RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 15 & 16 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA...
....Nikashuka ndani ya gari nikiwa ninazunguka nyuma kwenye gari ili niiingie kwenye siti ya dereva nikapata mshtuko baada ya kumuona msichana akianza kujivuta taratibu kutoka ndani ya gari huku akilia kwa maumivu makali ikanibidi nianze kupiga hatua za kwenda kumsaidia ila kadri jinsi nilivyo zidi kwenda moyo ukazidi kunipasuka kwani mtu anaye jitahidi kujitoa ndani ya gari ni Manka....


ENDELEA....
.....Nikaongeza hatua za haraka kwenda kumsaidia Manka,nikamkuta anatokwa na damu nyingi katika paji la uso wake huku mguu wake mmoja ukiwa umebanwa katika siti,Nikajitahidi kuitoa siti iliyombana Manka hadi nikafanikiwa kisha nikamuweka kando kwenye barabara na kwenda kutazama majeruhi wengine akiwemo Mwalimu Mayange.Nikachungulia chungulia ndani ya gari na ila sikuona mtu yoyote anayeomba msaada kwani ukimya mkubwa ulitawala ndani ya gari na kutokana na giza jingi nikajua moja kwa moja watu waliomo ndani ya gari watakuwa wamefarika dunia ua kupoteza fahamu.

  Nikarudi barabarani kumtazama Manka na kukuta hali yake inazidi kuwa mbaya nikamnyanyua na kwenda naye ndani ya gari na kumkuta dereva akiwa amekaa kwenye siti niliyokuwa nimekaa mimi huku akiwa kama amepigwa na bumbuazi kiasi kwamba hawezi kufanya kitu chochote huku jasho jingi likimtoka japo ndani ya gari letu aina ya VX G8 lina  Air condition(A.C) ya kutosha.Nikamuingiza Manka ndani ya gari na kumuweka siti ya nyuma kisha na mimi nikaingia kwenye upande wa dereva na kuwasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi,nikafika kwenye moja ya zahanati na kumkuta daktari mmoja na nesi ambao wapo zamu ya usiku.

Nikamtoa Manka ndani ya gari na kumuweka kwenye kitanda cha matairi kilichotolewa na nesi kisha wakamuingiza ndani ya chumba na kuniomba nisubiri nje na kunihitaji nikatafute PF3 ya polisi ili hata kama kuna hali yoyote itajitokeza juu ya Manka wao wasihusike kwa chochote.Nikarudi kwenye gari na kumkuta dereva nje ya gari akiwa amejiegemeza kwa unyonge huku akionekana kuwa na wasi wasi mwingi.

“Oya kuna kituo cha polisi hapa karibu”
Nilimuuliza dereva na kumuacha akiwa ananitazama kama hajalisikia swali langu nililo muuliza
“Oya broo mbona kama umesizi ni wapi kwenye kituo cha polisi ambacho ninaweza kupata huduma yao?”
“Hapo mbele”
“Wapi?”
“Labda Mombo kule nyuma tulipotoka kwani bado tupo Mombo”
“Powa ingia kwenye gari”

 Nikawasha gari na kuanza safari ya kurudi kule tulipotoka na safari hii gari nillizidi kuliendesha kwa kasi ili kuwahi kupata alichoniagiza daktari.Nikajikuta nikifunga breki za gari gafla na kusimama hii ni baada ya trafki mmoja kunisimamisha katika sehemu waliyo pata ajali Manka na ndugu zake na kukuta kuna askari wengine wakiendelea na vipimo vya ajali imetokea tokea vipi huku kukiwa na watu watatu wakiwa wamelazwa kando ya barabara na huku wakiwa wamefunikwa na mashuka maalumu ya polisi na baadhi ya wananchi wakiwa wanashangaa shangaa ajali.“Dreva washa taa ya ndani au ushuke ndani ya gari”.

Nikawasha taa ya gari na nikamuona trafki akishtuka nikajichunguza na kugundua kuwa chati langu la shule kidogo lina damu.Trafki aliye nisimamisha akaniomba tena nishuke ndani ya gari  huku bunduki yake akiishika vizuri na sikuwa mbishi nikashuka huku funguo nikiingiza mfukoni.“Ninaomba leseni yako na kadi ya gari”.

Nikaanza kujipapasa kama ninatifafuta leseni yangu kwenye mifuko yangu japo najua kuwa sina leseni ya aina yoyote kwenye mfuko wangu zaidi ya wallet yangu yenye kitambulisho cha shule na pesa za matumizi.

“Afande nahisi nimeishahau leseni yangu kwenye gari”
“Mbona shati lako limejaa mijidamu.Lete funguo za gari”
Nikamkabidhi trafki funguo za gari na kwaishara akaniomba niende kumchukulia leseni yangu na kumuacha akimnong’oneza mwenzake.Nikafungua mlango wa gari na kumkuta dereva akiwa na wasiwasi mwingi
“Oya kaka hivi una leseni yoyote hapo ulipo?”
“Ninayo ya kwangu”
“Siwezi kutumia ya kwako?”
“Huwezi kwani ina picha yangu”.

 Nikaufunga mlango na kumfwata trafki aliyenisimamisha na kila nilipozidi kumfwata huku nikimuita akajifanya kama hanisikii na kuzidi kwenda mbele kuwafwata wezake walipo huku mwenzake aliyekuwa akizungumza naye akielekea kwenye gari letu huku akimulika mulika ndani ya gari kwa kutumia tochi aliyo nayo.Nikamkimbilia trafki kidogo na kumshika shati.

“Afande si nina kuita”
“Nahitaji leseni yako na kadi ya gari”
“Kiukweli mimi sina leseni ya aina yoyote hapa nilipo nilikuwa ninakuja kituoni kwenu kuchukua PF3 ya majeruhi wa hiyo ajali hapo”
“Ahaaa kumbe nyinyi ndio muliwasababishia ajali hawa watu?”
“Hebu kuwa na akili wewe mimi nimsababishie ajali alafu nije kwenu.Mimi nimewasaidia kama masamaria mwema tu”.

 Nikajikuta nikizungumza kwa hasira huku nikimtazama trafki kwa jicho la hasira.Kabla hajazungumza kuna mwenzake mmoja akamuita akitokea lilipo gari letu huku akimuamrisha dereva wa gari letu kushuka ndani ya gari.
“Oya afande John haya ni mijambazi huku kwenye gari lao kumetapakaa mijidamu siti za nyuma na hakuna mtu”

Askari aliyekuwa kwenye gari letu alizungumza na kuwafanya wezake wapatao sita kuzikoki bunduki zao na kuzielekeza upande nilio kuwepo mimi na dereva
“Wee jamaa yangu vipi hivi ukituona hapa kuna sura ya jambazi.Mimi nimemsaidia huyu mmoja wa majeruhi katika hii ajali na wewe unaniletea habari za kise***”.

Nilizidi kuzungumza kwa hasira na kuwafanya askari kunijia juu huku kila mmoja akizungumza lake kwa hasira huku mmoja wao akitishia kunipiga mateke.
“Jaribu kunipiga hayo mateke yako uone kama hii nchi utaiona tamu kama unavyo iona sasa hivi”
“Afande hebu niachie nimuonyeshe shuguli huyu kijana tandu nitoke depo nijamuwasha mtu mateke siku nyingi”
“Aroo hembu lipige pingu hilo jambazi linajifanya jeuri.Na haya ndio yale yanayoiba magaria Moshi na kwenda kuyauza Dar”.

Dereva wetu akakubali kufungwa pingu na akaanza kupelekwa kwenye gari ya polisi aina ya Toyota.
“Aisee wewe nimekuambia lifunge pingu hilo likijana lisiumize vichwa vyetu”
“Sikilizeni hamuwezi kunifunga pasipo kujua kosa langu ni lipi kwani hamuwezi kukuta damu ndani ya gari na moja kwa moja mukaniambia kuwa mimi ni muhalifua”
“Aisee wewe lipige risasi kama linaleta ujinga”
Nikaitoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama ila simu yake ikaita hadi ikakatika,nikarudia tena kuipiga na akapokea simu huku akionekana alikuwa amelala.

“Vipi wewe mbona muda huu mumesha fika?”
“Hapana mama kuna askari wametukamata eti wanasema kuwa sisi ni majambazi”
“Majambazi tangu lini na mumekamatwa wapi?”
“Maeneo ya Mombo njia ya kuelekea Arusha…..”Gafla askari mmoja akanipokonya simu na kuanza kuzungumza na mama huku akionekana kuw na hasira nyingi.

“Kumbe wewe ndio unaye watuma hawa washenzi wako waje wateke teke magari ya kifaharii na munakazi ya kujikalia na kuitana mama mama pumbavu weee mwanamke mzima umekalia kazi ya kuwatumikisha vijana wadogo ili wakuletee mijigari ya kifahari na hili limoja umelivalisha minguo ya shule ili idanganyie raia barabarani wakati wa usiku Malaya mkubwa wee”

 Askari akakata simu na kuidumbukiza mfukoni mwake na kuzidi kunipandisha hasira kwani katika maisha yangu kitu nisicho kipenda ni kuzalilishwa kwa mama yangu
“Aisee hatukubembelezi wewe”
“Sasa niacheni nitakwenda mimi mwenyewe sitaki mnishike”
“Pumbavu hakuna kuliachia ndio maana jishati lako limejaa damu kwa ujambazi ujambazi wako”
“Mabroo nawaheshimu sana sitaki tuvunjiane heshima”
“Nenda kule”

Askari mmoja alizungumza huku akinipiga makofi mazito ya mgongo akinisukumia kwenye gari lao na kuninyanyua juu na kunisukumia ndani ya gari na kujikuta nikiangukia kifua na maumivu makali yakaanza kutawala katika kifua changu.....
                         *****SORY MADAM*****(16)
       
.......Dereva akanisaidia kuninyanyua na kunikalisha katika sehemu aliyokaa yeye kisha baada ya muda wakaziingiza maiti moja huku ikiwa imefunikwa na askari wawili wakapanda na kukaa nyuma tulipo sisi huku wakiwa na bunduki zao kusha mwengine wawili wakapanda mbele upande wa dereva na safari ikaanza.

“Yaani nyinyi ngojeni tu mtaona ngoja mama aje”
“Funga bakuli lako shenzi kabisa wewe na mama yako wote tutawasweka ndani mnakazi ya kukaa na kuiba iba”
“Sawa sisi si majambazi basi nyinyi ndio mtakuwa majambawazii”.
“Unasemaje dogo”.
“Nasema kwa pua mdomo unatia saini”.

Nilizungumza maneno ya kejeli yaliyoandamana na hasira kumfanya askari kukasirika nusu anizabe kofi la kichwa.
“Mimi nawaambia masaa yenu ya kujidai ni sasa hivi ila ngoja hiyo asubuhi”
“Alafu wewe dogo mbona unaongea ongea kama mtoto wa kike unajua tutakupeleka Soweto ukafanyiziwe”
“Mpeleke baba yako wewe k***  nini?”.

Nilizungumza kwa hasira na kumfanya askari kumkabidhi mwenzake bunduki kisha akanishika shati langu na kunivuta kisha akanipiga kichwa kimoja kaniangusha na kujikuta nimeilalia maiti ambayo sikujua ni ya nani kisha akaninyanyua na kunitandika ngumi mbili za tumbo na kujikuta nikitoa vilio vya maumivu makali.

“Oya bro Sele muache utamuua mtu mwenyewe anaonekana mwili maji huyo”
“Muache nimfundishe adabu analeta maswala ya kiboya,watu tupo kazini hatupo kwenye sherehe”
“Kaka tuliza jazba mpotezee ngoja tufike kituoni”
“Oya Suka hawa moja kwa moja tuwapandishe Lushoto”
“Powa kamanda OVER”
“Eddy mdogo wangu hebu kuwa mstamilivu”.

Dereva alizungumza kwa sauti ya upole huku akinitazama kwa masikitiko kwani nilianza kuchuruzika damu kwenye sehemu aliyo nipiga kichwa askari.
“Powa wewe nionee sasa hivi ila zamu yako itafika”
“John unajua nitamchakaza huyu mwehu kwa risasi alafu nipotelee zangu huko milimani”
“Broo wewe mpotezee”
“Oya suka simamisha gari”.
Askari aliye nipiga alimuamrisha askari mwenzake anaye enedesha gari kulisimamisha naye akafanya kama alivyo ambiwa.Kisha akashuka na kwenda kukaa siti ya mbele na mwenzake mmoja akaja kukaa tulipo sisi.Kutokana ni usiku hakuna magari mengi tukawahi kufika wilaya ya Lushoto mjini na moja kwa moja wakatupeleka kwenye ofisi zao.“Msachi huyo chalii na atoe kila kitu”.

Yule askari aliye nipiga alimuamrisha askari mmoja tuliye mkuta katika kituo chao.Jamaa akaanza kunipapasa na kutoa waleti yangu kisha akaiweka pembeni kisha yule askari niliye mkremisha kwa jina la Sele akaichukua wallet yangu na kuanza kuhesabu pesa nilizo kuwa nazo na kukuta kuna laki mbili na sabini.

“Kweli hi mijamaa ni mijambazi tazama pesa zote hizi”
Alizungumza huku akiwaonyesha wezake waliopo ndani ya kituo hicho ambacho ndio kikubwa katika wilaya nzima ya Lushoto
“Wewe jishaue na hizo pesa zangu najua humo kuna laki mbili na sabini ole wako nikute kumepungua hata kumi”
“Alafu huyu dogo ananitafuta tangu tukiwa kwenye gari hivi unataka nikufanyaje?”
“Usijichekeshe chekeshe kama umepata bwana wa bure acha hizo pesa na ole wako ipungue hata kumi”.

Nilizungumza kwa hasira na kuwafanya baadhi ya askari kumcheka mwenzao kichini chini kwa maneno niliyo muambia ila alivyo wageukia wezake wote wakakaa kimya.Jamaa akampokonya mwenzake kifimbo alichokishika na kutishia kunipiga nikasimama nikimtazama huku mwili wangu ukiwa umejaa kwa hasira
“Hembu waingize chemba nisije nikavunja sheria za Jamuhuri bure”.

 Nikageuka na kumtazama dereva nikamuona mwenzangu akitetemeka mwili mzima huku machozi yakimwagika kiasi kwamba hadi nikaanza kumuonea huruma.
“Oya broo simu yako iko wapi?”
“Nimeiacha kwenye gari niliichomeka kwenye chaji”
“Ahhaaa sasa kwa nini na wewe usishuke nayo”
“Niliisahau ndugu”
“Ahaa na wewe umezidi uzembe”.

Askari aliye kuwa akitukagua akatusukuma akiashiria tutembee kuingia ndani ya chumba chenye mwanga hafifu wa taa ya duara kwa haraka haraka ni kama Walti 40 huku kikiwa na nondo ndefu na pana kwenye mlango wake kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kuuvunja mlango huo.

“Ingieni ndani hizo story zenu mutazizungumzia humo ndani”
“Na wewe acha sifa za kutusukuma sukuma unajua hili shati limenunuliwa shilingi ngapi?”
“Sina haja ya kujua limenunuliwa shilingi ngapi cha msingi wewe ingia huko chemba ukakutane na vigego wezako”
“Sawa ila sio kutusukuma sukuma uachage ufala wewe”
“Powaa mimi fala ila ingia ndani”.

 Sikujua hata maneno machafu nina yatolea wapi kwani nilizungumza maneno yasiyo na maana na kwa mtazamo wa haraka haraka mtu ukinitazama hutotegemea kuwa ninaweza kuzungumza vitu vya ajabu kiasi hicho.Tukaingia ndani ya chumba na kukuta kuna njemba(Jamaa wenye misuli mikubwa) nne zimakaa huku wakiwa hawajavalia mashati na kuvifanya vifua vyao vikubwa kuonekana kirahisi huku sura zao zikiwa mbaya na za kuogopesha kiasi kwamba mtu hata uwe mbabe kiasi gani ni lazima uyasome mazingira ya humo ndani na ndio uendelee na ubabe wako
“Niaje raia?”
 Niliwasalimia kwa ucheshi huku nikijitahidi kuiweka sura yangu katika tabasamu ila salamu yangu haikuitikiwa na mtu hata moja zaidi ya wao kuniangalia kwa macho makali.Dereva akazidi kutetemeka hadi ikafikia hatua suruali yake ikaanza kulowa akiashiria ameshindwa kuizuia hali ya kujikojolea.Mkojo wa dereva ukaanza kusambaa kwenye baraza uku ukienda kwenye mfumo wa kajimstari na kufika katika sehemu aliyokaa jijamaa moja jeusi lenye mwili mkubwa na ndevu nyingi kama za masanii maarufu duniani Rick Rose.

“Oya jibaba huyo mse***kakukojolea”
 Jamaa jengine lilizungumza kwa sauti nzito na ya kuogopesha na kumfanya mwenzake atazame mstari wa mkojo ulio igusa suruali yake iliyo chafuka kisha kamtazama dereva na taratibu jamaa likaanza kunyanyuka na kunifanya nikae kimya huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kiasi kwamba ujeri wote ukakata kama umeme wa Tanesco.
“Oya unyonye huo mkojo wako”.

Jamaa lilizungumza huku likimuinamisha dereva wetu kwa nguvu zake zote na kumfanya aanguke kifudi dudi na mimi nikajibanza kwenye kona ya ukuta nikiaangalia nini kitakacho fwata kwa dereva.
“Usinitazame kwa macho ya kike kike nimekuambia linywe hilo kojo lako”
Jijamaa lilizungumza huku mguu wake mmoja akiuweka mgongoni mwa deeva na kumfanya dereva kuanza kuunyonya mkojo wake uliopo juu ya sakafu inayoonekana ni mpya na haina siku nyingi tangu iwekwe
“Nimekuambia fastaa”.

Jijamaa likazidi kumuamrisha dereva wetu na kumfanya aongeze kasi ya kuunyonya mkojo wake hadi akaumaliza ndipo jamaa akamruhusu dereva kukaa kando.Jijamaa likanitazama mimi kwa macho makali na mimi nikanyanyuka na kujifanya na mimi ninamtazama kwa macho ya kibabe ila ndani ya moyo wangu unaoenda mbio  kama saa mpya laiti jamaa akijaribu kunitisha kwa kitendo chochote ninaweza kudondoka na kuzimia kwa woga hapo hapo.
“Dogo unaonekana mjanja sana wewe”

Kwa sentensi ya jamaa kidogo mapigo ya moyo yakakaa sawa na kijiubaridi kikapenya kwenye mwili wangu kwani tangu niingizwe ndani ya hichi chumba sikuweza kuihisi hali ya ubaridi.
“Yap”

Jamaa likanitazama kwa muda kisha likatafuta sehemu na kukaa hapo ndipo nikapata wazo la haraka haraka la kuzungumza huku nikikaa katika sehemu yangu.

“Broo yaani ingekuwa sio polisi hawa kutuwahi ningemalizia kumkata yule mwenye gari kichwa chake kama nilivyo wafanya watoto wake wawili na mkewe”.

Maneno yangu kidogo yakawafanya jamaa kunitazama kwa wasiwasi huku wakinitazama kwenye shati langu na kuziona damu zilizo jaa kidogo laiti wangejua ni damu za Manka nahisi wangenibamiza mamgumi mengi.

“Alafu ninausongo wa kujito muhanga na bomu bora nife kuliko kwenda jela.Hivi ule mfuko wa mabomu uliuficha pale pale ulipo uficha?”.

Nilimuuliza dereva swali amabalo naye akabaki anashangaa kwani nahisi ananiona kama nimechanganyikiwa ila lengo langu ni kujitengenezea hofu ya kuogopwa na mijamaa kwa maana bila ya kufanya hivyo usiku kwetu utakuwa mbaya na mrefu japo kwa dereva ulishaanza kuharibika.Nikamkonyeza kwa haraka dereva akatingisha kichwa kwa ishara ya kukubali.

“Tatizo lako wewe muoga ndio maana ukashindwa kuyachukua yale mabomu sasa kwa mfano polisi wakiyashika itakuwaje?Na huo uoga uoga wako ndio umekufanya umekunywa mikojo yako laiti ingekuwa ni mimi ningehakikisha asubuhi haifiki chumba kizima kimetapakaa damu”

 Mijamaa ikanitazama huku ikionekana kuwa na wasiwasi huku nahisi kila mmoja ananifikiria kivyake.Nikaanza kujipapasa kwenye mifuko yangu huku nikijifanya ninatafuta kitu ambacho sikujua ni nini.

“Kile kisu hao jamaa wamekichukua?”
“Ita..akuwa”
“Ingekuwa sio hivyo ningeondoka na roho ya mtu”
Jijamaa moja likavunja ukimya wao huku likijikoholesha koholesha na kunifanya nikae kimya kumsikiliza anataka kusema kitu gani.

“Oya daogo umeshatoa roho za watu wangapi hadi sasa hivi?”
“Daaa wengi sana kama kwenye tisini na nane au tisini na tisa”
“Ahaa utaonaje wewe ukamalizia list hiyo na ukawa wa mia moja”
“Mmmm……?”

“Usigune kwa maana tangu uiingie humu ndani una kazi ya kuropoka ropoka tuu oohhoo sijui nijitoe muhanga ohhooo nitamwaga damu.Jinsi unavyotuona sisi humu ndani ni wauji na nimajambazi sugu tena sana kama unajipenda funga domo lako tuna mawazo yetu sawa?”

Jamaa alizungumza na kunifanya nikaae kimya bila kuzungumza kitu cha aina yoyote huku nikimuomba Mungu asaidie asubuhi ifike mapema ili jamaa wasije wakanifanyia kitu cha aina yoyote.Asubuhi na mapema akaja askari huku akiwa ameongozana na mwanamke mmoja aliye valia suti na nikajua moja kwa moja nikajua atakuwa ameagizwa na mama kujua kutuoa.
“Ni wapi hao unaowatafuta kati ya hao watu humo ndani?”

 Askari alimuuliza mwanamke yule na akaanza kutuangalia mmoja baada ya mwengine na mwisho wa siku akatingisha kichwa kuashiria hayupo mtu anaye mtafuta kati yetu nikajikuta machozi yakianza kunilenga lenga huku nikimtazama mwanamke aliye simama nje ya ya mlango wa nondo.Mwanamke akaondoka na kumuacha askari akisimama na kututizama kisha akaanza kucheka.
“Dogo bado upo eheeee”

Askari akazidi kucheka huku akininyooshea kirungu chake na kuanza kukipiga piga kwenye nondo za mlango wa chumba hicho
“Oyaaa wewe fala unatupigia kelele”
Jijamaa limoja lilizungumza kwa sauti ya kukwaruza kwaruza huku likimnyooshea askari kidole
“Nyamaza wewe subirini hukumu yenu ya kunyongwa”
“Afande hadi sisi!?”
Nilimuuliza askari kwa mshangao na kuyafanya machozi yaanze kunimwagika.
“Tena nyinyi ndio mutakuwa wa kwanza na hiyo minjemba minne itafuatia”
“Acha kumrusha roho dogo wewe hebu tutolee hiyo sura yako kama kisigino chenye magaga”.

 Jijamaa linguine likamjia juu askari japo amembeza askari kuwa ana sura mbaya ila sura ya jamaa imezidi kwa ubaya kwani imechanwa chanwa kiasi kwamba imekuwa kama mistari ya mipaka kwenye ramani ya Dunia.Askari akaondoka huku akicheka,akili yangu ikaanza kumkumbuka Manka na sikujua kama yupo hai au amekufa na kujikuta nikizidi kutokwa na machozi ya uchungu na nikaanza kumuomba Mungu atende muujiza ili aweze kuyaokoa maisha ya Manka.Mida ya saa tatu asubuhi akaja askari mmoja na kutuita mimi na dereva na kabla sijatoka nikawaaga mijamaa kisha tukamfwata askari na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa polisi wa wilaya na kumkuta mama akiwa amekaa kwenye kiti huku amekasirika kiasi kwamba hata sikuweza kumsalimia.

“ Na wewe hapo kichwani umechanika na nini?”
“Shikamoo mama”
“Marahaba ehee ninakuuliza apo umechanwa na nini hapo kwenye paji la uso?”
“Kuna askari jana alinipiga kichwa na ngumi za kifuani”
“Kijana unaweza kuniambia huyu askari yupo vipi?”
“Mrefu hizi mweusi anaitwa Sele”
“Ahaa ok ngoja”

Mkuu wa polisi akanyanyua mkonga wa simu ya mezani kisha akaiweka sikioni na kuanza kuzungumza na mtu wa upande wa pili wa simu
“Nakuhitaji ofisini kwangu haraka”
“Ehee na nyinyi hebu nielezeni imekuaje kuaje hadi mkawa hapa?”

Mama alituuliza na dereva akaanza kuzungumza huku akijing’ata ng’ata na anavyo onekana anamuogopa sana mama.Ikanilazimu nianze kumuelezea mama kila kitu kilicho tukuta ila sikutaka kumuambia majeruhi niliyemuokoa ni Manka.Yule askari aliyenipiga jana usiku akaingia ofisini kwa bosi wake na kumpigia saluti na akaonekana kushtuka kumuona mama akiwa ofisini humo.

“Wewe ndio uliye mjeruhi mwanangu kiasi hichi?”
“Muheshimiwa mwanao ni mkorofi tena sana na anamaneno machafu sana”
“Kwahiyo ndio ummpige kiasi kwamba amechanika hapo usoni,wewe unajua ni jinsi gani nilivyopata naye tabu huyu mtoto hadi kufikia hatua hiyo aliyokuwa nayo?”
“Hapana mama yangu ila ukitaka kuhakikisha mwanao ni jeuri jana nilirekodi kila kitu alichokuwa akinijibisha na mimi”

 Afande Sele akatoa simu yake kisha akaweka sehemu sauti zetu tulizo kuwa tuna jibishana jana usiku kuanzia tulipokuwa barabarani hadi tulipofika kituoni.Mama akaachia msunyo mkali huku akinitazama kwa macho makali kiasi kwamba nikajikuta ninaanza kuogopa.

“Haya afande asante na samahani kwa kukusumbua……Afande Methew huyu kijana wangu niachie mimi nitamnyoosha tuu tembo hawezi kushindwa na mkonga wake”
“Sawa muheshimiwa waziri nimeshtuka sana akukuona huku kwetu asubuhi asubuhi”
“Aaaa wee acha tuu ni kwaajili ya huyu mjinga mmoja hapa.Haya kachukueni kila kitu chenu na niwakute kwenye gari”.

 Tukatoka na dereva na kupitia mapokezi na kukabithiwa kila kitu kilicho chetu kisha tukaenda kwenye gari la mama ambalo ni gari la kazini kwake.Baada ya muda mama akatoka huku akiwa ameongozana na yule askari aliyenipiga huku wakiwa wanazungumza kama marafiki kisha wakapeana mikono na kutufwata sisi tulipo na safari ikaanza huku akiendesha dereva wa kazini kwake.

“Eddy hicho kinywa chako kichafu umekianza lini na nani aliye kufundisha matusi?”
“Hakuna mama”
“Kwa hiyo siku hizi wewe umekuwa hadi unawatukana askari wa watu si ndio?”
“Mama wao walipo anza kukutukana wewe ndi…..”
“Ndio na wewe ukaamua kuwatukana….Unajua Eddy sishindwi kukuweka ndani hadi hicho kichwa chako kikae sawa…Unaljua hilo?”

“Likini mama wao ndio chanzo mimi nilikuwa ninarudi kuchukua sijui PF nini huku ili nikamtibu majeruhi tuliye muokoa sasa wao ndio wakaaanza chockochoko hadi wakanilaza ndani”
“Na wewe Hamisi kwa nini ulimuachia huyu mwehu aendeshe gari kazi imekushinda?”
“Hapana mama nakuomba unisamehe”
“Sasa ni hivi itabidi ukanionyeshe huyo majeruhi wenu aliye wachanganya hadi mkajikuta mnafanya vitu vya ajabu”
“Mama si wewe uendee tuu”
“Niende wapi?”
“Dar”

“Tena tukitoka kwenda kumtazama huyo mgonjwa wenu sote tunarudi Dar ukanieleze huo utumbo wako ulioufanya”
“Sawa je na gari tulilo kamatwa nalo lipo wapi?”
“Limeshapelekwa nyumbaini”
“Na nani?”
“Eheee usinihoji hoji maswali yako ya kijinga sawa?”
“Sasa mama hilo ni swali la kijinga?”
“Eddy mwanangu hebu niache kichwa changu kitulie”

    Kila tulivyo zidi kuifika Zahanati tuliyo mpeleka Manka jana usiku moyo wangu ukaawa unapoteza amaini kisi kwamba nikaanza kuhisi hali yahatari kichwani mwangu.Tukafika kwenye Zahanati na madaktari walipo muona mama wakaanza kuhaha kwani wanadhani amekuja kwa ajili ya kuwakagua.Mtu wa kwanza kukutana naye ni mganga(daktari) mkuu wa Zahanati hiyo
“Huo ndio utaratibu wenu wa kazi?”

Mama alizungumza huku akimshika shati huku likiwa limejikunja kunja kama limetafunwa na ngombe kisha likatwemwa
“Ha….haapa muheshimiwa”
“Na koti la kazi lipo wapi?”
“MMmmm lilipo ofisini?”
“Sasa hivi saa ngapi na muda wa kuripoti kazini ni saa ngapi?”
Daktari akaanza kubabaika babaika huku akijikuna kuna nywele zake zilizokosa kupitiwa na kitana kwani zimejinyongorota kiasi kwamba ni shida tupu

“Daktari mzima huna hata saa ya mkononi,pili haupo smart kimavazi unazani huyo mgojwa ukikuona wewe si ugonjwa wake unaweza kuongezeka kutokanan na uchafu wako,tatu unaonekana ndio unatoka kuamka mida hii na bado unanuka pombe kiasi kwamba unatia kinyaa.Sijui hata huo udaktari umeupataje”
“Hapana muheshimiwa”
“SNikimaliza unione”

 Mama akamuacha daktari na kuafuata wananchi walio kaa kwa wingi kwenye foleni isiyosogea kiasi kwamba wagojwa wamechoka sana na foleni hiyo.Akawasalimia wananchi na wakamuitikia kwa furaha kisha akaanza kuwahoji mwaswali,nikapata upenyo wa kwenda katika chumba alicho ingizwa Manka jana usiku na nikajikuta wasiwasi wangu ukizidi kuongezeka hii ni baada ya kumkuta Manka hayupo ndani  ya chumba hicho
    
ITAENDELEA....
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 15 & 16 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 15 & 16 ( Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by Unknown on 01:04:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.