SERIKALI ZETU ZINATAMBUA MCHANGO WA WANADIASPORA
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zinatambua mchango mkubwa wa Wanadiaspora na ndio maana hutayarisha
makongamano ambayo hutoa fursa ya kujadili masuala mbali mbali ya
kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi wa Tanzania na ustawi wa
wananchi wake.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid
Salum aliyasema hayo leo huko Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipofanya
mazungumzo na waandishi wa Habari mbali mbali kutoka Redio za FM
zinazofanya kazi zake hapa Zanzibar kuhusu Kongamano la Diapora la
Tanzania linalotarajiwa kufanyika hapa Zanzibar mwaka huu.
Katika
maelezo yake Katibu Mkuu huyo aliyekuwa pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Silima Kombo Haji,
alisema kuwa kwa miaka miwili iliyopita makongamano hayo yamefanyika
Dar-es-Salam na kusisitiza kuwa mikutano iliyokwisha fanyika imeweza
kuleta mafanikio makubwa.
Alisema
kuwa Mkutano wa mwaka huu unatarajiwa kufanyika hapa Zanzibar kwa muda
wa siku mbili kati ya tarehe 24 na 25 linatarajiwa kufunguliwa na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kufungwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli huko katika
ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Katibu
Mkuu huyo alisema kuwa mada mbali mbali zinatarajiwa kutolewa katika
Kongamano hilo ambalo kauli mbiu yake ya kila mwaka ni “Mtu kwao ndio
Ngao’ ambapo pia, ujumbe mkubwa kwa mwaka huu ni “Mtizamo mpya wa
Kuimarisha Utalii wa Tanzania na uekezaji”
Katika
melezo yake Katibu Salum alisema kuwa tayari matayarisho ya kongamano
huo yanaendelea vizuri na kueleza kuwa Wanadiaspora wamekuwa na mwamko
mkubwa katika ushiriki ambapo kila mwaka idadi ya ushiriki wao imekuwa
ikiongezeka huku akieleza kuwa vyombo vya habari zikiwemo Redio za FM,
vina nafasi kubwa katika kuwaeleza wananchi juu ya mkutano huo.
Aidha,
alisema kuwa miongoni mwa mafanikio yaliopatikana ni pamoja na
Wanadiaspora wengi wa hapa nchini wameweza kutoa michango yao mbali
mbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha mirado mbali mbali ya maendeleo
ikiwemo ya afya, elimu na mengineyo.
Katibu
Mkuu huyo alitumia fursa hiyo kueleza juhudi za viongozi hapa nchin i
katika kuhakikisha suala hilo linaimarika huku akitolea mfano juhudi za
makusudi zinazochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha ushirikiano kati ya
Wanadiaspora na Serikali zote mbili unaimarika.
Nae
Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Silima Kombo Haji aliwaeleza waandishi hao wa habari faida
zinazopatikana kutokana na kuunganishwa kwa Wanadiaspora hapa nchini
pamoja na changamoto zilizopo.
Balozi
Silima alizitaja baadhi ya nchi zilizopo ndani na nje ya Afrika ambazo
zimenufaika na zinazaendelea kunufaika kutokana na Wanadiaspora wa nchi
zao zikiwemo Kenya, Ethiopia, Ghanam Idia, Pakistan, Ufilipino,
Bangladesh na nyenginezo.
Sambamba
na hayo, Balozi Silima alisema kuwa serikali zote mbili zimeweka
mikakati maalum ya kuhakikisha Wanadiaspora wanapewa kipaumbele sambamba
na kushirikishwa katika masuala mbali mbali ya maendeleo kwa nchi yao.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar (P.T)
SERIKALI ZETU ZINATAMBUA MCHANGO WA WANADIASPORA
Reviewed by WANGOFIRA
on
21:09:00
Rating:
No comments: