FAIDA ZA KWENDA JKT KWA KIJANA WA KITANZANIA

upload_2016-5-21_8-34-17.jpeg
Habari zenu ndugu zangu ;
 
Leo napenda kuzungumzia  na mliobahatika kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza kwenda kambi mbalimbali za jeshi la kujenga Taifa yaani JKT mujibu wa sheria. Utaratibu ulianzishwa na kupitishwa na Bunge tukufu la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2013. 

Ambapo rasmi  suala la kidato cha sita na walimu kwenda JKT lilifanywa la kwa wanafunzi wote na kuwa moja wapo wa kigezo muhimu cha kupata ajira serikalini na hata kwenye makampuni binafsi.

Nashukru na najivunia kuwa miongoni  mwa vijana waliobahatika kupata mafunzo hayo baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka 2014 mwezi wa TANO ambapo nilipangiwa kambi ya MSANGE JKT KAMBI NAMBA 823 KJ iliyopo mkoani Tabora.

Nilishituka sana pamoja na kujua fika kuwa ilikuwa ni lazima kwenda lakini swali moyoni mwangu lilikuwa nitawezaje kuishi maisha haya mapya ambayo sijayazoea. Ambayo wengi usimulia yamejaa mateso na shida za kutosha. 
lakini pia niliuwaza usingizi wangu ambao kimsingi ilikuwa baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha sita kwa muda huo ilinipasa nipumzike ili nijenge afya na kujiandaa kwa maisha ya chuo kwa baadaye. 

sikuwa na mbadala au sababu ya muhimu kunifanya kukimbia au kutokwenda jeshini kwani baada ya kumaliza mitihani yangu, nilipumzika kama wiki tatu hivi. Nikipewa  uzoefu kidogo na rafiki na ndugu na hata wazazi wangu maana na wao enzi za ujana wao walipitia JKT.

hivyo ikawa rahisi kwangu kurudisha moyo wangu na kujiandaa kukabiliana na hali halisi ya jeshi ilivyo. na siku zilipofika niliondoka kwa Amani kutoka Musoma kuelekea Tabora na kisha nikaingia kambini kwa amani pasipo shida yoyote.

nikiwa kwenye gari nilikutana na wanafunzi wenzangu ambao nao walikuwa wanaelekea huko hivyo kuifanya safari yangu kuwa ya raha mstarehe. pia baadhi ya rafiki zangu walipenda sana jeshi na namshukru Mungu ni hivi majuzi wametunukiwa nishani ya ukapteni usu na Amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Nchi ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli.

Nakumbuka  nilifika mida ya jiomi kwenye saa moja hivi giza lishaingia, nilipofika getini nilipokelew kwa ukarimu na Afande Adam, ambaye alinipeleka moja kwa moja hadi jikonio na kupewa Chakula cha kutosha japo nilikuwa nimeshiba.
Nilisikia sauti za wenzangu waliotangulia wakiita mzalendo mzalendo na huku wengine wakicheka na huku pasipokujua kuwa kuwa mzalendo napo ni cheo cha kijeshini. 

Kiukweli maisha ya kweli mwanzoni yalikuwa mapya sana kwani nilichoshangaa zaidi ni kwamba salamu ya kule sio mambo, wala shikamoo tena bali NI JAMBO AFANDE.

Nikakutana na jamaa jeshi limeshawakolea nilichukua siku nyingi mpaka kuwazoea ,kiukweli tulikuwa wengi sana kwani nakumbuka kuwa  nilicheza singe na kwata kidogo japo nilikuwa doja mara moja.

Wadogo zangu, maisha ya jeshi ni mazuri sana kwani nimepata faida nyingi sana ambazo ni;

UZALENDO WA NCHI YANGU; Kwani hadi mda huu nimetokea kuipenda nchi yangu kwa kiasi kikubwa kana kwamba nikikuta mtu anaikashfu serikali hii natamani nimpige lakini kwa kuwa si ruhus kufanya hivyo inabidi nimpe elimu juu ya serikali ya nchi hii.

NIMEFUNDISHWA SILAHA ZOTE, KUZITUMIA NA KUZISAFISHA, ambapo ningebaki nyumbani nisingejua kufanya hivyo, naombeni mwende nanyi mjifunze.

NIMEPATA MARAFIKI WENGI SANA ,ambao wamenifanya kutembea mahala popote Nchini ninauhakika wa sehemu ya kufikia bila shida yeyote na sehemu ya kuishi.

NIMEJIFUNZA USHIRIKIANO,kwani kila kazi tulikuwa tukifanya kwa ushirikiano wa hali ya juu.

NIMEJIFUNZA KWATA,nilifurahi sana kwani nakumbuka nikiwa jeshini kombania yetu ya E-COY  maarufu kama EAGLE COY ilishinda kwata chini ya uongozi afande wepesi kwa jina la utani.

KWA LEO NIISHIE HAPO NIWATAKIE MAANDALIZI MEMA YA KWENDA KUJENGA TAIFA.

FAIDA ZA KWENDA JKT KWA KIJANA WA KITANZANIA FAIDA ZA KWENDA JKT KWA KIJANA WA KITANZANIA Reviewed by WANGOFIRA on 07:17:00 Rating: 5
Powered by Blogger.