BABU WA MIAKA 65 AMBAKA MPWA WAKE WA MIAKA 16 NA KUMPA MIMBA
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi za kumsaka zinaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria.
Bw Mutafungwa amesema, jeshi la polisi katika mkoa huo halitavumilia kuona vitendo vya ubakaji vikiendelea kutokea kwa watu wa aina hiyo ambao wanakatisha maandalizi ya maisha bora ya wanafunzi wasichana.
Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nkuu amesema, mjomba wake huyo alimbaka nyumbani kwake wakati alimpopelekea sola kwa ajili ya kuichaji ili apate nafasi nzuri ya kujisomea nyakati za usiku na ameiomba serikali aendelee na masomo baada ya kujifungua.
Baba mzazi wa msichana huyo Bw Kilasauko Nyuki ameiomba serikali imchukulie hatua kali za kisheria mzee huyo mwenye makazi katika kijiji hicho na majiji ya Arusha na Dar es Salaam ambaye inadaiwa ametoroka baada ya tukio hilo.
Via>>ITV
BABU WA MIAKA 65 AMBAKA MPWA WAKE WA MIAKA 16 NA KUMPA MIMBA
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:12:00
Rating:
No comments: