SERIKALI YA KUFIKIRIKA NA MIFUMO YAKE

Na, ABDUL NONDO
 0762599672
 
Tulizoea MCC huko marekani ikilazimisha wanachama wake kufuata masharti yake kabla haija zuia msaada.
Lakini leo nimeiona Tena MCC ktk nchi ya NIANZATA, nchi ya amani na utulivu, nchi ya NIANZATA ni nchi yenye raia walio katka u wanachama wa Jumuiya mbalimbali, Lakini viongozi wa kiifalme karibu wote wa nchi hii ya NIANZATA ni wanachama wa MCC.
 
Kutokana na uwanachama huu, kumezuka ubaguzi mkubwa miongoni mwa raia wake huku wakidai Ndio sheria ya Jumuiya hiyo, katika ngazi tofauti tofauti leo, nafasi mbalimbali Za majukum na ajira wamekuwa wakipewa wale tuu ambao ni wanachama wa MCC, na kuwatenga wale ambao sio wanachama wa MCC.
Mfano, ni miaka michache imepita TANGU ma DED wachaguliwe lakini mnakumbuka miaka kadhaa EDD Mmoja, mama yetu, Dada yetu alitenguliwa CHEO hicho Kwa sababu iliyosema sio mwanachama wa MCC bali yeye anatoka Jumuiya ya madola ya TCA,

Nchi ya NIANZATA Ina mambo kweli. Wafalme Hawa kweli wanamambo. Inasikitisha saana hadi chombo cha maamuzi kiitwacho NGEBU, kinaingiliwa na uongozi huu wa kiifalme, nchi hii haimruhusu Raia aongee ukweli, hata wawakilishi kadhaa kama mh. Ttozi wa goma, na mh. Suli wa ngida wamekuwa wakipurushana na walinzi wa serikali hii ya kiifalme ya NIANZATA,sababu ni kuongea ukweli.

Mh. Ttozi aliwahi mwaga unga wa rutba alipopata wasaa wa kuongea na raia, Mara punde akaitwa na walinzi wa kiifalme Kwa nini alikuwa anawapa unga wa rutba raia, Mara agizo likatoka Kwa mfalme kuwa hakuna ruhusa ya mikusanyiko Tena.

Kumbe hii ilikuwa JANJA tuu ili wenyewe wapate nafasi ya kuwalisha raia unga wa ndere badala ya rutba mikusanyo Yao MCC sio batili bali ya wengine ni batili,, mfalme huyu awe makini Kwa ubaguzi huu wa dhahiri anao uonesha.

Mbona sijawahi ona au sikia mwanachama wa MCC akipigwa na walinzi, akihojiwa na walinzi hii sio dhambi kusema WALINZI Hawa ni MCC, sababu wameshindwa kulinda raia, mfano, miaka 200 iliopita Kuna kijiji kilitekwa huko Kwa masaa 3, na majambazi Hawa wakachukua kila kitu kutoka Kwa raia, ila hakuna mlinzi aliyekwenda huko.

Sio uongo wala dhambi kusema MCC ipo kimaslahi binafsi na sio ya raia wake, ebu kumbuka kitabu cha sheria Za wananchi, kilicho undwa Kwa matakwa ya wananchi kikowapi, kilikanyagwa, kikasogezwa pembeni leo hii eti mfalme anasumbuka kutafuta kunguru anaye kula nyama, anatumia mkono kumkamata wakati alitupa mtego wa jaji mstaafu.


Nchi ya NIANZATA, na Serikali YA MCC. 

Nchi isiyopenda raia wake wajue ukweli, kuhoji, na kuongea ukweli, inapenda raia wale unga wa ndere na sio wa rutba, ha ha ha ha ni dhambi katika Imani yangu kumlisha raia unga wa ndere kwani pia ni kusaliti ukweli halisi ambae hata kipofu kipofu anauona.

SITALISHWA unga wa NDERE NITALISHA UNGA WA RUTBA. ili raia na rafiki zangu wasigeuki ZOMBI, wajitambue. ukishindwa elewa maana ya MCC ni MILLENNIUM CHALLENGE CORPORATION.

SERIKALI YA KUFIKIRIKA NA MIFUMO YAKE SERIKALI YA KUFIKIRIKA NA MIFUMO YAKE Reviewed by WANGOFIRA on 20:51:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.