Mwili wa Marehemu Senga kuagwa Sinza Leo


MWILI wa aliyekuwa Mpiga picha Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, unatarajiwa kuagwa kesho nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam, baada ya kuwasili leo ukitokea New Delhi nchini India. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Neville Meena, mwili huo utawasili saa 7:00 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya shirika la Ethiopia  (Ethiopia Airlines) na kupelekwa moja kwa moja Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuuhifadhi. 

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mwili wa marehemu Senga utapelekwa nyumbani kwake Sinza White Inn (Mtaa wa Sinza E) Jumapili kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya shughuli ya kutoa heshima za mwisho. 

“Saa 5:00 asubuhi tunatarajia shughuli za kuuga zitakuwa zimekamilika. Hivyo kutoa fursa ya kuanza kwa safari ya kuelekea Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi ambayo yamepangwa kufanyika Jumatatu,” ilieleza taarifa hiyo. 

Kabla mauti hayajamkuta, Senga alikwenda nchini humo Julai 12 mwaka huu  kwa ajili ya matibabu ambako Julai 19 alifanyiwa upasuaji wa moja ya mishipa ya moyo. 

Upasuaji huo ulimalizika salama na aliruhusiwa kutoka hospitalini Julai 27 jioni lakini ghafla hali yake ilibadilika na aliporudishwa hospitalini hata hivyo mauti ilimkuta.
Mwili wa Marehemu Senga kuagwa Sinza Leo Mwili wa Marehemu Senga kuagwa Sinza Leo Reviewed by Unknown on 20:48:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.