Waziri Mbarawa aitaka TPA kujenga gati
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),
kuanza ujenzi wa maegesho ya meli katika bandari ambazo meli mbili mpya
zinazojengwa na Mamlaka hiyo katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela,
zitatoa huduma ya usafiri baada ya kukamilika.
Waziri
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo alipokagua bandari ya Mbambabay iliyopo
Wilayani Nyasa ambayo ni miongoni mwa bandari ambazo meli hizo zitatoa
huduma na kubaini kuwa bado bandari hiyo haina maegesho kwa ajili ya
meli hizo.
“Nataka
kuona maegesho ya meli yanakamilika haraka ili kuwezesha meli mpya
kupakua na kupakia mizigo katika bandari hii”, amesema Waziri Prof
Mbarawa.
Ameeleza
kuwa meli hizo mbili za mizigo ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi
Agosti na Oktoba zitaongeza kasi ya utoaji wa huduma katika bandari hiyo
na kuwa chachu ya maendeleo hususan katika shughuli za biashara na
kiuchumi katika mkoa wa Ruvuma na nchi jirani.
Meneja
wa Bandari ya Kyela, Percival Salama (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
(wa pili kulia) ya namna shughuli za biashara ya makaa ya Mawe
zinavyoweza kuongeza pato kwa bandari ya Bambabay Mkoani Ruvuma.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amemtaka Meneja wa Bandari ya Kyela kuisimamia
kampuni ya M/s Songoro Marine Transport Boart Yard inayojenga meli hizo
ili zijengwe kwa ubora na viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya
fedha ambazo zinatokana na kodi za wananchi.
Katika
Hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara ya
Mbinga-Mbambabay yenye urefu wa Km 66 ambayo Serikali iko katika hatua
ya kumtafuta mkandarasi atakayejenga kwa kiwango cha lami.
Ameongeza
kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutaimarisha huduma ya bandari ya
Mbambabay na kupunguza adha ya usafiri kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa Ruvuma
Eng. Lazeck Alinanuswe amesema kuwa kwa sasa wakala unakamilisha zoezi
la kulipa fidia kwa wananchi waliopo katika hifadhi ya barabara wakati
hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa zinakamilishwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa kwanza
kulia) akisalimiana na baadhi ya Madereva wa Malori wanaosafirisha makaa
ya mawe Mkoani Ruvuma.
Naye
Meneja wa Bandari ya Kyela Percival Salama amemueleza Waziri kuwa
pamoja na changamoto ya kukosa wa chombo cha usafiri majini kinachotoa
huduma katika bandari hiyo pia ameomba kuboresha huduma za miundombinu
ya barabara kwa kiwango cha lami ili kuwezesha ufanisi wa bandari.
“Kuimarika
kwa barabara ya mbinga-mbambabay na barabara nyingine za maingiliano
katika bandari hii kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuongeza
fursa za uwekezaji na biashara na Mkoa na nchi jirani”,
Waziri
Prof. akame Mbarawa, yuko katika ziara ya Kikazi Mkoani Ruvuma kukagua
miradi ya Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, Mkoani Ruvuma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia) akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge
(wa pili kushoto) wakati alipokagua uwanja wa Songea Mkoani Ruvuma.
Muonekano wa uwanja wa ndege wa Songea Mkoa ni Ruvuma, ambao uko kwenye mradi wa upanuzi wa viwanja kumi na moja.
Waziri
wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa tano
kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Songea,
Valentine Fasha (wa nne kulia) wakati alipokagua barabara ya kutua na
kuruka ndege katika uwanja huo Mkoani Ruvuma.
Waziri
wa Ujenzi, Uchuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akiteta
Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Muonekano
wa Barabara ya Mbinga-Mbambabay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango
cha Lami unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Kukamilika kwa barabara hiyo
kutachochea uchumi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia bandari ya
Mbambabay. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Mbarawa aitaka TPA kujenga gati
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:53:00
Rating:
No comments: