Hifadhi Kubwa Zaidi ya Gesi ya HELIUM Yagunduliwa Tanzania



Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania, ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.


Wakitoa taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wamesema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.

Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka 2035. Mnamo mwaka 2010 Mwanafisikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.

Ukosefu huo ulikuwa umesababisha na wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya Oxygen.

Chris Ballentine kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema……..>>>”Gesi tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja nukta mbili za mashine za MRI” 
Via>BBC
Hifadhi Kubwa Zaidi ya Gesi ya HELIUM Yagunduliwa Tanzania Hifadhi Kubwa Zaidi ya Gesi ya HELIUM Yagunduliwa Tanzania Reviewed by WANGOFIRA on 20:13:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.