RAIA WA AFRIKA KUSINI AFARIKI DUNIA MLIMA KILIMANJARO
Raia wa Afrika Kusini waliopanda Mlima
hivi karibuni kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua taulo
za kusaidia watoto wa kike.aliyechuchumaa mbele (mwenye kofia) Gugu
Zulu ndiye anatajwa kufariki Dunia wakati akielekea Kileleni.
Gugu Zule (Kulia) akiwa na Richard Mabaso muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Gugu
Zulu akiwa katika lango la Marangu akipata picha na mmoja wa washiriki
wa safari hiyo muda mfupi kabla ya kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro.
Gugu Zulu (kushoto) akiwa na rafiki
yake muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro
katika kampeni ijulikanayo kama Trek4Mandela ikiwa na lengo la
kchangisha fedha kwa ajili ya kunua taulo za watoto wa kike pamoja na
kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa baba wa taifa la Afrika Kusini
,Nelson Mandela.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Ra ia wa Afrika ya Kusini
Guguleth Mathebula Zulu (38) aliyefika nchini kwa
ajili utalii wa kupanda Mlima Kilimanjaro amefariki
leo tarehe 18.7.2016 baada ya kupatwa na tatizo
la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa juu
mlimani.
Shirika la Hifadhi za
Taifa nchini kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali
za serikali zinaendelea na uratibu wa kurejesha
mwili wa marehemu nchini Afrika ya Kusini kwa
ajili ya taratibu za maziko.
Zulu alifika nchini na
kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro tarehe 14.7.2016
kwa ajili ya kuenzi jitihada za Rais wa
Kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela za
kusaidia familia maskini nchini Afrika ya Kusini,
hususani kuwapatia mahitaji muhimu watoto wa kike
ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu.
Hii ni mara ya pili
kwa watalii kutoka Afrika ya Kusini kupanda
Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuenzi juhudi za
Mandela katika kusaidia jamii ya watoto wa kike
kupitia kampeni maalum ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Hifadhi za Taifa Tanzania
S.L.P 3134
Baruapepe: dg@tanzaniaparks.go.tz
Wavuti: www.tanzaniaparks.go.tz
18.07.201
RAIA WA AFRIKA KUSINI AFARIKI DUNIA MLIMA KILIMANJARO
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:47:00
Rating:
No comments: