WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA ZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim
Majaliwa, amezindua kituo cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya
usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko Mikocheni
jijini Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016.
Kituo hicho kipya na cha kisasa,
kimejengwa kwa ufadhili wa serikali ya Norway na Tanzania, chini ya mpango
wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini.
“Serikali ya awamu ya Tano, iliwaahidi
Watanzania, wakati tukiomba kura, ya kwamba, tutaboresha huduma ya umeme kote
nchini, na leo hii ni ushahidi tosha tunatekeleza kwa vitendo ahadi zetu.”
Alisema Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais wa Tanzania, Mh. Dkt. John
Pombe Magufuli.
Akimkaribisha waziri Mkuu, Waziri wa
Nishati na Madini, Mh. Profesa Sospeter Muhongo amesema, watanzania wanahitaji
umeme tena ulio bora, na sasa kituo hicho ni jawabu la kuwapatia umeme ulio
bora.
“Kati ya vitu ambavyo sitarajii
kuvisikia ni mgao wa umeme, lakini pia bei ya umeme, kuusu bei tutakaa, pembeni
na watu wa TANESCO kulizungumzia hili. “ Alitoa hakikisho Waziri Muhongo.Kwa
upande wake, Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Mh. Kai Mykkanen,
alisema, teknolojia iliyotumika kwenye mitambo ya kituo hicho ni ya kisasa
ijulikanayo kama Distribution SCADA System, na inauwezo wa kutambua hitilafu ya
umeme kwa haraka na hivyo kurahisisha kurekebisha hitilafu hiyo kwa wakati.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
(katikati) na viongozi wengine kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO,
Dkt. Alexander Kyaruzi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt.
Juliana Palangyo,Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, (Waziri
Mkuu), Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen, Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Mhandisi Felchesmi Mramba, wakishangilia baada ya kukata utepe kuashiria
ufunguzi rasmi wa kituo cha cha udhibiti na usimamizi wa mifumo ya
usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam kilichoko Mikocheni jijini
Dar es Salaam, leo Novemba 16, 2016
Waziri Mkuu na wageni wengine
wakitembelea chumba cha mitambo yaudhibiti nausimamizi wa mifumo ya usambazaji
umeme Distribution SCADA System
Waziri Mkuu akitembeela moja ya
mitambo inayopatikana kwenye kituo chicho (Server)
Mtaalam wa mitambo, wa shirika la
Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Bi, Mwajua Turkey, kushoto, akimpatia maelezo
waziri mkuu wakati akitembelea kituo hicho muda mfupi kabla ya kukizindua rasmi
WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA ZA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM
Reviewed by WANGOFIRA
on
19:47:00
Rating:
No comments: