DAWASCO YAINGIA MITINI ZIARA YA NAIBU WAZIRI MPINA

Na, 
EVELYN MKOKOI

Katika hali isiyo ya kawaida shirika la maji safi na maji taka DAWASCO jijini Dar es Salaam na Pwani DAWASCO, limeingia mitini katika Ziara ya Naibu Waziri wa Mazingira na Muungano Mhe. Luhaga Mpina ya kutembelea miondombinu  ya maji taka na maji safi Jijini dar Es Salaam na Pwani jana.

Licha ya Shirika Hilo kupewa Taarifa ya Ziara ya Naibu waziri Mpina mwezi mmoja kabla limekaidi kwa kutoitikia wito huo hata kwa kumuwasilisha mtumishi mmoja kuwakilisha shirika hilo.

Akiongea kwa ukali baada ya kutembelea Bomba la kusafirisha maji taka kwenda baharini la Ocean road, Naibu Waziri Mpina amesema ubovu wa bomba la ocean road unatokana na kutokukarabatiwa kwa muda mrefu, unaonyesha dhahiri kuwa DAWASCO wana Jeuri kwa IKulu, kwa kutokulifanyia ukarabati kwa muda muda mrefu Bomba hilo lililoko karibu na maeneo hayo.

Alipotembelea mabwawa ya maji taka ya mabibo na buguruni, Mhe Mpina Alisema pamoja na kuwa miondombinu hiyo inaelemewa na wingi wa  wakazi wa Dar Es Salaam, Mamlaka husina zina wajibu wa kuyafanyia usafi mabwawa hayo lakini, hazijaonekana jitihada zozote za kufanya hivyo, na miondombinu hiyo inaonekana kutofanyiwa ukarabati kwa muda wa miezi sita.

Naibu Waziri Mpina alisisitiza kuwa ubovu na uchafu wa miundombinu hiyo unapelekea uchafuzi wa mazingira na hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na viumbe hai wengine.
Akiongea kwa Uchungu, Mkazi mmoja wa Mabibo aliyekataa kutaja jina lake alisema kuwa,  ninanukuu“Mabwawa haya ni ya Dawasco na hata tukitaka kuunganisha maji taka kwenye mabomba yao kuelekea kwenye mabwawa wana taka tuwalipe na tunafanya hivyo, wenye viwanda halikadhalika wanawalipa dawasco kwa kupitisha maji taka yao katika miundombinu ya dawasco, lakini najiuliza, kwa nini wanakuwa wagumu kuyafanyia ukarabati au hata kusafisha tuu?. Mwisho wa kunukuu.

Ziara ya Naibu waziri Mpina ya kukagua miundiombinu ya DAWASCO leo Jijini Dar Es Saalam ilihushisha maafisa kutoka DAWASA na Baraza la taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC na kuwaagiza NEMC, wapitie miradi yote inayosimamiwa na DAWASCO na kuon akama wanatenda haki katika kutoa huduma kwa wananchi.


DAWASCO YAINGIA MITINI ZIARA YA NAIBU WAZIRI MPINA  DAWASCO YAINGIA MITINI ZIARA YA NAIBU WAZIRI MPINA Reviewed by Unknown on 20:10:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.