FAIDA ZA KUNYONYA VIDOLE KWA WATOTO



 

Ripoti mpya inasema watoto wanaonyonya vidole au kung'ata kucha zao kwa meno huenda wasipate matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani.

Kwa mujibu wa waandishi katika jarida la Pediatrics, huo ni ni usafi dhanio,kwani yatokanayo na baadhi ya wadudu huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

Unyonyaji wa kidole gumba na ung’ataji wa kucha umeonekana kuzuia baadhi ya alergy.
Kati ya watu elfu moja wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi thelathini na mbili,walifanyiwa uchunguzi kwa muda nchini New Zealand.
Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali.

Uchunguzi uliofanywa na kurekodiwa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano na kumi na moja na wengine waliofanyiwa vipimo ni wenye umri kati ya miaka kumi na tatu na thelathini na miwili.

Huku thuluthi moja ya watoto hao ni wanyonyaji wa vidole mara kwa mara au hung’ata kucha zao na katika vipimo walivyofanyiwa watoto hao wameonekana kuwa wana kiwango kidogo cha kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani

Lakini tabia hii ya unyonyaji vidole na ung’ataji kucha haisaidii watu wenye pumu au mtu anapopata homa kali. 
 
Watoto wanaoweza kupata matatizo ya kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani (alergy) kutokana na vitu kama vumbi kutoka majumbani,manyoya ya paka au mbwa, lakini watoto wenye kunyonya vidole gumba na kung’ata kucha walikuwa ni chini ya theluthi moja kuliko watoto wenye tabia hii ya unyonywaji vidole.

Na tabia hii ya unyonyaji vidole au ung’ataji kucha inaonekana kuwa kinga mpaka wanapofikia umri wa utu uzima.
 
" kuwa na paka au mbwa majumbani,ndugu au jamaa wanaofanya kazi mashambani pia imeonekana kuwa ni sababu kubwa inayosababisha mazingira ya ukuaji wa magonjwa yanayosababishwa na

kuathirika kutokana na mazingira hewa au kula vyakula fulani


CHANZO; BBC
FAIDA ZA KUNYONYA VIDOLE KWA WATOTO FAIDA ZA KUNYONYA VIDOLE KWA WATOTO Reviewed by WANGOFIRA on 06:36:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.