Waziri Nape amemtetua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TaSUBa
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mosses Nnauye amemteua
Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Uteuzi huu umefanywa chini ya Kifungu Na. 9
(1) cha Sheria ya Wakala wa Serikali (Executive Agencies Act)
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 ambacho kinampa Waziri mamlaka ya
kufanya uteuzi huo. Uteuzi huu utaanza tarehe 01/07/2016.
Dkt.
Makoye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Juma Bakari aliyestaafu
kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma. Dkt. Makoye mwenye Shahada ya
Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Ghana na Shahada ya Umahiri – Sanaa
(M. A in Theatre Arts) toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kabla ya uteuzi huu Dkt. Makoye alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Idara ya Sanaa na Maonesho.
Imetolewa na,
Genofeva Matemu,
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.
28 Juni,2016
Waziri Nape amemtetua Dkt. Herbert F. Makoye kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TaSUBa
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:17:00
Rating:
No comments: