RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya13 & 14

MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA....
    Mama alizungumza kwa hasira huku akiuchukua mkono wangu mmoja na kuuweka kwenye koo lake ili nimkabe afe nikajikuta nikiogopa na mwili mzima ukianza kutetemeka kwani sikuwahi kumuona mama katika hali ya hasira kiasi kwamba anataka mimi nimuue...

ENDELEA...
 .....Machozi yakaanza kunitiririka kwa wingi huku moyo wangu ukijawa na maumivu ni kwanini nilizungumza kitu kama kile,nikautoa mkono wangu koo ni mwa mama na kumkumbatia na kukiweka kachwa chake begabi mwangu na kuanza kumbembeleza taratibu.

“Eddy mwangu kwa nini unataka kuwa kama huyu baba yako?”
“Mama ninakuomba unisamehe sio kusudio langu kuzungumza hivyo”
  
Nikaendelea kumbembeleza mama taratibu hadi akanyamaza na taratibu usingizi ukaanza kumpitia baada ya muda kidogo akalala,Nikachukua shuka lake na kumfunika vizuri kisha nikatoka ndani ya chumba chake huku nikizima taa ya chumbani kwake na kushuka gorofani na kukaa kwenye sofa huku maneno ya mama akiwa anazungumza na dokta yakaaza kunirudia taratibu katika akili yangu huku yakiwa yanapita kama kanda wa video aina ya VHS.Kitu kinacho niumiza kichwa sana ni nani baba yangu na kitu kingine watu wengi wanasema ninafanana sana na baba yangu.

“Au mama atakuwa amechoka ndio maana akazungumza hivi?.........ila hata kama ni kuchoka itakuwaje akamwambia daktari mtu asiye husika katika familia yetu?”

Nikaendelea kujiuliza maswali yasiyo na majibu kiasi ya kujikuta taratibu nikiaanza kupitiwa na usingizi na kujikuta nikilala kwenye kochi.Nikaanza kuisikia sauti ya mama kwa mbali ikiniita taratibu huku akionekana akiomba msaada,Nikayafumbua macho yangu na kuuta mlango wa kuingilia hapa sebleni nikatazama nje na kukuta bado kuna giza jingi.
Nikanyanyuka kwa haraka na kwenda chumbani kwa mama nikakuta mlango wake ukiwa wazi nikaingia na kukuta kuna mwanaume yupo juu yake akimkaba huku kichwani kwake akiwa amevaa maski(Kinyago).Nikachukua chombo cha udongo kilichowekewa uwa la pambo na kwenda kumpiga nalo la kichwani na akaangukia kwa pembeni baada ya kuniona mimi akachomoka na kukimbia sikumjali zaidi ya kumuangalia mama kama yupo sawa au laa.Mama akanyanyuka huku akiwa anakooa huku akiwa amejishika koo.

“Mama unajisikiaje?”
“Vizuri mwangu fungua hiyo droo yangu ya kabati na unitolee bastola yangu”

  Nikafanya hivyo na kuitoa bastola yake kisha mama akanyanyuka kitandani na kuvaa raba zake za kufanyia mazoezi na taratibu tukaanza kutoka ndani kwa umakini wa hali ya juu huku na mimi nikifuata kwa nyuma.Tukashuka chini na kutoka nje kabisa ambapo kwa safari hii mlango ulikuwa umefungwa.Tukazunguka nyumba nzima kutazama kama kuna usalama kwa bahati nzuri kuna usalama.Tukaelekea getini ambapo hukaa askari ila hatukumkuta na wala hapakuwa na kitu chochote kinacho ashiria kuna tatizo lililo tokea katika eneo hilo.“Eddy kimbia kaniletee simu yangu ndani.”
 
  Nikaanza kujikongoja kongoja huku nikipiga hatua za haraka nikaamini kuwa mama amesahau kuwa mimi ni mgonjwa.Nikapanda ngazi kwa mwendo wa haraka kidogo kitendo cha kushika kitasa cha mlango wa kuingilia chumbani kwa mama nikasikia milio mitatu ya risasi ikitokea nje.Nikabaki nikiwa nimesimama huku miguu yote ikiwa inaanza kuishiwa na nguvu.Nikaaona hakuna haja ya kuingia ndani kuchukua simu moja kwa moja nikakimbilia jikoni na kuanza kukitafuta kisu ila sikukiona zaidi ya kuona Umma wa kulia chipsi,nikiona unanitosha kwenda kupambana na kitu chochote bitakacho kutana nacho nje.

 Nikafungua mlango na kujikuta mapigo ya moyo yakianza kuenda mbio huku wasiwasi ukiinza kunikamata mwili wangu kwani katika sehemu nilipomuacha mama sikumuona,Nikajikuta ninaaza kupata kiwewe cha miguu kila nikijaribu kusogea mbele ninajikuta ninashindwa sasa sikujua ni woga ndio unachangia kwani sikujua ni wapi mama yupo.Nikiwa bado nimesimama nikasikia mlio mwengine wa risasi ukitokea nje ya geti kwa mshtuko nusu nijikojolee kwani sikujua huo mlio ni nani aliyepigwa nao kwani kipindi nipo mdogo mara kwa mara baba alikuwa akinifundisha jinsi ya kutambua milio ya risasi pale inapokuwa imempiga mtu au kumkosa na moja kwa moja mlio niliousikia nikajua moja kwa moja risasi iliyolia imetua kwenye mwili wa mwanadamu.
    
 Nikajikaza kiume na kuanza kupiga hatua za kwenda nje ila kwa umakini huku uma wangu nikiwa nimeushika kwa umakini wa hali ya juu huku nikiwa makini kwa chochote kitakachojitokeza huku mwili mzima jasho lilinimwagika.Nikafungua geti dogo taratibu huku nikiwa nimetanguliza kichwa,Nikamkuta mama akiwa amesimama na askari kama watano wakiwa na bunduki zao mikonini huku kukiwa na mtu mmoja akiwa amelala chini huku mwili wake ukiwa unavuja damu nyingi.Nilicho kikumbuka kwa haraka haraka ni nguo alizo zivaa mtuu huyo na kukumbuka ni yule mtu niliyempiga na bakuli la dongo lililo kuwa na uwa la pambo.

“Alafu bado kijana mdogo sana”
“Ndio huyu nahisi ametuwa na mtu wa humo ndani kwako kwa maana haiwezekani ajiamini kiasi kwamba ya kujua moja kwa moja chumani kwako”
“Hilo usemalo litakuwa na ukweli ndani yake”.

 Mama akaendelea kujadiliana na askari wanaolinda eneo tunaloishi akiwemmo na askari wetu huku mama akimshushia lawama askari wetu ni kwa namna gani mtu anaingia ndani pasipo yeye kufahamu,askari wengine wakaja na gari lazo na kuchukua maiti huku wakimchukua askari wa getini kwetu kwenda kumuhoji maswali.

                                                      ***                       
  Mama akamfungulia kesi ya mauaji Manka huku lengo lake kubwa ni Manka kwenda kufungwa kifungo cha maisha,Siku ya kesi kusikilizwa ikawadia huku mahakamani kukiudhuriwa na watu wachache baadhi yao wakiwemo ndugu wa upande wa Manka akiwemo dada yake na pamoja na mwalimu Mayange.Tangu tukiwa nyumbani  mama aliweza kuzungumza kitu kitakacho muhukumu Manka.Ila moyoni mwangu nikaanza kuhofia endapo atasema tulifanya mapenzi itakuwa aibu kwangu na mama yangu.Watu wakiwa wanaanza kuingia ndani ya chumba cha mahakama mimi nilikaa nje huku nikimdanganya mama kuwa kuna mtu nina mpigia simu na muda si mwingi nitaingia ndani.Alipoingia nikaelekea katika sehemu yenye mtuhumiwa na kawaonga kila askari elfu hamsini na walikuwa wanne ili wanipe nafasi ya kuzungumza Manka ambaye kwa wakati wote sura yake ilijaa machozi na huzuni hadi na mimi nikajikuta nikiwa na huzuni moyoni mwangu.

“Eddy nakuomba unisaidie katika kesi hii wewe ndio kiongozi wangu wewe ndio unaweza kuzizima ndoto zangu katika maisha yangu……..Eddy sikukusudia kukuua na wala sikuwa na lengo baya la kukudhuru yote yalitokea kwa sababu ninakupenda Eddy na sikujua ni jinsi gani ya kukushawishi ili unipende nilidhani utanichezea na kuniacha”

Manka alizungumza kwa huzuni huku akilia kwa uchungu akionekana kujutia kwa kitu alicho kifanya
“Sasa Manka kwa nini hukuwa mstaarabu mpaka tushikiane bastola kwa kitu kidogo”
“Eddy nakuomba unisamehe ila nakuomba unisaidie katika hili swala”

“Manka siwezi kukusaidia katika lolote inakubidi na wewe ulipe kwa kitu ulichonifanyia”
“Kaka muda umekwisha anatakiwa kuingizwa kizimbani”
Askari alizungumaza na kunifanya nianze kupiga hatua za kutoka nje ila Manka akaniwahi na kunishika mkono huku akilia.

“Eddy hata nikinyongwa au kuhukumiwa kifungo cha maisha ila tambua kuwa ninazawadi yako nitakayo kupa kama ukumbusho katika maisha yangu”.

 Nikautoa mkono wake kisha nikaondoka na kwenda katika chumba cha mahakama,Manka akaingizwa na askari huku akiwa analia huku sura yake akiielekeza chini ila mara kwa mara alikuwa ananitazama.Kesi ikaanza kusikilizwa huku mawakili wa pande zote mbili wakianza kumuhoji maswali Manka na kila kitu ambacho Manka alicho kuwa akiulizwa hakujibu zaidi ya kulia.Ikafika zamu yangu ya kuhojiwa maswali na nikaanza kuhojiwa swali moja baada ya jengine.

“Mr Eddy ulifwata nini kwa nyumbanni kwa Mwalimu Myange?”
“Nilikwenda kuchukua pesa ya matumizi”
“Ulikuwa una ruhusa ya kwenda kwake?”
“Hapana?”
“Kwahiyo ulitoroka shuleni kwenu?”
“Ndio”
“Basi ninaweza kusema kuwa wewe ni jambazi umwekwenda kuvamia nyumbanni kwa mwalimu mayange ndio maana Manka akakupiga risasi?”.

Wakili wa upande wa Manka akaendelea kunibana na maswali yake ambayo ni magumu kupita maelezo nikamtazama Manka kwa jicho la kuiba na kumkuta sura yake akiwa bado ameielekeza chini.

“Mimi sio jambazi na Manaka si mtu aliye nipiga risasi”
Miguno ikaanza kusikika ndani ya mahakama nikamtazama mama nikaona jinsi sura yake ilivyo badilika gafla na kuwa na hasira,kutokana na minong’ono hakimu ikamalzimu kugonga nyundo mezani na kuwaomba watu wakae kimya.

“Kwa nini unasema kuwa Manka siye aliye kupiga risasi na kwa madai yenu ya washtaki mnasema Manka anahusika na wewe kupiga risasi?”

“Narudia kusema Manka hausiki na kitu chochote katika kunipaga risasi wala kunijeruhi mimi.Nilikwenda nyumbani kwa Mwalimu Mayange na kukuta hayupo ila nikamuomba Manka nimsubiri mwalimu hadi atakapo rejea ila kutokana alipata safari ya gafla yeye na mke wake ikanilazimu kuondoka na kupita njia za vichochoroni ndipo nikakutana na majambazi walio waliokuwa wakinilazimisha nitoe pesa ila kutoka na ubishi wangu mmoja wao akanipiga risasi ya kifua na baada ya hapo sikujua ni kitu gani kinacho endelea”.

 Mahakama nzima watu walikaa kimya huku wakinisikiliza ninavyo zungumza kidogo nikamuona Manka akiwa na tabasumu usoni mwake.

“Kwa hiyo Manka sio mtu aliye kupiga risasi?”
“Wewe vipi kwani hukunisikia nilivyokuwa nikizungumza au?”
Nilizungumza kwa jazba kidogo na umfanya wakili anaye nihoji kuanza kujichekesha chekesha
“Sijasikia labda wewe ndio unaweza ukawa unaidanganya Mahakama tukufu Mr Eddy”
“Sijamdanganya mtu na Manka hajanipiga risasi na muheshimiwa hakimu moja ya sura za majambazi nilio waona mmoja kama ni huyo wakili anayenihoji maswali yake ya ajabu ajabu”.

“Wewe kijana kama umekosa kitu cha kuzungumza sema kuliko kuanza kunipakazia vitu vya kishenzi”
“Kwa hiyo mimi mshenzi si ndio….Hakimu ndivyo jinsi mnavyowafundisha hawa mawakili wenu kutukana watu?”
Nilizungumza huku nikiwa makini na kuzidi kumchanganya wakili ambaye nimeamua kumuuzia mashtaka.
“Muheshimiwa hakimu huyu kijana atakuwa amechanganyikiwa ninaomba mahakama yako akapimwe akili”.

“Nani akanipime akili kama si wewe uliyenipiga risasi na wenzako na mbaya zaidi wewe si ulikuja kunichimba mkwara hapo nje kuwa nikikutaja utaniua au sio wewe?”

 Hakimu akalazimika kuihairisha kesi na kuomba turudi ukumbini muda wa mchana kwa ajili ya keundelea kwa kesi,Mama hakunisemesha kitu hadi tukatoka nje ya mahakama na kuingia ndani ya gari

“Hivi wewe mtoto ni kitu gani kilicho kupata?”
“Mama hakuna kilicho nipata zaidi ya kwamba Manka hakunipiga risasi ila ni yule wakili na alikuwa na wezake wamelewa”
“Sasa mwangu mbona hayo yoyote hukuyazngumza wakati unatambua fika kwamba Manka ninamchukia kama baba yake?”

“Baba yake yupi?”
“Ok tuachane na hiyo mada”
“Mama tena nakuomba unaimbie ni kitu gani kinacho endelea kati yako wewe na baba kwani niliwasikia maneno yenu yote kuanzia mwanzo hadi mwisho”
“Unataka kujua ukweli si ndio ni hivi Manka ni mtoto wa baba yako alizaa na mwanamke mwengine kabla hajakutana na mimi”.

    Nikaanza kuhisi kijasho kikianza kunimwagika huku mwili ukinza kunitetemeka huku nikaanz kufikiria ni jinsi nilivyokuwa nilifanya mapenzi na Manka
“Kwa hiyo nilifanya mapenzi na dada yangu?’
“Unasemaje wewe?”

 Nlishtuka baada ya mama kuniulizwa swali ambalo nilijikuta nikilopoka bila kutarajia kuwa nitazungumza kitu kama hicho,nikabaki nikimtazama mama huku naye akinitazama kwa macho ya uchungu na hasira


                               *****SORY MADAM*****(14)
   
 “Hapana mama sijasema kitu chochote”
“Ujasema kitu chochote wakati umezungumza hicho ulicho kizungumza?”
“Mama tupotezee hiyo mada”
“Eddy Eddy wewe lete huo ujinga wako tuu na ole wako nichunguze hilo swala alafu nijue ni kweli oune jinsi itakavyokuwa kama sintokufunga”.

 Mama alizungumza kwa hasira huku akishuka ndani ya gari na kuelekea sehemu aliyoingizwa Manka.Sikujua atakwenda kuzungumza nani ikanilazimu nishuke ndani ya gari na kumfwata kwa haraka,nikamkuta mama amesimama na Manka huku akimuonya.

“Nisikie siku una uhusiano na mwangangu utanitambua mimi ni nani hapa si anajifanya anakutetea ila ukiingia ndani ya mikono yangu utajuta kuzaliwa”
“Mama mbo……”
“Tena na wewe funga bakuli lako nenda nikukute kwenye gari”
“Lakini mam……”
“Hakuna cha lakini nimekuambia funga bakuli lako na sihitaji uzungumze upumbavu wowote sawa.Angekuua huyo ndio ungefurahi si ndio?”
 “Ila mama si nimeshasema Manka hausiki na kitu chochote”.
  
 Mama akanitazama kwa jicho la hasira kisha akanisonya na kutoka huku akitembea kwa hatua ndefu kurudi kwenye gari huku mlinzi wake akimfwata kwa nyuma akimtuliza jazba.Wakati wote mama alipokuwa akizungumza Manka alikuwa ameinama chini huku analia kwa uchungu,nikamsogelea taratibu na kumkumbatia japo mikono yake imefungwa pingu kwa mbele.

“Eddy niache tu nikafungwe mama yako amesha tengeneza chuki juu yangu”
“Manka ni maneno gani unayoyazungumza eti?? sipo tayari iwe kama hivyo nahitaji utulize akili katika hili nakuomba tena sana mmmm”
“Eddy hata nikiwa huru sintoweza kuwa na uhuru kama mwazonni….Laiti baba yangu angekuwapo nisinge nyanyasika kiasi hichi”
“Kwani baba yako nyupo wapi?”

“Ni historia ndefu Eddy ila kwa ufupi baba yangu ana uwezo mkubwa wa kiuchumi ila alimtelekeza mama baada ya kunizaa mimi……….ila sijui ni wapi alipo japo ninasikia sikia amepandishwa cheo kazini kwake”
“Ulisha wahi kukutana naye hizi siku za karibuni?”
“Hapana  mara ya mwisho kukutana naye nilikuwa na umri wa miaka mitano kuanzia hapo nina msikia sikia”.
  
Nikajikuta ninapata maumivu mengi moyoni mwangu huku mawazo ya kwa nini baba anafanya hivi yakitawala kichwani mwangu.
“Eddy mama yako anachokizungumza  ni kweli nakuomba uniache nikafie jela”
“Manka acha kuzungumza kitu kama hicho ila tambua kuwa nipo upande wako hadi dakika ya mwisho”.

Nilizungumza na kuondoka na kumuacha Manka akibaki ananishangaa.Muda wa kuingia mahakamani ukawa tayari umesha wadia sikuhona haja ya kumsubiria mama kuingia naye kwenye ukumbi wa mahakama nikatangulia mwenyewe na kumkuta mwalimu Mayange na familia yake wakiwa wamekaa kwa masikitiko.

“Eddy”
Mwalimu Mayange liniita na nikamfuata katika sehemu waliyokaa.
“Eddy mwanangu nakushukuru kwa masaada wako japo tunasubiria majibu ya mahakama”
“Usijali mwalimu Mungu atasaidia yatakwisha”
“Kumbe mama yako ni waziri?”
“Ndio”
“Hongera”
“Asante”.

Nikaondoka na kwenda kukaa katika eneo nililokuwa nimekaa mwazoni na baada ya muda kesi ikaanza,kutokana muhusika mkuu nilikataa Manka kuwa sio muhusika ikalazimika kesi kufutwa na Manka kuachiwa huru.Upande wa familia ya Manka ikatawaliwa na furaha ila kwa upande wangu mama amekasirika.

“Kwenye gari langu hupandi na utakuja kwa miguu”
“Mama….
“Hakuna cha mama, Zuhura hebu mpe alfu ya daladala”
“Sawa bosi”
Mlizi wa mama akafungua kipochi chake na kunipa alfu moja ya daladala kisha wao wakaingia ndani ya gari na wakaondoka nikabaki nimesimama ninawashangaa kwani sikuamini kama mama anaweza kunifanyia kitu kama hicho.Nikiwa bado sijui cha kufanya nikasikia sauti ya Manka ikiniita kwa nyuma nikageuka na kumkuta amesimama huku akiwa na tabasabu usoni mwake.

“Eddy nashukuru kwa msaada wako yaani sijui hata nikushukuruje”
“Usijali best yangu”
“Ila Eddy nina zawadi yako kama nilivyokuambia pale mwazoni”
‘Una zawadi gani?”
“Nina ujauzito wako”Kusema kweli mapigo ya moyo nikahisi yamepoteza muelekeo na kunifanya mwili mzima kuanza kuzizima kiasi kwamba jasho likaanza kunimwagika huku mdomo ukiwa mzito kuzungumza kitu ninacho taka kukizungumza hadi Manka akahisi kitu.

“Eddy una tatizo?’
“Hapana…..mnarudi Arusha leo?”
“Ndio ninamsubiria shemeji aje kutuchukua amelipeleka gari gereji”
“Ahaa basi Mungu akibariki hilo swala la mtoto tutakuja kulizungumza huko Arusha”
“Lakini mbona unaonekana kama huna furaha nilivyokuambia kuwa mimi ni mjamzito?”
“Haaa nimefurahi ila tutatafuta muda tulizungumze”

  Tukaagana na Manka kisha mimi nikaondoka na kumuacha akazungumza na ndugu zake kisha,Nikakodi boda boda ya pikipiki hadi nyumbani nikamuacha jamaa getini nikingia chumbani kwangu kumchukulia pesa ambayo ilipungua kwenye malipo yake kisha nikarudi ndani na kumkuta mama sebuleni akionekana akinisubiri.Nikaanza kupandisha ngazi za kwenda ndani kwangu.

“Wewe Eddy”
“Naam”
“Hebu shuka hapa”
 Nikashuka na kukaa kwenye moja ya sofa kisha na yeye akakaa kwenye sofa jengine.
“Hebu wewe mtoto niambie ni nani aliye kupiga risasi?’
“Mama kile nilicho kizungumza mahakamani ndio hicho hicho”

“Ila Eddy manangu kwanini siku ya kwanza nilivyo kuuliza ukasema Manka ndio muhusika?”
“Hapana labda nilikosea”
“Kukosea tena mwanangu…..Ila na kwanini ulisema umetembea na Manka?”
“Ahaaa mama ulinisikia vibaya”

“Eddy Eddy mwanangu jua kuwa mimi ni mtu mzima na kila unachopitia,mimi pia nilishapitia kipindi ninakua sasa usitake kunidanganya hebu niambie ukweli mwanangu ni kweli Manka ulitembea naye?”
“Sijatembea naye wewe si umesema ni dada yangu?”
“Ndio ni ndugu yako……Kachukue begi lako la nguo dereva akupeleke shule”

Mama jioni yote hii dereva anipeleke shule?”
“Maamuzi ndio hayo kavae nguo zako za shule dereva akupeleke Arusha”
“Lakini mama sijapona vizuri”
“Hujapona vizuri au unataka kujidekeza dekaza kumbuka kuwa wewe ni A level tena mwenyewe unajiita PCB sasa sijui huko shule kama unasoma au ndio kurukaruka vaa upelekwe shule”.
  
Kitendo cha mama kuniambia nijiandae nirudi shule kikanikosesha amani katika moyo wangu na sikuwa na jinsi zaidi ya kujiandaa na taratibu ili dereva anirudishe.Hadi namaliza kujiandaa ikawa imeshatimu saa kumi na moja jioni.Nikabeba begi langu la nguo na kulipakiza ndani ya gari.

“Eddy nataka huko shule ukasome sihitaji michezo ya kijinga jinga tambua kuwa wewe umesha kuwa mtu mzima unapaswa kuaanza kufikiria maisha yako na ya wanao ila sio kufanya ujinga kama ulio ufanya”
“Sawa mama”
“Kama mutakuwa munachelewa mutalala kwenye Hotel yoyote njiani”
“Sawa”.

Mama akanipa kiasi cha kutosha cha matumizi ya pesa ya kutumia shukeni pamoja na pesa ya matumizi njiani na safari ikaanza,kutokana na foleni iliyopo jijini Dar es salaam ikatifanya tusimame simame san njiani
“Kaka naomba niendeshe niendeshe gari”
“Ningekupa mdogo wangu ila huna leseni”
“Kwani usiku huu ni trafki gani atakaye tusimamisha njiani?”
“Mbona wapo wengi hii ni barabara ya mkoani ni lazima tutawakuta wengi”
“Sawa”

 Safari ikaendelea huku nikiwa nimelala kwenye siti ya gari na kumuacha dereva kufanya kazi yake.Dereva akaniamsha na nikakuta tumesha fika katika sehemu moja inaitwa Mombo kwenye hoteli moja inaitwa Liverpool,tukaingia na kuapata chakula cha usiku na tukarudi dani ya gari na safari ikaanza.Kutokana sikuwa na mazoea na huyu dereva mpya wa mama nikaona ni bora kulala kwani sikuwa na chakuzungunza naye.
Nikastushwa na breki kali za gari letu na kunifanya nishtuke na nikamkuta dereva akijitahidi kuikwepa gari ndogo aina ya PREMORE inayopinduka pinduka katikati ya barabara.Gari ikatulia na kuingia ndani ya mtaro ikamlazimu dereva kulisimamisha gari letu mbele kidogo kutoka sehemu gari ndogo ilipo angukia.Mimi na dereva tukajikuta tumetulia kama kwa dakika tano huku kwa upande wangu mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba nikashindwa nifanyaje.

“Kaka imekuwaje?”
“Mmmmmm?”
“Imekuwaje?”
“Nilikuwa ninamuomba dereva wa lile gari anipishe njiani ila akawa anashindana na mimi katika akukimbiza gari…..ila kutokana na taa za gari zangu kuwa uwezo mkubwa basi nikajikuta ninamuwashia zote ndio jamaa akaanza kijichanganya changanya hadi akadondoka”.

“Mmmmm huu msala tusepe zetu basi”
“Mmmm siwezi hata kuendesha gari”
“Ngoja mimi nije kuendesha”.

  Nikashuka ndani ya gari nikiwa ninazunguka nyuma kwenye gari ili niiingie kwenye siti ya dereva nikapata mshtuko baada ya kumuona msichana akianza kujivuta taratibu kutoka ndani ya gari huku akilia kwa maumivu makali ikanibidi nianze kupiga hatua za kwenda kumsaidia ila kadri jinsi nilivyozidi kwenda moyo ukazidi kunipasuka kwani mtu anaye jitahidi kujitoa ndani ya gari ni Manka....

ITAENDELEA......
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya13 & 14 RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya13 & 14 Reviewed by Unknown on 22:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.