Zaidi ya Wavuvi 9 Waliokuwa Wakifanya Uvuvi Mto Kagera Wafariki Katika Mazingira ya Kutatanisha

<script async src="//pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js"></script>
<script>
  (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({
    google_ad_client: "ca-pub-4220756307325687",
    enable_page_level_ads: true
  });
</script>




ZAIDI ya wavuvi tisa waliokuwa wakifanya shughuli zao za uvuvi ndani ya mto Kagera wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati tofauti.

Akisoma taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Lameck Mwigulu Nchema,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kanali mstaafu Shaabani Lissu alisema kuwa wavuvi hao wanatokea katika mialo ya Rubwela,Kanyika,katwe na Ruko katika ziwa ngoma.

Alisema matukio hayo ya vifo vya utata yameanza kutokea kuanzia mwezi wa pili mwaka huu wakati wavuvi hao wanapoenda kuvua ndani ya mto Kagera unaotenganisha nchi ya Rwanda na Tanzania.

"Mara nyingi wavuvi wakienda kuvua ndani ya Mto Kagera huwa hawarudi,huwa wanatekwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani ya Rwanda"Alisema Mkuu huyo wa Wilaya

Alisema hivi karibuni wavuvi wawili walienda kuvua ndani ya mto Kagera na mmoja aitwaye Emanuel Kahonda alipigwa risasi na kufariki dunia huku mwenzake Yoha Misago akinusurika katika tukio hilo na kukimbia na kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

"Mhe.Waziri ni juzi tu kuna mvuvi alipigwa risasi ndani ya mto Kagera hata msiba kwake bado upo, mwenzake aliyeshuhudia na kufanikiwa kuwatoroka wauaji hao yeye kunusurika ndiyo alikuja kutoa taarifa ofisini kwangu"alisema

Naye mwenyekiti wa mwalo wa Kitwe Ustadhi Hakimu alimthibitishia Waziri kuwa wavuvi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kuuwawa kikatili na askari wa nchi jirani ya Rwanda.

"Hapa kijijini kuna wajane wengi,waume zao walikuwa wakienda kuvua samaki ndani ya mto Kagera hawarudi,wanadai tunavua samaki kwenye maji yaliyopo nchi mwao,na mto kagera wameufanya wao peke yao,Tunaomba utusaidie Mhe.Waziri hili tatizo liishe

Upande wa kule kwao kuna misitu sana na huwa wanajificha humo,yaani wakikuona tu wala hawakusemeshi wanakupiga risasi tu humo humo majini,na maiti zimekuwa zikipotelea mtoni humo humo"alisema Mwenyekiti huyo.

Naye waziri wa mambo ya ndani ya nchini Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa kukutana na viongozi wa mialo ili wapate taarifa rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili waweze kutoa tamko rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.

"Hali hii imenistua sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa kikatili kiasi hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata kwa kuwasiliana na wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au ni uhalifu"alisema Nchemba.






<script async src="//pagead2.googlesyndication.com/pagead/js/adsbygoogle.js"></script>
<script>
  (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({
    google_ad_client: "ca-pub-4220756307325687",
    enable_page_level_ads: true
  });
</script>
Zaidi ya Wavuvi 9 Waliokuwa Wakifanya Uvuvi Mto Kagera Wafariki Katika Mazingira ya Kutatanisha Zaidi ya Wavuvi 9 Waliokuwa Wakifanya Uvuvi Mto Kagera Wafariki Katika Mazingira ya Kutatanisha Reviewed by WANGOFIRA on 21:44:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.