WAZAZI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MARAFIKI WA WATOTO WAO.
Kutokana
na baadhi ya watoto kuwa na tabia ambazo hazipendezi watu bila ya
kufahamu chanzo chake, imeelezwa kuwa ni vyema wazazi wakajenga mazoea
ya kuwafahamu watu ambao wanakuwa karibu na watoto wao ili kuchukua
hatua mapema.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies
Zone, Usia Nkhoma Ledama wakati wa mahali ya nne ya shule hiyo ambapo
watoto wa ngazi mbalimbali za madarasa walihitimu.
Usia alisema kuwa wazazi wengi wamekuwa wakitumia muda wao mwingi
kujishughulisha na kazi zao bila kuwa na muda wa kukutana na watoto wao
na hivyo kuwa ngumu kutambua chanzo cha tabia ambazo zinaibuka kwa
watoto wao kutokana na wao kutowafatilia watu ambao wanakuwa karibu na
watoto.
"Tunafahamu wazazi wengi mnakuwa busy na kazi zao na hivyo mtoto
akitoka shule anakuwa na dada au kuangalia tv lakini akiwa katika
michezo na watoto wenzake mnakuwa hamjui ni vitu vya aina gani
wanafanya,
"Nadhani ni vyema sasa kuhakikisha mnawafahamu marafiki wa watoto
wenu, marafiki zao wa shuleni na marafiki zao wa nyumbani, huwezi kujua
wanafanya nini kama huwafahamu tabia watoto wanaocheza nao lakini kama
ukiwajua unakuwa unafahamu rafiki anayefaa ni yupi," alisema Usia.
Aidha aliwatoa hofu wazazi kuwa shuleni hapo wanawafundisha watoto
tabia njema na wanawafahamu vyema wanafunzi wao hivyo kazi kubakia kwa
wazazi kuhakikisha wanakuwa makini na watoto wanapokuwa nyumbani.
Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma
Ledama (kushoto) akizungumza na mmoja wa wazazi Bw. Ally Msoya
alipowasili kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika katika
ukumbi wa Msasani Tower jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Modewjiblog)
Kwa upande wa mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mkurugenzi
Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga aliwapongeza wanafunzi ambao wamehitimu
masomo na wazazi kwa moyo wao wa kujitoa kuwasomesha watoto wao lakini
pia kuwataka kuwasimamia vyema watoto wao ili waweze kufika mbali
kielimu.
"Elimu ni muhimu sana kwa watoto wenu wanatakiwa kusoma ili kufika
mbali kimaisha niwasihi kuwasimia vyema watoto ili wanapokuwa shuleni
wafanye vizuri na wanaporudi nyumbani pia wafanye vizuri," alisema Eda.
Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mhitimu wa darasa la Laurey, Thomas Mboya akiongoza watoto wenzake
kwenye burudani maalum wakati wa mahafali ya nne ya shule hiyo.
Mwanafunzi wa Lilies Class, Iptihaj Kinyaga akiongoza darasa la
wanafunzi wenzake kutoa burudani kwa wazazi kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wa Laurel Class wakitoa burudani ya kuagana na wanafunzi wenzao katika mahafali ya nne ya shule hiyo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo
Bwana na Bibi Lugoe wazazi wa mhitimu Abigail Lugoe wakiwa meza kuu.
Wazazi wa Watoto ya O'Jays Kiddies Zone wakitazama burudani na
vipaji mbalimbali vilivyokuzwa shuleni hapo kutoka kwa watoto wao.
Lantana Class wakitoa burudani kwenye mahafali ya kaka na dada zao
Mkurugenzi wa Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma
Ledama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mama Eda
Sanga kutoa risala kwenye mahafali ya nne ya shule hiyo yaliyofanyika
jana kwenye ukumbi wa Msasani Towers jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA,
Eda Sanga akitoa nasaha kwa wazazi na walezi waliohudhuria mahafali ya
nne ya darasa la Laurel Shule ya Watoto ya O'Jays Kiddies Zone
yaliyofanyika katika ukumbi wa Msasani Towers jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na walezi wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi.
Wazazi maalum wa mtoto Abigail Lugoe, Bwana na Bibi Lugoe wakitoa
shuhuda ya malezi bora na elimu aliyoipata mtoto wao ambaye mwakani
atajiunga na darasa la kwanza. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Watoto
ya O'Jays Kiddies Zone, Usia Nkhoma Ledama.
Wazazi wakiendelea kushuhudia matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye mahafali hayo.
Bw. Ally Msoya na familia yake.
Kutoka
kushoto ni Victoria Martin, Thuwein Makamba na Husni Seif, LTE
Specialist wa Tigo Tanzania katika mahafali shule ya Shule ya Watoto ya
O'Jays Kiddies Zone.
Dada Faiza Ally akibadilishana mawazo na mmoja wa wazazi katika mahafali ya shule hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Eda Sanga akimtunuku
cheti, Joylyn Marandu mhitimu wa Laurel Class katika mahafali ya nne ya
shule hiyo.
Wahitimu wakiendelea kutunikiwa vyeti.
Mhitimu Patrick Kasanga akipokea cheti chake. (Picha zaidi ingia hapa)
WAZAZI WATAKIWA KUWA MAKINI NA MARAFIKI WA WATOTO WAO.
Reviewed by WANGOFIRA
on
10:20:00
Rating:
No comments: