Afisa Usafirishaji wa Kampuni ya Athwal Transport & Timber LTD Afikishwa Kizimbani Kwa Kutoa Rushwa Ili Utingo Akiri Kosa la Wizi


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha mahakamani Ofisa Usafirishaji wa Kampuni ya Athwal Transport & Timber LTD , Godfrey Tarimo, kwa mashitaka ya kutoa rushwa kwa mtumishi wa kampuni hiyo akiri kosa la wizi.

Tarimo alipandishwa kizimbani jana, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Tabora Jackton Rushwela .

Wakili wa Takukuru, Simon Mashingia alidai Tarimo alitenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu katika Gereza la Uyui mjini hapa.

Wakili Mashingia alidai kuwa siku hiyo mshtakiwa akiwa ni Ofisa Usafirishaji wa ATT alitoa rushwa ya Sh 400,000 kwa Said Hamis ambaye alikuwa utingo wa gari katika kampuni ya ATT.

Akifafanua katika mashitaka hayo, wakili Mashingia alidai kuwa Tarimo akiwa kama wakala wa kampuni alitoa fedha hizo kama kishawishi kitakacho mfanya Hamisi akiri kosa la wizi katika kesi ya jinai namba 13/2015 iliyokuwa inamkabili.

Ilidaiwa kwamba, Hamisi baada ya kupokea fedha hizo alipofika mahakamani alikiri kosa ambapo Hakimu Rushwela alimpa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela. Mwendesha mashitaka alidai, uchunguzi umebaini kuwa Tarimo alipoteza tumbaku iliyokuwa inasafirishwa na magari ya kampuni ya ATT.

Alidai kwamba, ili kampuni hiyo isionekane ina sura mbaya katika biashara, walimbambikia kesi utingo huyo na kumshawishi akubali kuwa ndiye aliiba ili baadaye waweze kumsaidia atoke lakini alihukumiwa kifungo.
Afisa Usafirishaji wa Kampuni ya Athwal Transport & Timber LTD Afikishwa Kizimbani Kwa Kutoa Rushwa Ili Utingo Akiri Kosa la Wizi Afisa Usafirishaji wa Kampuni ya Athwal Transport & Timber LTD Afikishwa Kizimbani Kwa Kutoa Rushwa Ili Utingo Akiri Kosa la Wizi Reviewed by WANGOFIRA on 20:41:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.