WAZIRI NCHEMBA AAGIZA GEREZA LA IRINGA MJINI KUHAMIA NJE YA MJI

waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Bw  Mwigulu Nchemba akisalimiana na  waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Bw  Wiliam Lukuvi (kuli)  leo  baada ya  kukutana  ofisi ya mkuu wa mkoa  wa Iringa
Waziri Lukuvi katikati  akimtambulisha  mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela kwa waziri Nchemba leo
Waziri Nchemba  akisikiliza jambo  kutoka kwa waziri Lukuvi
Kamanda  wa  polisi wa mkoa wa Iringa Bw  Peter Kakamba  akisalimiana na waziri wa mambo ya  ndani ya nchi Bw Nchemba
Mbunge  Msigwa akisalimiana na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Bw Mwigulu Nchemba
Mbunge  wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa pili kushoto  wakisalimiana  kwa  furaha na  mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abeid Kiponza  huku waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Bw Mwigulu Nchemba na  mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  (kushoto)  wakiangua  kicheko
Waziri Nchemba  akitembelea  eneo la Hospitali ya  Rufaa ya mkoa wa Iringa
Mganga  mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Salmu Robart akimwonyesha  waziri Nchemba ufinyu wa eneo la  Hospitali  hiyo ya rufaa ya mkoa wa Iringa

WAZIRI  wa mambo ya ndani ya  nchi Bw  Mwigulu Nchemba  ameagiza  uongozi  wa Magereza  ya  mkoa  wa Iringa  kuanza mchakato wa kuhamisha magereza  ya Manispaa ya  Iringa  ili  eneo  hilo  kutumika  kupanua  Hospitali ya  rufaa ya  mkoa  wa Iringa.

Bw  Nchemba  ametoa  agizo hilo  leo  baada  ya  kutembelea  eneo   hilo ambalo  limekuwa  likiombwa kwa  muda  mrefu na  viongozi  wa serikali ya  mkoa wa Iringa  ili  litumike  kwa ajili ya matumizi ya Hospitali  hiyo ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa .

Akizungumza baada ya   kutembelea  eneo hilo lililopo  eneo la Hospitali  ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  alisema  kuwa amekubaliana na maombi ya  viongozi wa mkoa wa Iringa ya  kuomba  gereza  hilo  kuhamishiwa katika  eneo la Mlolo nje  kidogo  na Manispaa ya  Iringa  huku  eneo hilo la Magereza litumike  kupanua  majengo ya  Hospitali  hiyo ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa.

“ Kwa  kawaida  kati ya Hospitali na  magereza  kinachotakiwa  kuwepo  mjini ni  Hospitali na  sio magereza  hivyo   hivyo kati ya  mgonjwa na mfungwa ama mahabusu anayeweza  kufanya kazi ya  kufyatua  tofari  za  ujenzi ni mahabusu ama mfungwa na  sio mgonjwa ……hivyo naagiza mtaalam wa ujenzi  wa magereza  kuanza  kuandaa vifaa vya  kufyatualia  tofari  na  kwa  kufuata taratibu za magereza waorodheshwe  wale ambao  watakuwa  tayari  kujitolea  kufanya kazi ya ujenzi  ili kazi  hiyo  ianze” 

Hata  hivyo  waziri  huyo alisema kuwa kuanzia  leo jioni anataka  kupata orodha  ya  wafungwa waliopo gerezani hapo ambao  wanauwezo  wa kufanya kazi.

Pia  alisema  suala  la  kuhamishwa kwa gereza  hilo  litafanyika kwa awamu na  kuwa wakati  gereza  linajengwa na baadhi ya  nyumba  za watumishi bado askari  wataendelea  kuishi katika eneo hilo huku majengo  yao likiwemo  jengo la Ghorofa  utawekwa utaratibu wa  kujengewa jingine  ili  hilo linalotumiwa na magereza  litumike kwa ajili ya  madaktari .
WAZIRI NCHEMBA AAGIZA GEREZA LA IRINGA MJINI KUHAMIA NJE YA MJI WAZIRI NCHEMBA AAGIZA GEREZA LA IRINGA MJINI KUHAMIA NJE YA MJI Reviewed by WANGOFIRA on 20:24:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.