Babu Atiwa mbaroni kwa kumbaka mjukuu wake


JESHI la Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka 12.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba aliyebakwa ni mwanafunzi wa darasa la tano na ana umri wa miaka 12.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, mtuhumiwa huyo ambaye ni mlinzi, Philipo Stephano , alikamatwa Agosti 2 mwaka huu, saa tisa mchana katika maeneo ya Soweto, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi mkoani hapa.

“Yule mtoto ambaye jina lake tunalihifadhi, alibakwa na babu yake mzaa mama yake, mkazi wa Soweto.

“Kabla ya mtuhumiwa kufanya tendo hilo, alimwambia mjukuu wake huyo amwelekeze na alipokubali, alimpeleka katika eneo analolinda na kumfanyia unyama huo.

“Baada ya uchunguzi wa daktari, ilithibitika mwanafunzi huyo alibakwa na kusababishiwa maumivu makali katika sehemu zake za siri.

“Kwa hiyo, mtuhumiwa tumemkamata na tunaendelea na upelelezi kabla hatujampeleka katika vyombo vya sheria,” alisema Kamanda Mutafungwa.
Babu Atiwa mbaroni kwa kumbaka mjukuu wake Babu Atiwa mbaroni kwa kumbaka mjukuu wake Reviewed by WANGOFIRA on 20:11:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.