WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.
Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada
ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini
Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza
kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu,
ambao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto) akimuelezea
jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) wakati
Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Kinondoni, jijini Dar es
Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu,
alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia
mwezi Desemba mwaka huu, ambao wananchi hao wamesajiliwa kupitia mpango wa
usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta
(TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed Khamis (wapili
kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji
wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo hicho cha Usajili na
kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam leo.
Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (wapili kushoto-mbele)
akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto mstari
wa mbele) mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya kutembelea ofisi za
NIDA Makao Makuu na ofisi zake za usajili wa taarifa mbalimbali za waombaji wa
vitambulisho, zilizopo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
WAZIRI MWIGULU ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR
Reviewed by WANGOFIRA
on
19:44:00
Rating:
No comments: