Tundu Lissu Asomewa Mashitaka Matatu Mahakamani


Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameshtakiwa kwa makosa matatu la kwanza kutoaa maneno ya uchochezi kwamba Agosti 2 katika Mahakama ya Kisutu kwa nia ya kujenga chuki kwa wananchi dhidi ya Rais na Serikali alitoa maneno ya uchochezi.

Shtaka la pili pia uchochezi kwamba Agosti 2 katika mahakama hiyohiyo kwa nia ya kudharau mhimili wa utoaji haki, alisema kuwa hawezi kufungwa kwa mashtaka na kesi ya upuuzi na shtaka la tatu ni la kudharau mahakama akidaiwa kuwa tarehe hiyohiyo mahakamani hapo, alitoa maneno ya uchochezi kuwa hawezi kufungwa kwa kesi na mashtaka ambayo ni upuuzi na ya kimagufulimagufuli
Tundu Lissu Asomewa Mashitaka Matatu Mahakamani Tundu Lissu Asomewa Mashitaka Matatu Mahakamani Reviewed by WANGOFIRA on 20:15:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.