RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 16

MTUNZI:ENEA FAIDY

....DOREEN alikuwa bado hana hali nzuri kiafya, mwili wake ulikuwa hauna nguvu kabisa kwani ile adhabu aliyoipata usiku ilimwadhibu haswa. Alijikuta anamwogopa Nadia kupita kiasi, moyoni mwake alikiri kuwa kweli Nadia Joseph alikuwa Mchamungu kweli.

Wakati huo akiwa bado yupo kitandani akiugulia maumivu, Doreen alifikiria jinsi ya kuweza kupata titi la msichana mrembo ili akamilishe kazi yake aliyotumwa kuifanya. Siku zilikuwa zimeisha sana lakini alijipa moyo kuwa ameshamaliza kazi kwani kupata titi aliona kama kazi rahisi tu ingawa ilishaanza kupata vikwazo.

Doreen alishuka kitandani kwake. Akavua nguo zote kisha akasogelea begi lake na kuchukua shanga nyeusi akaivaa shingoni mwake.

Na kwakuwa alikuwa peke take chumbani mle Doreen alifanya mambo yake bila woga. Akachukua kichupa kimoja kidogo kwenye begi lake halafu akamimina kidogo unga unga uliokuwamo mle na kujipaka usoni kisha akapiga magoti chini na kuinamisha kichwa chake huku akitamka maneno Fulani.

Ghafla karatasi ambayo ilifanya mauaji ya walimu ofisini ikamjia mkononi make.Ikumbukwe kuwa karatasi ile ilichukuliwa na mwalimu Jason ambapo kulikuwa na maandishi yaliyomuonya kuwa asimpe mtu mwingine, hivyo Mwalimu Jason aliamua kukimbia nayo na alikuwa akikaa Nayo kwa siku zote zile.

Doreen alitabasamu baada ya kuitazama karatasi ile, akaishika vizuri kwa mikono miwili kisha akasema "NENDA KWA MWALIMU JASON! MWAMBIE ANILETEE TITI LA MSICHANA MREMBO! NAKUAMINI!" alisema Doreen kisha akaiachia karatasi ile, ikapaa hewani na ikapotea.

Doreen alifurahi sana akajua tayari amekwisha maliza kazi yake. Akiwa bado ameketi pale chini akiendelea na mambo yake mengine ghafla mlango wa bweni lake ukagongwa halafu akakumbuka kuwa hakuubana mlango ule vizuri kwa komeo Doreen alishtuka sana kwani alikuwa mtupu na alikuwa na maunga unga usoni. Akahisi fumanizi la uchawi tayari limemfikia.
   

                                       ********
Mansoor alikubali kumsaidia Dorice ili kumwokoa Eddy lakini bado moyo wake ulimuuma sana. Hakuwa radhi kumwacha binti yule kirahisi pasina kumuoa ilhali moyo wake ulizimia kwa mapenzi kwa mrembo yule. Mansoor alimpenda sana Dorice hivyo akajiona bwege sana kumwacha msichana yule aondoke kwenye himaya yao wakati moyo unamhitaji.

"Mwanamke anahitaji kubembelezwa! Nikimbembeleza sana anaweza kunikubali.... Yawezekana anamuogopa mama yangu kutokana na vitisho alivyompa... Mhh nitajaribu tena bahati yangu kwani moyo wangu hautakuwa na amani kabisa nikimuacha Dorice!" Aliwaza Mansoor akiwa ametulia peke yake kando ya Maua mazuri yanayotoa harufu ya kuvutia. Aliwaza sana juu ya kumpata Dorice lakini bado hakuona njia sahihi ambayo ingekubalika haraka zaidi ya kumshawishi tu huba na kumbembeleza kwa mahaba.

Akiwa katika wingu hilo zito la mawazo Mansoor alishtushwa na upepo mkali. Akajua moja kwa moja mama yake alikuwa njiani kwani upepo ule zilikuwa in hatua za Malkia. Punde si punde malkia akatia timu na kuketi kando ya Mansoor.

"Vipi mwanangu? Mbona unasononeka sana kiasi cha kuondoa amani ya moyo wangu?"
"Hakuna tatizo mama!" Alijibu Mansoor huku akijaribu kuachia tabasamu.
"Unanificha Mansoor.. Au yule binadamu asiyejaa hata kiganjani bado anakusumbua?"
"Hapana mama.. Hana tatizo lolote na anaonesha moyo wa kunipenda!" Ilibidi Mansoor amdanganye mama yake kwani alijua madhara ambayo angemfanyia Dorice kama angemweleza ukweli.
"Kweli?" Malkia alifurahi.
"Kweli mama yangu.. Malkia mtukufu..!" Alitabasamu Mansoor ingawa moyoni aliumia.
"Vizuri sana... Nadhani furaha yako itarejea sasa!"
"Ndio mama wala usiwe na wasiwasi!"
Malkia aliondoka zake akiwa ameghairi lengo lake la kumwangamiza Dorice. Kwani alipanga kuondosha uhai wake endapo angekataa kumpenda Mansoor.

Mansoor alimfuata Dorice kwenye chumba alichokuwa anaishi. Aliingia chumbani mle akiwa amemletea zawadi ya maua mazuri yanayonukia vizuri sana. Alipoingia tu, akasikia sauti ya kilio kutoka kwa Dorice. Mansoor akashtuka kidogo kisha akamsogelea taratibu Dorice.

"Unalia mini Dori?"
"Nataka nirudi nyumbani... Wazazi wangu watakuwa wananitafuta sana..!"
"Usilie Dorice...!"
"Siwezi kuzuia maumivu yangu juu ya wazazi wangu Mansoor... Pia namfikiria mpenzi wangu..!"
"Nyamaza Dorice.. Nitakusaidia kwa yote hayo... Hebu nitazame!" Mansoor alimkazia macho Dorice kisha akamkabidhi Maua aliyokuwa ameyashika.
"Yanini..?"
"Usijali.. We pokea tu.."
Dorice aliyapokea maua Yale huku akisitasita sana. Baada ya kuyapokea mansoor alitabasamu sana.
"Asante kwa kupokea zawadi yangu Dorice... Nakupenda sana!" Dorice hakujibu kitu zaidi ya kumshangaa Mansoor.
"Nataka nikusaidie... Upo tayari..?"
"Nipo tayari Mansoor tafadhali.."
"Sawa Dorice.. Kabla sijakusaidia nahitaji unisaidie kitu.."
"Kitu gani!?" Dorice alishtuka sana.
"Nataka uolewe na Mimi.. Tafadhali Dorice... Nitakusaidia kwa lolote utakalo ukikubali kuolewa na Mimi..!"
"Mansoor! Nilishakwambia nampenda Eddy..."

"Ukikubali kuolewa na Mimi nitakusaidia kumpata Huyo Eddy na nitakuruhusu uendelee Naye... Nakuomba Dorice! Ilidhishe nafsi yangu!" Alisema Mansoor huku akipiga magoti.

                                             *******
Mwalimu Jason alikuwa akisumbuliwa sana na karatasi lile alilolichukua ofisini baada ya kifo cha Mwalimu Mbeshi. Halikutakiwa kuonekana na MTU yeyote wala kuguswa na maji.

Lilikuwa likimchanganya sana kichwa kwani kila siku lilikuwa likibadili ujumbe na kuandika masharti mapya.Siku hiyo asubuhi mwalimu Jason kutokana na kutokwenda kazini aliamka asubuhi na mapema ili afue nguo zake.

Alikusanya nguo chafu zote na kuziweka kwenye beseni la kufulia lenye maji na sabuni. Na alikuwa na uhakika kabisa kuwa karatasi halikuwa kwenye nguo zile. Akaanza kufua nguo zake kwa umakini ili azitakatishe ndipo alipogundua kuwa suruali yenye karatasi lile la maajabu ipo ndani ya beseni la maji.

Kengele ya hatari ikagonga kwa kasi moyoni mwake, akaipoa suruali ile huku mapigo yake ya moyo yakimpiga kwa kasi.

Akaanza kutafuta karatasi lile kwenye mifuko ya suruali ile. Hofu ikamzidia maradufu baada ya kutafuta kila mfuko na kulikosa karatasi lile.

Mwalimu Jason alichanganyikiwa sana, ikambidi aanze kupekua suruali zake zote na kutafuta vizuri karatasi lile alikuwa akiliita karatasi la kifo kwani kila mara lilikuwa likimuonya kuwa akikosea sharti basi lazima afe.

Mwalimu Jason alipekuwa kila suruali aliyokuwa ameiloweka kwenye maji lakini bado hakuona karatasi akazidi kuchanganyikiwa. 

Alizitupa chini nguo zote kisha akaingia ndani na kuanza kupekua kwenye kila suruali lakini bado hakuona karatasi lile. Mwalimu Jason alipigwa na butwaa. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka kila kona ya mwili wake. Akajitupa kitandani na kuanza kulia kwa woga. Alijua tayari kifo kiko mbele yake si muda mrefu.

Ghafla simu yake ikaita na kwakuwa alikuwa kwenye kilio hakuweza kupokea simu. Akaicha tu bila hata kuingalia.

Lakini kwa bahati njema aliona karatasi ikiwa pembeni ya mto wake wa kulalalia. Mwalimu Jason alifurahi kisha akaichukua karatasi ile na kusoma ujumbe mpya ulioandikwa hivi "MSICHANA YEYOTE ATAKAYELALIA KITANDA HIKI.. UNATAKIWA UMKATE TITI LAKE LA KUSHOTO HARAKA IWEZEKANAVYO. LASIVYO UHAI WAKO UTAFIKIA KIKOMO!"

Mwalimu Jason akatumbua macho kwa mshangao. Akarudia kusoma ujumbe ule mara mbilimbili lakini hakuna kilichobadilika. Akahisi mwili wake unaishiwa nguvu kabisa kwani Siku ile alikuwa na miadi na mpenzi wake. Alijiuliza atafanya nini hakuwa na la kufanya.Simu take ikaita tena akaitazama ilikuwa ni namba ya mpenzi wake. Akapokea.

"Baby mbona hukupokea simu?"
"Ulipiga?" Jason alijifanya kama hajui lolote kama simu ilipigwa.
"Kwani hukuona? Ok.. Nipo njiani nakuja!"
"Eeeh!" Jason alishtuka sana.
"Vipi mbona unashtuka?"
"Ah..una.. Naomba usije home Leo.. Kama vipi tukutane Hotelini.."
"Hivi Jason una akili timamu wewe? Hapo kwako kuna nini? Au una MTU mwingine?"
"Sina MTU mwingine baby.. Ila.." Jason alitamani kujitetea ila hakuweza kufanya hivyo.
"Nitoke Dar kuja Iringa kwaajili yako halafu uniletee hizo habari zako.. Kwani tulikubaliana nini?" Msichana yule alimjia juu mwalimu Jason
"Usipaniki baby basi.. Hotelini ni kuzuri pia..!"
"Kama una michepuko yako basi tutajua..!"
Msichana yule akakata simu.

Mwalimu Jason alijiona ana mtihani mkubwa sana. Aliwaza na kuwazua lakini bado hakupata jibu. Majira ya SAA Kumi na nusu jioni mlango uligongwa. Mwalimu Jason alienda kufungua akakutana USO kwa uso na sura ya Judith ambaye ni mpenzi wake akiwa amenuna sana. 

Mwalimu Jason hakuwa na la kufanya zaidi ya kumkaribisha Judith ndani.Waliposalimiana tu Judith akaingia chumbani kwa mwalimu Jason ili akaweke mizigo yake.Lakini kila alipomtazama Mwalimu Jason, hakuwa na furaha hata kidogo.

"Mbona hujanifurahia?"
Aliuliza Judith
"Nipo kawaida.. !" Alijibu mwalimu Jason.
"Ok basi ngoja nikapumzike kidogo maana nimechoka kweli..!" Alisema Judith huku akipiga hatua kuelekea kitandani........

ITAENDELEA....
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 16 RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 16 Reviewed by WANGOFIRA on 20:13:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.