtu mliyezidiana umri ni skendo,
nipo tayari kwa hiyo. Mimi nilichoangalia ni mapenzi ya kweli, siyo
umri. Mume wangu tumeelewana na naona kila mmoja anakidhi haja za
mwenzake, sasa tatizo nini?
“Nampenda na nitamheshimu mume wangu hadi kifo kitakapotutenganisha,
wanaosema na waseme, sisi tumeziba masikio yetu. Wala hatufikirii
kuachana. Sisi ni wa maisha.
Riyama Ally Awafunga Midomo Mashabiki wanaomsema yeye na Mumewe
Reviewed by WANGOFIRA
on
08:37:00
Rating:
No comments: