Riwaya:Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi na Tano

MTUNZI:ENEA FAIDY

...DORICE alikuwa akiyatafakari maneno ya malkia wa himaya aliyokuwepo kwa wakati ule. Alikuwa haelewi afanye nini na achague lipi kati ya kifo au kuolewa na jini. Alijikuta yupo kwenye wakati mgumu sana mpaka akajuta kutoroka shuleni. Alimlaani sana Doreen kwani ndiye chanzo cha matatizo yote. Alijikuta analia bila kujua msaada wake utatoka wapi.

Akiwa katika wimbi la mawazo alishtushwa na harufu Kali ya marashi iliyomfanya azinduke na kumtazama mgeni wake. Alipoinua kichwa chake alikutana tabasamu mwanana kutoka kwenye sura nzuri ya upole ya kijana Mansoor.

"Nakupenda Dorice.. Olewa na Mimi!" Alisema mansoor kwa sauti tamu iliyojaa huba. Lakini sauti na maneno hayo habvikuwa kitu kwa Dorice, aliachia sonyo Kali iliyodhihirisha chuki kuu dhidi ya Mansoor.

"Kama kuniua niueni! Siwezi kuolewa nawewe!" Dorice alisema maneno hayo kwa ujasiri sana bila kujali jambo hilo lingeonekanaje kwa Mansoor.
Mansoor alihuzunika sana, akatikisa kichwa kama ilivyokuwa kawaida yake . Akashindwa kuyazuia machozi ya damu machoni mwake lakini Dorice hakujali hilo.
"Dorice! Kwanini haunipendi? Au kwa sababu Mimi sio binadamu mwenzio?" Aliongea Mansoor kwa huzuni sana lakini Dorice hakujibu kitu.

"Tafadhali niambie Dorice... Nikufanyie nini ili uamini kuwa nakupenda?" Aliuliza mansoor kwa sauti ya upole.
"Utanifanyia?"
"Ndio Dorice!"
"Naomba unirudishe duniani..."
"Nikikurudisha sasa nitakuoaje? Siwezi ishi mbali nawewe!"
"Umesema utanifanyia nikuombacho.. Umeniahidi!"
"Ndio ila hilo suala gumu... Kwanini hunipendi?"
"Nampenda mtu mwingine.. Na ndie aliyenifanya nipate matatizo haya yote.." Dorice alisema maneno hayo huku machozi yakimlengalenga kwani kila alipomkumbuka Eddy alidondosha chozi na hakutaka kuamini kama Kweli Eddy amemwacha na yupo na Doreen.
"Unampenda nani?"
"Nampenda mtu anaitwa Eddy, siko tayari kimkosa nataka nipiganie penzi langu... Samahani sana Mansoor... Wewe ni mzuri ila sins hisia na wewe kabisa!" Dorice alijikuta akiropoka maneno hayo yote ili kufikisha hisia zake kwa Mansoor. Maneno Yale yaliugusa vyema moyo wa Mansoor, alihuzunika sana ila ilibidi akubaliane na ukweli.
"Nashukuru kwa kuwa mkweli Dorice.. Nakupenda sana ila siwezi kukulazimisha unipende... Hakutakuwa na mapenzi hapo.. . Naumia sana ila inabidi nizielewe hisia zako!" Alisema Mansoor kwa sauti iliyojaa masikitiko makubwa sana ila hakuwa na jinsi. Mansoor alikuwa ni mini mstaarabu kupita kiasi ingawa mama take alikuwa katili tena mwenye roho mbaya sana.

"Umenielewa Mansoor?!"
"Ndio.. Nimekuelewa sana! Ila nisimulie ilikuwaje?"
Dorice alifuta machozi na kutabasamu kidogo ingawa bado alikuwa na maumivu ya mapenzi kwa Eddy. Akajua ule ni msaada wa kwanza kwake kwenye eneo lile, akaamua kumsimulia kila kitu kama ilivyokuwa kati ya yeye na Eddy na kisa cha kutoroka.

Mansoor alihuzunika sana, akamwonea huruma sana Dorice.
"Binadamu wabaya sana..!"alisema Mansoor.
"Inaniuma sana! Nampenda sana Eddy..!"!

Mansoor alichukua kitu kama kioo, akakitazama kwa muda kisha kikamletea picha ya Doreen.
"Mh! Huyu Doreen.. Ni mtu mbaya sana .. In mtu hatari kupita kawaida..!"

Alisema Mansoor kwa mshtuko huku akimtazama Dorice. Dorice alikuwa haelewi chochote akabaki akishangaa tu.
"Doreen ni mchawi sana.. Na kuna kitu anatafuta! Amemharibu sana Eddy... Eddy yupo kwenye wakati mbaya na muda wowote anammaliza..!"

Maneno ya Mansoor yalimshtua Dorice
"Amemfanyaje? Nisaidie kumwokoa Eddy tafadhali..!"
"Mama hatanikubalia ila inabidi nikusaidie Dorice.. Yote ni kwasababu nakupenda.. Nitakusaidia usijali!"
Alisema Mansoor.
"Nitafurahi sana ukinisaidia Mansoor!"
"Usijali.. Ila mama ni kikwazo..!"
"Jitahidi Mansoor!"
Dorice alichanganyikiwa sana baada ya kusikia kuwa Eddy atauliwa muda wowote na Doreen, ilibidi azidi kumsihi Mansoor aweze kumsaidia kwa namna yoyote ile kwani alitambua uwezo mkubwa aliokuwa nao jini yule mstaarabu.

                                            ******
Doreen alibaki pale chini kwa muda mrefu sana akishindwa kutoka mle ndani.
Alihangaika sana mpaka kijasho kikaanza kumtoka kwani aliziona kabisa dalili za kufamwa, aliwaza aibu ambayo ingemkuta hakujua afanyaje.

Akiwa katika harakati hizo za kutaka kuondoka akahisi moto mkali ukimpitia, akapiga kelele za maumivu huku akigalagala pale chini. Chumba kizima kilikuwa kimya sana kwani wanafunzi wote walikuwa wamelala fofofo na hakuna aliyeweza kusikia kilio kile.

Doreen aliteseka sana na tangy aanze uchawi hakuwahi kukumbana na hali ile.

Aliona uchawi sasa ni wa mateso, kwani maumivu aliyokuwa anayapata hayana mfano.

Doreen alijitahidi kufanya kila awezalo ili aweze kutoka ndani ya bweni lile lakini halo ikazidi kuwa mbaya. Ghafla akasikia mtu akikohoa akajua mwisho wake umefika. Akaanza kuropoka maneno yake ya uchawi ili aweze kutoka hatimaye akafanikiwa. Ikawa ahueni yake ingawa mwili wote ulikuwa unamuuma vibaya sana.

Alifika kwenye kichaka ambacho aliacha vitu vyake, akajibwaga kama mzigo huku akiugulia maumivu. Aligalagala pale chini kwa muda wa SAA zima hatimaye maumivu yakapungua. Akaamua kurudi bwenini kulala.

Alinyatanyata mpaka alipokifika kitanda chake. Alilala huku akimfikiria Nadia.

"Mh! Huyu mtu si wa mchezo dah!" Alijisemea Doreen kimoyomoyo, kwa maumivu aliyoyapata hakuweza hata kuinuka kitandani.
" Nitafanyaje Mimi? Siku zimeisha sana sasa lakini bado kitu kimoja tu, titi la msichana mzuri! Nitapataje sasa?" Alijiuliza Doreen bila kupata majibu.
"Enhe! Inabidi nifanye kitu.. Nimtumie MTU..!" Doreen alipata wazo kuwa inabidi amtumie mtu ili kupata titi hilo ili akamilishe mambo aliyoyahitaji. Lakini asingeweza kufanya kwa usiku ule kwani alikuwa hoi bin taabani.

Usingizi ukampitia kidogo na kwakuwa ilikuwa SAA kumi na nusu hakulala sana kengele ya kuamka ikamshtua.
Kulikuwa tayari kumekucha. Doreen alikuwa hana nguvu kabisa mwilini na mwili wake ulikuwa bado unamuuma hivyo akashindwa kwenda darasani kwa madai kuwa alikuwa mgonjwa. Ila moyoni alimwogopa sana Nadia na hakutamani hata kumwona kwani alimuonea aibu.

Wanafunzi wote walienda darasani isipokuwa Dorice, alibaki bwenini na alitaka kuitumia nafasi ile vizuri ili amtumie mtu kutafuta titi la msichana mzuri wa kuvutia.

                                           ******
Wazazi wa Eddy walishika njia kutokea mkoani Iringa kuelekea pangani Tanga.
Walikuwa na matumaini mazito ya kumpata mganga mashuhuri aitwaye Tembo wa Bahari.
Hawakua na wasiwasi wowote juu ya mganga huyo kwani tayari walikuwa wamezisikia sifa zake kuwa yupo vizuri sana katika suala la matibabu.

Eddy alikuwa ametulia kimya ndani ya gari lile ambalo dereva alikuwa ni Mr.Alloyce.
Kila Mara aliyakumbuka maneno ya Doreen kuwa endapo watafika kwa mganga basi uhai wake utakuwa umefikia kikomo. Kuna wakati aliyapuuzia mawazo hayo lakini wakati mwingine alihisi yana ukweli ndani yake, kama Doreen aliweza kumtoa sehemu zake nyeti atashindwa kumuua? Alijiuliza Eddy.
Ukimya ulitawala ndani ya gari lakini kelele nyingi zilitawala kichwani mwa Eddy kwani mawazo yalikuwa hayakauki kichwani mwake
"Mama!" eddy aliita.
"Sema mwanangu..!"
"Nina njaa!"
"Ngoja nikupe chakula..!"
Mama Eddy alichukua hotpot na kumtolea mapaja ya kuku yaliyokaushwa vizuri pamoja na chipsi mayai zilizoshikana vizuri.
"Chukua ule.."
"Sawa! Ila nipe chakula!"
"Mh! Chakula hicho!"
"Hicho siwezi kula maana kina uchafu..!"
Alisema Eddy maneno yaliyomchanganya sana mama yake kwani kila alipotazama chakula kilikuwa kizuri tu.
"Hakuna uchafu..!"
"Upo!"
Eddy alisisitiza na Mara hiyo akaanza kuhisi kichefuchefu.
"Mama simamisheni gari nataka nikatapike nje.."alisema Eddy. Kwa haraka Mr.Alloyce alisimamisha gari wakamtoa nje Eddy ili akatapike.
Eneo like lilikuwa na miti mingi kwani lilikuwa pori. Eddy aliwatazama wazazi wake, kisha akasogea kando kidogo.
Akawatazama tena kwa jicho la wizi , akajiweka sawa kisha bila wazazi wake kutarajia akatimua mbio Kali kuelekea porini.
Wazazi wake wakapigwa butwaa sana wakashindwa wafanye nini wakabaki wamezubaa huku wakitazama kwa mshangao. Eddy alikuwa tayari amewapotea machoni mwao kwani mbio alizokuwa akikimbia zilikuwa za MWENDOKASI.....

ITAENDELEA...........
Riwaya:Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi na Tano Riwaya:Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi na Tano Reviewed by WANGOFIRA on 20:11:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.