Gazeti la The Post lafungwa Zambia

 



Gazeti kubwa zaidi la kibinafsi nchini Zambia la The Post, limefungwa kutokana na kutolipwa kwa kodi.

Mhariri wa gazeti hilo aliliambia shirika la habari la AFP kuwa, wafanyikazi walifanikiwa kuchapisha gazeti hilo wakisaidiwa na kampuni ya kibinafasi ya uchapishaji.
Polisi na maafisa wa kukusanya kodi walifunga ofisi za gazeti hilo katika mji mku Lusaka, baada ya kudai dola milioni 6.1 za kodi ambayo haijalipwa.
Gazeti hilo linasema kuwa lilifungwa licha ya kulipa kodi yote
Gazeti la The Post lafungwa Zambia Gazeti la The Post lafungwa Zambia Reviewed by WANGOFIRA on 07:05:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.