Nape Nnauye Aungana na Watanzania Wengine Kupokea Mwili wa Senga Aliyepiga Picha za Mauaji ya Mwangosi

 

Moja ya habari iliyotawala Julai 28 2016 katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari ilikuwa ni pamoja na hii ya kutokea nchini India iliyohusu kifo cha mpiga picha wa Gazeti la Tanzania Daima Joseph Senga aliyefariki akiwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo. 




Marehemu Joseph Senga ndiye mpiga picha aliyenasa tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari wa kituo cha talevisheni CHANEL 10 Daud Mwangosi kilichotokea September 2 2012 katika kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.



Jana Julai 30 2016 mwili wa marehemu Joseph Senga tayari umewasili nchini ukitokea India, ambapo Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye aliungana na baadhi ya watanzania wakiwemo wapiga picha wenzake wa kutokea vyombo mbalimbali vya habari. 

Tayari nimekusogezea picha kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam 

 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) na baadhi ya waandishi wa habari na wapiga picha, wakilitazama jeneza lenye mwili wa Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeneza hilo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. 



Waziri Nape Nnauye na wananchi wakishiriki kubeba jeneza 

 

 


Baadhi ya wapiga picha wakiongozwa na Loveness Bernard wakiwa katika vazi la pamoja 


Wapiga picha kutokea vyombo mbalimbali vya habari walipokuwa wakiusubiri mwili wa marehemu 

 
Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili 

Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere 
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa
 

  
Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga 

Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili 

Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwili wa marehemu Senga kuwasili 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambo na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo 
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo 
 
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka
 (Picha zote na Othman Michuzi na Khalfan Said)
Nape Nnauye Aungana na Watanzania Wengine Kupokea Mwili wa Senga Aliyepiga Picha za Mauaji ya Mwangosi Nape Nnauye Aungana na Watanzania Wengine Kupokea Mwili wa Senga Aliyepiga Picha za Mauaji ya Mwangosi Reviewed by WANGOFIRA on 21:00:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.