JPM AMTEUA DR. JIM YONAZI KUWA MKURUGENZI WA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN)

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
   
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 Juni, 2016
JPM AMTEUA DR. JIM YONAZI KUWA MKURUGENZI WA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) JPM AMTEUA  DR. JIM YONAZI KUWA MKURUGENZI WA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN) Reviewed by WANGOFIRA on 10:26:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.