Awa BUBU Baada ya Kugombana na Mpenzi Wake

Mkazi wa Shunu kata ya Nyahanga mjini Kahama mkoani Shinyanga, Baraka John (22) amejikuta akishindwa kuzungumza baada ya kugombana na mpenzi wake MAGRETH JOHN nyumbani kwake katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.
 
Mashuhuda wa tukio hilo PAULO SAMWELI na RICHARD JACOB wamesema baada ya kufika eneo la tukio walimkuta BARAKA hawezi kuzungumza chochote hali ambayo ilisababisha watoe taarifa kwa uongozi wa mtaa. 

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Shunu, KUBE SHIJA amesema kuwa baada ya kupokea taarifa za tukio hilo waliamua kwenda kumkamata MAGRETH JOHN na mama yake aliyetambulika kwa jina la MAMA MAGRETH.

Tukio hilo la aina yake, lilizusha hasira miongoni mwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo na kutaka kuishambulia familia ya msichana huyo hali iliyomlazimu SHIJA kuwasihi wasichukue sheria mkononi na kuviacha vyombo vya usalama vifanye kazi yake. 

Naye Afisa mtendaji wa mtaa huo wa Shunu BENJAMINI MAKELO akizungumza na Kahama Fm kwa njia ya simu amesema baada ya MAGRETH na Mama yake kufikishwa Polisi na kuhojiwa, ghafla hali ya BARAKA ilibadilika na kuanza kuzungumza. 

Tukio hilo linalohusishwa na ushirikina ni la pili kutokea mjini Kahama wiki hii. 

Jumatano iliyopita kijana mmoja mkazi wa Majengo aliyetambuliwa kwa jina la MLINDA alikutwa mlangoni kwa bibi Kizee mmoja akiwa hawezi kuzungumza wala kuondoka. na bado watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na polisi.


SOURCE: KAHAMA FM
Awa BUBU Baada ya Kugombana na Mpenzi Wake Awa BUBU Baada ya Kugombana na Mpenzi Wake Reviewed by Unknown on 20:24:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.