Mwanajeshi Mlevi Aliyevuta Bangi Aua Watu 8 Kwenye Kambi ya Jeshi Baada ya Kugombana na Mke Wake



Jumla ya watu wanane wameuawa baada ya kupigwa risasi ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye mjini Kampala nchini Uganda.

Msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, anasema kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe.

Anaripotiwa kuwa mlevi na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi kiholela akimtafuta mkewe ambaye alifanikiwa kutoroka.

Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi waliuawa wakati wa kisa hicho.

Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu.

Mwanajeshi huyo naye aliuawa kwa kupigwa risasi.
Via>>BBC
Mwanajeshi Mlevi Aliyevuta Bangi Aua Watu 8 Kwenye Kambi ya Jeshi Baada ya Kugombana na Mke Wake Mwanajeshi Mlevi Aliyevuta Bangi Aua Watu 8 Kwenye Kambi ya Jeshi Baada ya Kugombana na Mke Wake Reviewed by WANGOFIRA on 20:20:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.