CCM Yawasilisha Gharama Za Uchaguzi Kwa Msajili Wa Vyama Leo
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) leo kimewasilisha kwa Msajili wa Vyama, hati zake
za gharama ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana, na kuwa chama cha
pili kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.
Ujumbe
wa CCM uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa CCM, Stanslaus Mamilo na
Mwanasheria wa CCM Adamson Sinka na kuwasilisha hati na vielelezo vya
matumizi hayo kwa Mwangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama, Mkuu wa
Masijala Galasia Simbachawene.
Akikabidhi
hati na vielelezo hivyo Mamililo alisema, CCM imelichukua swala hilo
umuhimu mkubwa ndiyo sababu imefanya hivyo ndani ya wakati kwa kuwa mda
wa kuwasilisha matumizi ya gharama za uchaguzi kwa wagombea na vyama
vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 2015, ni Juni 25,
2016.
"Sisi
hatuwezi kuwa kama vyama vingine kwa kuwa ni Tasisi kubwa ambayo haina
budi kufuata kanuni, taratibu na sheria za nchi hasa ikizingatiwa kwamba
CCM ndiyo chama tawala hivyo lazima kionyeshe mfanomzuri ili kiendelee
kuwa chama cha kuigwa ", alisema Mamilo.Mamililo aliwasilisha hati
na vielelezo vya matumizi ya Chama na wagombea wa nafasi mbalimbali
kupitia CCM ikiwemo Urais, Wabunge na Madiwani.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa hati na vielelezo hivyo, Galasia alisema, katika
vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita ni CCM na
ACT-Wazalendo ndivyo ambavyo tayari vimekamilisha bila shuruti sheria ya
kuwasilisha gharama zake za uchaguzi.
Alisema,
uwasilishaji wa gharama hizo ni muhimu sana kwa kuwa ni suala la
kisheria, kwa kuwa vyama au wagombea wanaoshindwa kutimiza sheria hiyo
watachukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa makahamani ambako wakipatikana kwa
upande wa Chama kitafungiwa kushiriki uchaguzi wowote utakaofuatia na
kwa upande wa wagombea mhusika atatozwa faini ya sh. milioni 2, au
kifungo cha mwaka mmoja jela au vyote pamoja.
CCM Yawasilisha Gharama Za Uchaguzi Kwa Msajili Wa Vyama Leo
Reviewed by WANGOFIRA
on
07:08:00
Rating:
No comments: