SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOFANA KATIKA VIWANJA VYA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK

DSC_0447
JAMII imetakiwa kubadilika kwa kuacha kufanya ukatili wa watoto ili kuweza kuwa na watoto kwa kujitambua. Hayo ameyasema leo Mkugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali C-SEMA, Kiiya Joel, wakati wa maadhimisho ya siku mtoto wa Afrika iliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete, amesema kesi nyingi za watoto kutelekezwa ambazo zimekuwa zikifikia kituomn hicho kupitia huduma ya simu mkononi.

 Kiiya amesema watoto wanatelekezwa na kufanya watoto kuishi mitaani na kuhitaji msaada wa kujikimu hali ambayo inafanya watoto kukosa haki ikiwemo kukosa elimu. 

Amesema kuwa katika utoaji wa huduma ya simu C-SEMA imejipanga kuboresha huduma visiwani Zanzibar ili kuhakikisha vitendo viovu vya watoto vinapatiwa taarifa. “Tumepata fedha ambazo C sema itaboresha huduma kupiga ya simu kwa ajili ya kupata matukio ambayo yanakandamiza watoto visiwani Zanzibar “, amesema Kiiya.

Na amewataka watanzania kutoa ushirikiano kwa kupiga simu ya bure 116 na kutoa taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili yaweze kutatuliwa mara moja.  Watoto katika picha ya Pamoja .

Amesema kuwa kituo cha huduma ya simu kwa mtoto kimekuwa hakipokei simu nyingi kutokana na kwamba huduma hiyo haijafahamika maeneo mengi ambapo kwa mwezi hupokea simu 30 kiwango ambacho ni kidogo kulingana na ukubwa wa tatizo.

 “Naomba watanzania wote popote pale walipo kupiga simu ya bure 116 pale wanaposikia taarifa za kuwepo kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto ili yaweze kufanyiwa kazi,” amesema 

Amesema kuwa toka kituo hicho kianze Juni 16, mwaka 2013 wamekuwa wakipokea simu za matukio ya watoto kupewa ujauzito, matunzo ya watoto baada ya kutekelezwa, ulawiti na ubakaji. 

Read More
SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOFANA KATIKA VIWANJA VYA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOFANA KATIKA VIWANJA VYA JAKAYA KIKWETE YOUTH PARK Reviewed by WANGOFIRA on 06:18:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.