RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11 & 12 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

   MTUNZI:EDDAZARIA G.MSULWA
 
ILIPOISHIA
 

.....Manka akamaliza kuvuta sigara yake kisha akatoka chumbani huku bastola yake ikiwa mkononi.Nikaona nikiendelea kujilaza kitandani utakuwa ni ujinga wa karne.Nikajivuta juu kidogo na kuanza kuifungua kamba ya mkono wa kulia kwa kutumia meno japo ninapata maumivu ila nikayapotezea,Nikafanikwa kuifungua kamba kisha kwa haraka nikaifungua kamba ya kumkono wa pili na kumalizia kamba za miguuni kala sijanyanyuka kitandani nikajikuta tunatazamana na Manka huku bastola yake akiwa amenielekezea kwangu.Nikamrukia Manka kabla hata sijamfikia nikstukia kitu chenye ncha kali na chamoto kikipenya ndani ya kifua changu na kuningusha chini.....

ENDELEA....
.....Maumivu makali yakanitawala katika kifua changu nikajishika kwenye kifua changu na kugungua kuna damu zinanitoka ikanibidi niukaze mkono wangu ili kuzuia damu nyingi kuendelea kuvuja katika sehemu risasi ilipo pita.Manka akaanza kuweseka huku akiwa kama haamini kwa tukio alilo lifanya.Akaitupa bastola chini na kupiga magoti kuangalia eneo aneo alilo nijeruhi kwa risasi

“Eddy nilikuwa ninakutania”
Manka alizungumza huku akilia na kuonekana kuchanganyikiwa kwa kitendo alicho nifanyia.Taratibu nikahisi nguvu zikiniishia huku mwili ukizizima kwa kukosa uwezo wa kufumbua machona taratibu nikajikuta hali nzito ambayo sikuwahi kuipata katika maisha yangu ikiutawala moyo wangu.

                                           ***
 Macho yangu yakafunguka na kujikuta Mama akiwa amekaa pembeni yangu huku puani kwangu nikiwa na mashine ya kupulia.Mama alipo niona nimefungua macho yangu akaanza kuliita jina langu na nikamuitikia kwa sauti ya chini

“Mwanangu unajisikiaje?’
Nikataka kunyanyuka ila nikashindwa na mama akanirudisha chini na kugundua kuna bandeji kuwa nimefungwa kwenye kifua changu.Kumbukumbu zinanikumbusha dakika za mwisho nilikuwa na Manka ila kuanzia hapo sikuelewa kitu kilicho enedelea hadi mama akawa pembeni yangu.

“Mama nipo wapi?”
“Mwanangu upo hospitalini?”
“Nani kanileta?
“Ni story ndefu kidogo mwanangu ila kwa sasa pumzinka nitakuadisia ukipata nafuu”

   Simu ya mama ikaita akaitazama kwa muda kisha akaipokea na nikamuona sura yake ikiwa imebadilika kidogo na kuwa sura ya hasira

“Ndio ameamka”
“Godwin nakuomba unielewe hapa huna mtoto na huyo mwanao aliye mfanyia mwanangu hivi nilazma nimfunge”
“Ahhhh kwahiyo wewe ndio umemtuma amuue mwanangu si ndio?”

“Sasa lazima nimfunge na kumbuka kuwa tangu mwanangu akiwa utotoni hukuwa na mapenzi naye sasa naomba umuache na wala sihitaji urudi uje umuuone”

 Mama akakata simu huku akiachia msunyo mkali,sasa sikuelewa anazungumza na nani na kumfokea kiasi hicho
“Mama unazungumza na nani?”
“Ahaaa mwanangu nitakuambia”

Mama alanijibu huku akiwa anatabasamu kisha akanibusu katika paji la uso wangu.Simu yake ikaiita tena na ikamlazimu kutoka nje.Sikutaka kujisumbua mama anamfokea nani niahisi watakuwa ni watu wa serikali anao fanya nao kazi.Mama akarudi na kukaa karibu yangu huku machozi yakimlenga lenga akionekana kuwa na hasira kubwa na tangu nizaliwe sikuwahi kumuona mama akiwa katika hali kama hiyo.

“Mama nipo hospitali gani?”
“Ni KCMC”
 Mlango ukafunguliwa akaingia mzee wa makamo akiwa amevalia nguo za polisi huku akiwa na vyeo vingi
“Habari yako mheshimiwa?”
“Salama vipi mumesha mkamata aliye sababisha hili tukio?”

“Ndio muheshimiwa ila ninashindwa kuelewa kwani mzee ananiambia nimuachie huru ili we……”
“Nisikilize wewe mimi si ndio nimetoa  amri yule binti kukamatwa?”
“Ndio”
“Sasa mbona unaniletea Kiswahili.Muwekeni ndani hadi mimi nije sawa”
“Sawa mkuu”

Askari akatoka na kutuacha ndani ya chumba na ukimya ukatawala huku mama akonekana kusongwa na mawazo na mara kwa mara akawa anasunya sikujua kinacho mfanya asunye ni nini.

 Nikakaa hospitali kwa wiki moja nikapewa ruhusa japo sikuwa nimepona vizuri.Safari ya kwenda uwanja wa ndege wa KIA ikaanza huku dereva anayemuendesha mama akiwa makini katika uendeshaji wake kutokana Dokta ameniambia nisifanye kazi ngumu wala kupata mitingishiko ya aina yoyote kwani kidonda changu kinaweza kisipone kwa haraka.Tukakuta ndege ya kukodi ikiwa tayari kwa ajili yetu mimi na mama.Tukapanda na dereva akaondoka na gari ya mama na tukaahidiana naye atatukuta nyumbani.Safari ikaanza taratibu huku ndege aina ya Fast Jet tuliyoipanda ikizidisha kasi kadri muda unavyo kwenda tukiwa angani

  “Pole kaka”,Muhudumu wa kike wa ndege akanipa pole huku akiniwekea juisi kwenye kimeza kidogo kilichopo mbele yangu
“Asante”
“Muheshimiwa huyu ni mwanao”
“Ndio ni mwangu wa kwanza na wamwisho”
“Aisee mtu akikutizama wala hata amini kama unamtoto mkubwa kiasi hichi”

“Unajua kipindi sisi tulipokuwa tunamaliza kidato cha sita mika ya themanini tulipelekwa jeshini sote na ilitusaidia kuweza kuzilinda afya zetu ni tofauti na hao kina Eddy mtu nikimwambia mwanangu ana miaka 20 haamini”
“Mmmm mama umekosea nina miaka 21”

“Sasa sibado haijatimia”
“Sasa muheshimiwa nyinyi si mupo huku ngazi za juu kwanini musirudishe sheria ya wanafunzi wanao maliza kuingia jeshini?”

“Ile imerudishwa sasa sijui huku mwanagu kama ataweza kwa maana mmmm”
“Mama wewe unaniona mimi nimeoza sana”
“Wewe hujioni”

Tukacheka sote na safari ikaendelea,haikuchukua muda sana kutua katika uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere.Gari ya serikali ikaja kutuchukua na kutupeleka nyumbani maeneo ya Masaki.Nikakumbuka kuna kitu ninakihitaji kukijua vizuri kutoka kwa mama kwani kila nilipohitaji kumuuliza nilijikuta nikisahau

“Mama hivi pale hospitalini nilifikaje?”
“Eddy mwanagu hata hatujapumzika umeanza kwa maswali?”
“Ndio ama nataka kujua?”
“Kavue nguo zako chumbani kwako upumzike kisha wakati wa jioni tutazungumza ngoja mimi niende ofisini jana kuna kazi niliiacha”

“Kwani mama jana ulikuja ofisini?”
“Ndio kila siku nilipokuwa ninakuja hospitali nilikuwa ninalala Dar asubuhi ninakuja kwa ndege jioni au mchana ninarudi kwa ndege”

“Mmmmm mama mbona nyumba ipo kimya dada wa kazi yupo wapi?”
“Nimemfukuza”
“Kwa nini?”
“Nitakuja kukuambia jioni nikitoka kazini”

Mama akaondoka mimi nikaelekea chumbani kwangu,sikukuta kuna mabadiliko ya aina yoyote tangu nilipo kiacha pindi nanakwenda shule.Nikaingia bafuni nichukua taulo na kulichovya kwenye maji na kuanza kujisujgua sehemu ya mwili kwani ndio oga yangu tangu nikiwa huspitalini hii ilisaidia kidonda kuto kuingia maji.Nikamaliza na kurudi kitandani kutokana nimeshiba nikaamua kulala.

Nikaamka mida ya saa moja jioni na kutoka chumbai kwangu na kumkuta mama akiwa anaandaa chakula.Nikamsalimia na kukaa kwenye moja sofa zilizopo katika sebule yetu.

“Umekunywa zile dawa za kutuliza maumivu?”
“Hapana?’
“Kwa nini wakati unatakiwa kuzinywa kila jioni?’
“Mama sibado sijala.Nikila nitameza”
“Unanjaa nikupakulie chakula?”

“Mmmm nitakula baada ya kuzungumza na wewe”
“Eddy yaani mwanangu ukishikilia bango kitu yaani hadi kikamilike”
“Ila mama hiyo tabia si nimeridhi kwako”

“Kwenda zako mimi sina tabia za king’ang’anizi kama wewe”
    Mama alizungumza huku kija kukaa karibu yangu na kuanza kukichunguza kidonda changu kikiwa ndani ya bandeji kubwa iliyo zungushwa nusu kufua na kufungiwa kwa mgongoni

“Alafu hicho kidonda ukikitia maji kitachelewa kukauka”
“Sijakitia….eeehe mama kwanza swali langu la mimi nimefikaje pale hospitalini ujanijibu hadi leo?”

“Pale hospitalini ulipelekwa na wasamaria wema ambao walikuokota pembezoni mwa mto huku ukiwa umevalia suruali ya jeans na ulikuwa kifua wazi.Kwa mashuhuda nilio zungumza nao katika kituo cha polisi waliseama ulitupwa mida ya saa kumi na moja asubuhi na binti aliyekuwa na pikipiki”

“Sasa ikawaje?”
“Kuna bibi alikuwa yupo na mjukuu wake wa kiume walikuwa wakielekea shamba ndio wakakuona pembezoni ya mto huku mtu waliyemuona akiwa anakimbia na pikipiki……Unamjua mtu huyo?”

 Swali la mama likaniweka njia panda huku nikijiuliza maswali ni nini nimjibu mama kwani nikisema nina mjua ataniuliza ni nani na nikisema simjui atasema nilikuwa ni wapi ninatoka wakati wa usiku

“Ninamjua”
“Ahaaa basi baada ya watu hao kukuwahisha hospitalini kwani hali yako ilikuwa mbaya sana ikawalazimu madaktari wapewe namba ya baba yako na mmoja wa waalimu aliyedai ni shemeji wa yule binti kisha baba yako ndio akanipigia mimi”

“Alafu mama nilikusikia kama ukibishana na simu kuwa kuna mtu alimtuma yule binti aniue?”.Mama akakaa kimya huku akinitazama kwa macho yaliyojaa masikitiko na kwa mbali machozi yakaanza kumlenga lenga.

“Mwanangu kuna historia ndefu sana unatakiwa kuijua ila kwa kipindi hiki nakuomba usome kwa juuhudi sana na uaache michezo”

“Mama na hisoria gani?”
“Utakuja kuijua tuu”
“Mama nataka kuijua kwani mama una mtoto mwengine zaidi yangu wa kumwambia mambo yanayohusu familia yetu?”

 Mama akanitazama kwa macho yaliyo jaa uchungu na machozi yakaanza kutapakaa kwenye uso wake na kunifanya na mimi nimpokee kwa machozi yalioanza kunichuruzika na kwa mistari mistari kwani mara ya mwisho kumuona mama analia ni miaka kumi iliyopita siku ya kifo cha mama yake.

“Eddy nakuomba uwe na moyo na koo la kuvumilia hiki nitakacho kuambia kwani kinahitaji moyo wa ujasiri na nisiri ambayo sijawahi kumuambia mtu wa aina yoyote zaidi yako na ninakuambia hivi kwa sababu wewe ni mwangu wa pekee”
“Niaimbie mama”

“Eddy nilikutana na baba yako kwenye ajali moja ya basi iliyotokea kipindi mimi ninaelekea chuo katika kumaliza mafunzo ya mwisho ya udaktari.Katika ajali ile watu wengi walijeruhiwa na kama sijakosea ni watu wawili tuu walipoteza maisha.Mimi namshukuru Mungu sikupata majeraha makubwa zaidi ya michubuko midogo midogo ila kwa upande wa baba yako yeye alipata majeraha makubwa sana katika maeneo ya kiunoni na kutokana mimi nilikuwa ni daktari wa upasuaji basi nilijumuika na madaktari wezangu kumfanyia baba yako upasuaji chini ya kitovu ambapo tulikuta mirija yake ya uzazi imeharibika na tukashauriana na madaktari wezangu ambao walinishangaa kuniona nina uwezo mkubwa wa kumfanyia mtu upasuaji japo kuwa nilikuwa bado ni mwanafunzi tukaona ni vyema tukamtoa……..”

Mapigo ya moyo yakanipasuka na kujikuta nikikaa vizuri kwenye sofa na kumtazama mama ambaye uvumilivu unamshinda na kujikuta akiendelea kutokwa na machozi.Mama akameza fumba la mate kisha akaendelea

“Tuliichoma sindano mirija yake ya uzazi ili kuwatoa bacteria ambao wangeweza kushambulia mirija hiyo kwa jinsi ilivyokuwa imeharibika.Lakini mwanangu kusema kweli ile sindano haikuwa nzuri kutokana inamfanya mwanaume kukosa uwezo wa kuzalisha mbegu zenye nguvu zitakazo mpelekea mwanaume kumzalisha mwanamke”

 Nikajihisi mwili mzimwa kupoteza nguvu kutokana na maelezo ya mama na moja kwa moja hisia za baba niliye naye sasa hivi si baba yangu zikaanza kuutawala moyo wangu na kujikuta nikiwa mapigo ya moyo yakianza kunienda kwa kasi hadi na kwa maumivu ya kifua yanayotokana na jeraha la risasi yakanisababishai kizungu zungu kikali kilichonipelekea kujilaza kwenye kochi na nikaanza kuliona giza kubwa likitawala macho yangu kama ilivyokuwa siku niliyo pigwa rasasi na Manka....

                                           *****SORY MADAM*****(12)
........Nikafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nimelala kwenye sofa jengine lililopo sebleni huku mama akiwa pembeni yangu pamoja na mzee mmoja ambaye nilikuwa  nikimuonaga akija kumtibu mama kipindi akipandwa na presha.Mama akabaki akinitazama huku sura yake ikiwa haina tabasamu wala huzuni

“Kijana unajisikiaje?”
“Afadhali kidogo”
“Kwa sindano niliyokuchoma itakusaidia na utakuwa sawa kwani ni mshtuko mdogo uliupata”
“Eddy nikuletee chakula mwanangu?”
“Ehhee ila usinitilie chakula kingi”

“Inakubidi ule ili nguvu zikurudie mwanangu wewe ujioni mwili ulivyoisha tofauti na ulivyokuwa ukienda shule”
“Sawa mama ila chakula kidogo kitanitosha”

   Mama akaondoka sebleni na kuelekea kwenye meza ya chakula na kunipakulia chakula na kurudi nacho nilipokaa
“Haya nyanyuka sasa nikulishe”
“Mmmm mama nitakula mwenyewe”
“Sawa”
“Muheshimiwa naona hali ya mwanao sasa imekuwa nzuri ngoja niwaache”

“Dokta mbona unakimbia wakati chakula kipo mezani?”
“Muheshimiwa yaani pale uliponipigia simu nilikuwa mezani ninakula kwahiyo hapa nipo sawa”
‘”Jamani dokta kaa basi ule hata vijiko viwili vitatu”
“Muheshimiwa hapa ni sawa na nyumbani kwahiyo siku yoyote nitakuja kula tena na sasa hivi upo wizara yetu ya afya basi ninajisikia faraja kwa hilo yaani ni zaidi ya kula”

“Sawa ila na wewe siku utanialika kwako halafu sintokula”
“Muheshimiwa sasa huyo yatakuwa ni malipizo kwani si mara nyingi huwa ninakula chakula hapa…….ila nimekumbuka kitu muheshimiwa”
“Kitu gani?”

“Unajua muheshimiwa Raisi alipo kuhamishia kutoka uwaziri wa maliasili na utalii na kuwa waziri wa afya nikaona kidogo kile kilio chetu kitakuwa kimesikika kutokana nitakuwa na fursa ya kuzungumza na wewe pamoja”

“Kilio gani Dokta Amdanil?”
“Mama kwani umehamishwa wizara?”
“Mwanangu siku zote ulikuwahujui?”
“Sijui kwani shule kwenyewe hata TV yenyewe hatutizami?”
“Ehee makubwa hayo sasa ni kwanini hamtizami TV?”
“Waalimu wanatubania”
“Mwanangu siku hizi unakiswahili cha kiuni kubaiwa ndio nini?”
“Hawataki”

“Eheee dokta endelea mwaya kwani huyu mtu akianza kuzungumza hapa hamalizi na sasa unaweza kusema amemeza CD ya mziki”
“Mamaaa!”
“Mama nini wakati huo ndio ukweli”

“Kweli hali yake imekuwa nzuri uchangamfu kidogo umemrejea………Muheshimiwa mimi ombi langu naweza kusema nimaombi yangu pamoja na madaktari wengi…..Muheshimiwa hebu naomba kidogo mishahara yetu muifikirie kwa mara nyingine kwa maana kodi kila kukicha inaongezeka na ukitazama mishahara haipandi”
“Hilo ndio nitalipa kipaumbele tukirudi bungeni mwezi ujao na wala usiwe na mashaka na hilo”

   Nikanyanyuka na kujiweka pensi yangu ya michezo vizuri na kuwafanya mama na Dokta wakinitazama
“Unakwenda wapi?”
“Toilet”(Chooni)
“Hizo ngazi za gorofani upande taratibu usije ukaanguka na urudi umalizie chakula chako”
“Mama nimeshashiba”
“Nimekuambia urudi uje kumalizia chakula chako”
“Sawa mama Eddy”

   Nikaondoka na kuwaacha mama na daktari wakiendelea kuzungumza mambo yao ya kikazi,nikaingia katika chumba changu kilichopo gorofani na moja kwa moja nikaingia katika choo kilichopo ndani ya chumba changu na kujisaidia haja ndogo.Nikakumbuka kwenye kabati la chumbani kwangu kuna simu yangu ambayo niliiacha kipindi ninakwenda shule nikatoka chooni na kufungua kabati langu na kuaanza kuchangua vitu na kuanza kuitafuta kwani katika sehemu niliyoiweka haikuwepo.Nikatafuta zaidi ya dakika tano sikuuiona ikanibidi nitoke chumbani kwenda kumuuliza mama ila kabla sijashuka kwenye ngazi nikasikia swali la daktari na kunifanya nisimame na kuyasikiliza mazungumzo yao pasipo wao kuniona

“Yule dada wa kazi amekwenda wapi?”
“Yule niliamua kumrudisha kwao kwani amenivurugia familia yangu”
“Kivipi?”

“Dokta yaani ni makubwa sana yaani watu wa nje wanapo ona mtu uanishi katika jumba kubwa magari mazuri wanahisi haya ndio maisha mazuri ila kusema kweli dokta yaani ingekuwa sio haya majukumu ya kiserikali ningeondoka nchini na mwanangu kwenda kuishi mbali na Tanzania”

“Muheshimiwa kwa nini umezungumza hivyo wakati Mungu amekujalia kila kitu katika maisha”
“Ndio amenijalia kila kitu katika maisha ila sio amani katika ndoa yangu…..Daktari ninakuambia hivi kutokana wewe ni sawa na kaka yangu na mamo mengi umekuwa ukinishauri ila hata hili nahitaji unishaur kutoka kwako”

“Kwani kuna kitu kibaya kilicho tokea kati yako na mzee?”
“Ndio tena ni kikubwa sana ambacho kinaninyima usingizi kila nikikifikiria……Si nilikuwa masomoni kwa kipindi kirefu kidogo”
“Ndio”
“Basi huku nyuma nilimuacha huyu kijana wangu yule binti wa kazi na mzee”
“Ndio”

“Wakati nikirudi nchini sikutaka mume wangu atambue kitu chochote…..Nilifika hapa Tanzania mida ya saa saba usiku na pia sikutumia gari yangu kohofia dereva wangu anaweza kumuambia mume wangu kuwa ninarudi”
“Sasa ni kwanini hukutaka mzee ajue?”

“Nisikudanganye dokta kwa jinsi nilivyokuwa nikimpenda baba Eddy basi kama kuna kitu chochote kibaya kitakuwa kanamtokea basi mimi moyo wangu hujikuta na wasi wasi sana kiasi kwamba hata kama anakuwa na safari ya muhimu huwa nina mzuia asiende na akibaki ujue kuna tukio baya litatoke sehemu aliyokuwa anahitaji kwenda…….
Basi miezi mine nyuma hali hiyo ikawa inanisumbua sana kiasi kwamba nikaanza kuwa na mashaka kuwa kuna kitu mume wangu atakuwa anakifanya ambacho ni kinyume na makubaliano ya ndoa yetu……..Basi niliingia hapa usiku kama saa nane kasoro hivi kwa kutumia taxi ya kukodi hadi askari wa getini akanishangaa.Sikushtuka kutokana ni kawaida ya nyumba yangu kuwa na ukimya,nilipitiliza moja kwa moja hadi ndani kwangu…..Dokta huwezi amini yaani nilimkuta Baba Eddy akiwa amelala na yule binti”

“Weeeee…..!!?”
“Ndio dokta na mbaya zaidi juu ya kitanda changu nilicho kinunua kwa pesa yangu”
“Yule binti kumbe anatabia chafu kiasi hicho?”

“Dokta weee acha tuu hapo ndipo nikaamini ule usemi wa mfadhili mbuzi kuliko binadamu kwani anamaudhi.Na ninamshukuru Mungu ile siku presha yangu haikupanda”

“Sasa hapo ndio naanza kupata pichaa”
“Picha gani dokta?”
“Mwezi uliopita yule binti alikuja pale hospitalini kwangu”
“Alifwata nini?”
“Ndio nakuja huko uliponiuliza……Alikuja kwa lengo nimtoe mimba?”
“Mimba…..!!?”

   Mama aliuliza kwa sauti ya juu hadi na mimi nikshtuka niliposimama na kunifanya niwachungulie na kumuona mama akiwa amekaa katika kochi lake nililomuacha huku akimtazama dokta kwa umakini

“Ndio alikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja na nusu”
“Sasa hiyo mimba atakuwa ameipataje pataje wakati mume wangu hana uwezo wa kumzalisha mwanamke?”
“Ehhee mbona uwezo huo anao tuu wakumzalisha mwanamke?”

“Dokta mbona unanichanganya na wewe…..Mimi ninazungumza hivyo kutokana mimi nilihusika katika oparesheni ya mume wangu kipindi amepeata ajali na tulimchoma sindano ambayo asingeweza kumzalisha mwaanamke wa aina yoyote,Kumbuka hata mimi nilikuwa ni daktari?”

“Ndio nalitambua hilo kuwa wewe ni dokta ila hichi ninacho kuambia mimi nina uhakika kutokana miezi mitano hivi ya nyuma kuna madaktari wa wachina walikuja pale hospitalini kwetu wakijishuhulisha na maswala ya wanaume walio na tatizo kama hilo unalo lisema.Mzee alikuja kunitembelea ila hakujua kama kuna huduma hiyo ya kupima wanaume inatolewa pale hospitalini.Katika mazungumzo yatu nikamtania kiutani utani akapime na yeye ili ajue kama ana uwezo au hana…….Alipopima kama ulivyosema wewe kuwa hana uwezo wa kumzalisha mwanamke ndivyo majibu yake yalivyokuwa.Kutokana wezetu wachina wapo mbele kwa taaluma hiyo basi wakamfanyia upasuaji mdogo akarekebishwa katika mirija yake akapewa dawa na akapona kabisa”

“Ndio akaamua majaribio yake ya kama amepona ua hajapona ndio akaamua ayachukulie kwa mtoto wa watu?”

“Kwa hilo hata mimi sijui….Basi yule binti alinibembeleza sana niweze kuitoa mimba aliyokuwa nayo kwa akili za haraka haraka nikajua mimba amepewa na vijana wako wa kazi…..Ila nikaja kupata mashaka zaidi pale binti siku ya pili alipo nijia na milioni tano ili nimfanikishe kumtoa mimba”
"Na wewe ukamtoa?”

“Sikudhubutu ukiachilia mbali maadili yangu ya kazi hayaruhusu daktari kumtoa mwanamke mimba pia hata imani ya dini yangu hairuhusu jambo hilo”

“Ehee  ikawaje?”
“Nilimfukuza akaondoka akiwa analia.Nikachukua jukumu la kuwasiliana na mzee nikakutana naye ila mimi kama dokta kwajinsi mzee alivyokuwa akinijibu nikaanza kupata mashaka ila nikaja kuachana nalo kutokana nilijua mzee atalifanyia kazi”

“Kwanini na wewe usinipigie simu ukanieleza hilo swala?”
“Muheshimiwa niliogopa kutokana wewe upo masomoni na isitoshe ulikuwa unakaribia kipindi cha mitihani”

 Mwili wangu ukashikwa na ganzi iliyonifanya nitulie sehemu nilipo huku machozi yakinilenga lenga sikuamini kama baba anaweza kutembea na msichana wa kazi na mbaya zaidi msichana wa kazi maisha ya kwao sio mzuri kabisa na ndugu zake wanasomeshwa na kwa pesa ya mama

“Muheshimiwa futa machozi usilie”
“Dokta inauma mwanaume niliye mwamini na kumuinua kimaisha leo hii ananifanyia kitu kama hichi”
“Muheshimiwa hizo ni changamoto za maisha”

“Hapana dokta huo ni upumbavu tena upumbavu ulio pindukia yaani pia nashukuru sijazaa na huyu mwanaume”

  Nikastuka kusikia mama akizungumza kitu kama hicho huku akiwa analia kwa uchungu na kunifanya na mimi kujawa na hisia za huzuni na taratibu machozi yakaanza kunitoka,Kutokana na hali yangu ya kuumwa sio nzuri sana ikanilazimu kukaa katika ngazi ya juu huku nikiwa nimeuegemea ukuta na kuendelea kuwasikiliza mama na daktari

“Muheshimiwa unataka kuniambia huyu kijana si mtoto wa mzee?”
 Kabla daktari hajajibiwa swali lake na mama simu yake ikaita,akaitoa na kupokea na kumfanya mama akae kimya
“Ajali ya basi gani?’
“Majeruhi 34?’
“Ninakuja ninakuja sasa hivi”
“Dokta ni ajali ya basi gani?”

“Basi la Msulwa Express limegongana na roli la mbao maeneo ya maili moja”
“Ehee wamekufa watu wangapi?”
“Watano ila majeruhi nao wana hali mbaya kiasi kwamba hali ya vifo itaongezeka wakati wowote na majeruhi wapo hospitalini kwetu”

“Duu poleni.Haya mwaya Dokta nikuache ukatumikie majukumu yako”
“Sawa muheshimiwa hali ya mgojwa wangu itakavyo endelea utanijulisha”
“Sawa nahisi atakuwa amelala”
“Haya kama atakuwa bado yupo macho utamuambia mimi nimesha ondoka”
“Hakuna shaka juu ya hilo”
 
Nikasikia mlango wa kuingila sebuleni ukifunguliwa na kufungwa nikajua moja kwa moja dokta atakuwa ameondoka.Mama akanza kupandisha ngazi akaanza kupata wasi wasi baada ya kuniona nimekaa katika ngazi huku machozi yakinimwagika

“Eheee mgonjwa bado hujalala na unalia nini mwanangu?”
“Mom who is my father?”(Mama baba yabgu ni nani?)”
 Mama akabaki kimya huku akinitazama akionekana kuto kulitarajia swali kama hilo nililo muuliza.Akapanda ngazi na kukaa ngazi niliyo kaa mimi

“Eddy my son i will tell you tomorrow now your supporse to relax”(Eddy mwanangu nitakuambia kesho sasa hivi unatakiwa upumzike)

“Momy i can’t relax because i don’t know who is my real blood father”(Mama siwezi kupumzika kwasababu simjui baba yangu wa damu)

 Nilizungumza kwa hasira huku machozi yakinimwagika na kumfanya mama aniegemeze kichwa changu kwenye bega huku akinibembeleza

“Eddy my son do you love me?”(Eddy mwanangu unanipenda mimi?)
“I love you mother but i need know the truth”(Nakupenda mama ila nahitaji kujua ukweli)

“Ok my son am happy to hear that you love me.I need you to listen me very carefull”(Sawa mwanangu ninafuraha kusikia kuwa una nipenda.Nahitaji unisikilize vizuri kwa umakini)
“Ok mom am listen up”(Sawa mama nina kusikiliza)

“Now is night give me a chance to go and prepair my some of the office work and tomorrow after i came back i will give you good explaination and i will tell you who is your real father”(Mwanagu sasa hivi ni usiku,nipe nafasi ya kwenda kuandaa baadhi ya kazi za ofisini kwangu na kesho nitakapo rudi nitakupa maelezo mazuri na nitakuambia nani ni baba yako)

  Mama alizungumza huku akinifuta machozi kwa kutumia kiganja chake na kunifanya nizidi kulia kwa uchungu
“Mama sitaki tena nimesema sitaki nahitaji kumjua baba yangu ni nani kwa jinsi ninavyo ona  hauto shindwa kusema mimi sio mwanao wa kumzaa”

  Nilizidi kuzungumza kwa hasira iliyo changanyikana na uchumgu na nikaanza kujihisi upweke ambao nikaanza kuufananisha na mtoto aliye kosa wazazi wote awili
“Eddy what are you say?”(Eddy unasemaje?)
“Yeah you can tell me that your not my mother”(Ndio unaweza ukanimbia kuwa wewe sio mama yangu)

 Nlizungumza kwa hasira nikastukia kofi likitua shavuni mwangu kutoka kwa mama na kumfanya anyanyuke kwa hasira na kuelekea chumbani kwake na akaubamiza kwa mguvu mlango wa chumbani kwake.Nikamfwata na kumkuta akiwa amelala gubi gubi kitandani kwake huku akiwa analia taratibu nikakaa kitandani na kumgusa mgongoni

“Momy am sory i d…”(Mama samahani si……)
“Eddy leave me alone now”(Eddy ondoka na uniache peke yangu sasa hivi)
“Mom am sory i din’t mean to say that words”(Mama samahani sikuwa na maana ya kusema maneno yale)

“Eddy do you whant me to die?”(Eddy unahitaji mimi nife?)
“No mamy”(Hapana mama)
“Your father comfused me and you too so if you need me to die kill me now”(Baba yako ananichanganya na wewe pia.Sasa kama unataka mimi nife niue sasa hivi)
 
Mama alizungumza kwa hasira huku akiuchukua mkono wangu mmoja na kuuweka kwenye koo lake ili nimkabe afe nikajikuta nikiogopa na mwili mzima ukianza kutetemeka kwani sikuwahi kumuona mama katika hali ya hasira kiasi kwamba anataka mimi nimuue
 
ITAENDELA...
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11 & 12 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 11 & 12 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 06:42:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.