RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 29 & 30 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Kwa nguvu zungu zote nikarusha teke lililo mpiga kwenye miguu yake kwa nyuma na kumfanya aanguke kama mzigo wa kuni na akaangukia pua kitendo kiliho shuhudiwa na watu wengi ikiwemo askari walio anza kukimbia wakija kwenye eneo tulilopo huku bunduki zao zikiwa mikononi mwao huku wakinimrisha nisifanye kitu cha iana yoyote na john akabaki akiwa haamini kitu alicho kiona

Endelea...
Nikamnyanyua mwanasheria wa  serikali  na kumuamrisha kuelekea lilipo gari lake na askari walio kuwa wakinifwata wakajikuta wakisimama huku wakionekana kunishangaa.Ila mmoja wao akanifwata akiwa na bunduki yake na kumbukumbu zikanikumbusha kuwa ni askari wa getini ambaye mara ya mwisho alinisaidia katika kotoroka mikononi mwa baba
“eddy vipi tena?”
“safi”

Nilizungumza huku nikumuongoza mwanasheria hadi kwenye gari lake nikamuomba funguo yake kilazima na akaitoa kabla sijaingia kwenye gari nikastukia nikiguswa bega na nikageuka nikakutana na sura ya askari wa getini
“kaka eddy huyo mkuu ana nini?”

“si unamkumbuka yule binti niliye kuwa naye siku ile tulivyo kuwa tunatoroka home?”
“ndio si amehukumiwa kifuno cha maisha tayari?”
“ndio ila kwa kosa la kuonewa sasa ndio huyu fala ninamuomba anipeleke alipo anakazi ya kunizingua hapa”
“ahaa mimi ninapajua tunaweza kwenda pamoja”

Tukaingia ndani ya gari na kumkabidhi askari wetu wa getini funguo ya gari na safari ikaanza.Kitu ambacho ninakishukuru kutoka kwa askari wetu wa getini ni kuwa mtu muelewa japo ni askari wa jeshi la polisi ila mama alipendekaza kuwa askari wa kuilinda nyumba yetu kutokana na upole na hekima aliyo nayo ni tofauti na maaskari wengine ambao wana dharau kiasi kwamba mtu unashindwa kuwadhamini katika maisha.

“kaka eddy unajua hata mimi niliamini kuwa umefariki dunia?”
“sijakufa ndugu yangu ila wee acha tuu”
“basi unajua habari za kifo chako zilinistua kiasi kwamba nikawa nipo njia panda kwa maana yule binti kwa muonekano anaonekana anakupenda kiasi kwamba hasikii la mtu juu yako sasa sikuelewa nilipo ambiwa kuwa amesababisha kifo chako”

“najua zote ni mbinu za mzee ila zitafikia mwisho”
“jamani ninaomba munisikilize”
Mwanasheria wa serikali alizungumza na kutufanya sote tukae kimya na kumsikila kitu anacho taka kutuambia
“jamani ukweli ni kwamba sheila hajanyongwa japo mahakama ilitoa hukumu ya namna hiyo”
Sote tukajikuta tukiguna kila mmoja kwa mtindo anao ujua yeye mwenyewe kiasi kwamba tukabaki tukimsikilizia kitua atakacho kizungumza.

“ukweli ni kwamba mr godwin alitokea kumpenda yule binti na akahitaji tuweze kumhukumu hivyo ila yeye amepanga safari ya kwenda naye kuishi visiwa vya komoro na hapa ninavyo zungumza amenitumia meseji akidai yupo uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea visiwa vya comoro”

Nikajihisi nguvu za mwili zikiniiishia kiasi kwamba nikabaki nikiwa kimya nisijue nini cha kufanya na hasira kali dhidi ya baba yangu ikanipanda na kujikuta nikinyang’ata meno yangu kiasi kwamba sauti ya msuguano wake ikasikika kwa kila mtu.
“muheshimiwa amekuambia kuwa anaondoka na ndege ya saa ngapi?”
“ngoja niwaonyeshe meseji aliyo nitumia”

Mwanasheria akatoa meseji aliyo tumiwa na baba na kuanza kumuonyesha john ambaye nikamshuhudia akishusha pumzi nyingi kiasi kwamba akionekana kuchoka na kile alicho kisoma na kabla hajamuonyesha askari wetu wa getini nikampokonya simu na kuisoma meseji iliyopo kwenye simu yake.

{mr kilongo mimi nipo nipo uwanja wa ndege ninaelekea visiwa vya comoro kula raha na huyu mtoto,jana nimemuonja ni mtamu sana.Ile pesa nimekuingizia kwenye akaunti yako asante kwa kazi nzuri uliyo ifanya na hakikisha unamalizia juhudi za kuzibinafsisha mali za mke wangu nitakupa robo ya utajiri wangu}

Nikabaki nikiwa ninatetemeka kwa hasira kiasi kwamba nikajihisi michuruziko ikinitoka puani kwangu na matone baadhi yakadondoka kwenye mapaja juu ya nguo za wauguzi nilizo zivaa na kugundua kuwa ni damu ndio zimenitoka puani na sikujua zimesababishwa na nini kwani ndio mara yangu ya kwanza kutokwa na damu za puani.John akanipa kiatambaa chake na kujifuta damu zinazo nitoka na askari akasimamisha gari pembeni ya barabara na wakaniomba nishuke nipigwe na upepo wa wa halisi kulilo ic iliyo tawala ndani ya gari.

Nikashuka na kuinama chini na damu zikanitoka kidogo na chakumshukuru mungu zikakata japo kichwa nikaanza kukihisi kikiwa kimetaliwa na maumivu makali
“unajisikiaje?”
“kichwa kidogo kina gonga”
“noja tukakutafutie dawa”
”hapana twendeni air port”
“utaweza kweli eddy?”
“john usijali kwa hilo nitaweza tu”

Tukaingia ndani ya gari na safari ikaanza upya na kwawakati huu tukaelekea uwanja wa ndege na hatukuwa na uhakika sana kama tunaweza kuwaona baba na sheila au laa.Tukafika uwanja wa ndege na sote tukashuka kwenye gari na mimi nikawa wa kwanza kuelekea sehemu ya abiria na nikajitahidi  kuyapa wepesi macho yangu katika kuwatazama watu wengi waliopo kwenye eneo hili ili niweze kuwaona baba na sheila ila juhudi zangu zikagonga mwamba kwani sikuweza kuwaona.

Kwa kupitia kioo kikubwa kinacho onyesha sehemu ndege zilipo simama na kuwashuhudia baba akiwa amemshika sheila kiuno wakimalizi ngazi ya mwisho kuingia ndani ya ndege na kunifanya niaze kumuita sheila huku mkono wangu mmoja ukipiga kioo ila hawakuweza kunisikia na kuwafanya askari waliopo uwanja wa ndege kunishika na kunizui kitendo kilicho nifanya machozi kunimwagika kiasi kwamba nikaanza kupata maumivu ya kiua.

John na askari wa nyumbani kwetu wakanichukua na nikaishuhudia ndege waliyo panda sheila na baba ikiacha ardhi na kupaa angani na kunifanya nishiwe nguvu na kujikuta nikianguaka chini.John na weza watu wengine wakaninyanyua na sikujua ni wapi wananipeleka na kujikuta nikiwa kwenye kitanda cha matairi na kuingizwa ndani ya gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali.Madaktari wakaanza kunifanyia uchunguzi na wakanichoma sindano ambayo sikujua inakazi gani mwili mwangu.

Ndani ya madaa matano madaktari wanipa ruhusa ya kutoka huku wakiwa wamenifungushia na baadhi ya vidonge vya kunywa pale nitakapo tokwa na damu kwani waliniambia chanzo cha damu kunitoka puani ni kutokana na kuwaza sana kiasi kwamba mishipa yangu inayopandisha damu kichwani husindwa kufanya kazi vizuri.Askari wetu wa getini akanipeleka nyumbani kwake ambapo anaiishi peke yake kwenye chumba kimoja alicho pangisha maeneo ya mbagala rangi tatu.Na tukafika kweye nyumba iliyo jaa wasichana wengi ambao kitendo cha sisi kupita mbela yao wakaanza kunong’onezana na kucheka kwa kicheko kikubwa.

“eddy wazoee ndivyo walivyo hawa wanawake humu ndani?”
Askari wetu wa gatini alizungumza na sikumjibu kitu cha aina yoyote na sote tukaingia ndani ya chumba chake alicho kihaza viti vingi vya dhamani
“eddy jisikie huru ndugu yangu”
“asante”

“hapa ninaishi peke yangu ila ni mara chache mke wangu anakuja kutokana yupo masomoni arusha”
“ni mwanafunzi wa sekondari au chuo?”
“ni mwanafunzi wa sekondari yupo shule moja hivi ya bodi na miezi minne ya nyuma wamechoma shule yao ila wazazi wake wamempeleka shule ya wasichana iringa”
“ahaaa anaitwa nani?”
“salome alex edward”

Moyo ukanipasuka na kujikuta nikimtaza askari wetu wa getini kwani salome anaye mzungumzia ni yule miongoni mwa wapenzi wangu japo mimi na yeye tumeachana kwa katika mazingira ya kutatanisha na mbaya zaidi ametembea na mkuu wa shule na ameambukizwa virusi vya ukimwi.

“yule dogo ninampenda sana hadi imefiki hatua mimi ninamlipia ada ya advance”
“yupo kidato cha ngapi?”
“kidato cha tano japo sasa hivi anadani kuwa nimuache asome ndio tutaendelea na mapenzi imenilazimu nimsomeshe kwani familia yake ni duni sana”

“mmmm pole sana ndugu yangu”
“kwa nini unanipa pole”
“jukumu la kumsomesha mtu ni kubwa sana na ikitegema ndio hivyo wazazi wake hawajiwezi kiuchumi”
“ndio ndugu yangu si unajua mwanaume unatakiwa kujikaza na tumeubwa kupambana na ile pesa uliyonipatia kidogo ilinisaidia kumlipia ada na matibabu hospitalini”
“alikuwa anaumwa na ugonjwa gwani?”
“waliniambia kuwa ni mstuko wa moyo”
“ahaa ndugu yangu hongera sana”
“asante ndugu yangu”

John akanionyesha nguo za kuvaa nikitoka kuoga kutokana ni uswahilini ikanilazimu kutoka na kindoo cha kuogea huku nikiwa nimeshika kopo lenye sabuni na john akanionyesha bomba la maji na nikakuta kuna kindoo kimekigwa ikanilazimu kusubiri kwa muda na kuna wamama wawili wapo pembeni wanapika vyakula vyao kwa ajili ya jioni wakaanza kunong’onezana taratibu.

“eheeee osama bin laden ameingia mbagala jamani....Mabomo yasije yakalipuka tena”
“shosti sema wewe obama nikisema mimi bush nitaambiwa ninakiherehere”
“mmmm na hayo mandevu sasa unaweza kusema kama kama paka aliye mwagikiwa na mchuzi wa moto”

Moja kwa moja nikajua wananisema mimi kotokana na jinsi nilivyo na ndavu nyingi ambazo zimenifanya kuonekana na sura ya kutisha.Nikabaki nikiwa nimewatazama kwa jicho la hasira mpaka wakajistukia.Nikaona nikiendelea kusimama katika bomba watanikera zaidi na nilicho kifanya ni kuyamimina maji yaliyopo kwenye kindoo nilicho kikuta na kuyaweka kwenye ndoo yangu na kabla sijaondoka mama mmoja akasimama na kunifwata kwa haraka huku akubwatuka

“wee wee usijifanye muhuni rudisha hayo maji sehemu ulipo yatoa”
“kwani si nimekikinga kindoo chako si kitajaa?”
“koma mwanaume mzima ovyoo unazani pale nimekalisha makalio yangu bure...Nimekaa ili kindoo changu kijae maji”
“samahani kama nimeuudhi”

Nikayamimina maji niliyo yatoa kwenye kindoo cha huyu mama ambeye sikujua ni kwanini amenichukia pasipo kuwa na sababu maalumu kwani ni siku yangu ya kwanza kufika atika nyumba hii ila wanaonekana kunichukia sana”

Nikakikinga kindoo changu hadi kikajaa na kwenda nacho kweye bafu alilo nionyesha askari wetu ambaye hadi sasa hivi nilisahau jina lake kani nilisha zoea kumuita afande.Nikaoga na kumaliza na kurudi ndani kwangu na kumkuta askari wetu akivaa nguo nyingine za kazini.

“unaondoka?”
“ndio kaka hapa nimepigiwa simu ninahitajika lindo si unajua nilitoaka pasipo kuaga inanilazimu kwenda kufidi muda niliokuwa sipo kazini”
“ahaa sawa ndangu yandu ila mbona hawa mama humu ndani wamekuwa watu wa maneno ya chini chini?”
“hao wamama huwa wanapenda kumpima mtu....Hata mimi kipindi nilipokuwa ninakuja walikuwa wanavimaneno vya chini chini hadi kuna siku kuna mama nilimzaba makofi ndio wote wakaniheshimu”

“wana waume?”
“ndio wana waume zao ila waume zao nao ni wanaume suruali”
“wanaume suruali kivipi?”
“wanawategemea wake zoa wao kila ikifika asubuhi hukaa maskani hadi mida ya kula ndio utawaona wakirudi mmoja mmoja”
“mmmm ndio maana wake zao wanakuwa na dharau?”
“ndio hivyo ndugu yangu”
“kaka hivi unaitwa nani?”
“eddy ina maana siku zote hulijui jina langu?”
“silijui ndugu yangu?”
“mimi ninaitwa afande josephat”

Josephat akanipa elfu kumi kwa ajili ya kununua chakula cha usiku kisha yeye akaondoka na mimi nikavaa nguo zake alizo nipa nizivaa kisha nikaenda kununua chipsi kwenye kibanda kisicho mbali na sehemu ya nyumba yuliyopo na nikarudi na kabla sijaingia mlangoni nikakutana na msichana ambaye sikuwahi kumuona akiwa anagonga mlango wa chumba cha josephat.

“mambo vipi kaka?”
“salama vipi?”
“safi tuu jose nimemkuta?”
“hapana amekwenda kazini”
“hawezi kurudi leo?”
“sijajua”
“ahaa mimi ni mgani wake ameniambia kuwa nije je nimsubiei huku kwake?”
“mmmm amekuambia saa ngapi?”
“ahha..Si....Sijana”

Dada alizungumza huku akiwa anajing’ata ngat’ata kiasi kwamba sikuwa ninamuelewa ni kitu gani kilicho mleta na akapita dada mmoja na akaropoka neno lililo muudhi dada niliye simama naye
“wewe asha ngedere usione chaka mavi yanakubana utakuja kufa nyoo mwanamke kila ukimuona mwanaume kidubwasha chako kina kuwasha”
“koma na wewe sura mbaya kama kwapa la bibi kizee”
“wee wee tena utaifananisha sura yangu na hilo sura lako kama ku** ya changudoa aliye kosa mteja”

Maneno yao makali yakawafanya wapangaji waliomo kwenye yumba vyao kutoka wakiwa wanashangaa majaibizanio yao,sikutaka kuwaingilia nisije na mimi nikavurugwa bure nilicho kifanya ni kuingia ndani na kufungua mlango na nikasikia masufuria yaliyo pangwa kwenye kordo yakianguaka huku watu wangine wakishangilia na nikagundua wanapimana lishe na nilicho kifanya nikufungulia redio yenye spika kubwa hadi mwisho na sikuzisikia sauti zao wakigombana.

Baada ya muda ugomvi wao ukaisha kisha na nikapunguza sauti ya redioa na kuanza kula nilicho kinunua huku nikiwa siamini kama ipo siku nitaishi maisha kama haya ninayo yaishi na mipango ya kwenda ikulu ikaanza kujipanga taratibu kichwani kwangu na lengo zima ni kwenda kujua ni jinsi gani wataweza kunisaidi juu ya kumpata mama.Kwa msongamano wa mawazo mengi nikajikuta nikipitiwa na usingizi kwenye sofa moja lililopo kwenye  chumba hicho kilicho jaa vitu vingi na mbaya zaidi kina dirisha moja tuu.

Nikastushwa na mlango unao gongwa huku nikiisikia sauti ya josephat ikiita nje ya mlango.Nikanyanyuka na kwenda kumfungulia mlango na akaingia huku akionekana kuwa na haraka sana.

“kaka nimepata safari ya kikazi naelekeaa kagera”
“kuna nini tena?”
“ni maswala ya kikazi tu na ninaweza kukaa hata wiki hapo nimekuja na wezangu wananisubiria hapo nje”
“ahaaa kwani ni saa ngapi saa hizi?”
“nane usiku”

Afande josephat alizungumza huku akidumbukiza nguo zake kwenye begi na la mgongoni kwa haraka akachukua vitu vyake muhimu kisha akatoa elfu hamsini na kunipatia kisha akaiiandika namba yeke ya simu pembeni na kuniambia endepo nitapata tatizo lolite nitafute simu kwa ajili ya kumpigi.Akatoka na mimi nikarudi kitandani na kujibwaga na kutokana na uchovu mwingi usingizi ukanipitia tena wa safari hii ulizidi usingizi wa mwazo.

Kwa mbali nikahisi mlango ukifunguliwa nikayafumbua macho yangu na kugundua mwanga wa juu ukiwa umetawala ndani ya chumba changu ikiashiria kumesha pambazuka.Nikayapeleka macho yangu mlangoni kumtazma mtu anaye usukuma sukuma mlango na akaingia kwa haraka
“sapraizzzz baby jos........”

Macho yangu yakakutana na salome ambaye alishindwa kuimalizia sentensi yake na sote tukabaki tukitazamana kwa mshangao huku yeye akionekana kunishangaa zaidi......

                          *****sory madam*****(30)
   
Nikajinyanyua tararibu kitandani na kukaa kitako huku salome naye akiliingiza begi lake la nguo na kuliweka pembeni na taratibu akakaa kwenye sofa lililopo ndani ya na kuanza kuminya minya vidole vyake vya mkononi huku sura yake akiwa ameilekezea chini akionekana kujawa na aibu kubwa ikanilazimu kuanza kumsalimia.

“mambo”
“powa vipi?”
“salama za huko utokapo?”
“mmmm....?”
“za huko utokapo vipi?”
“nzuri tu”
“karibu mbona unaona aibu?”
“eheee walaa jose yupo wapi?”
“ahh amesafiri kikazi”
“mungu wangu sijui itakuwaje?”
“iakuwaje nini?”
“mmmm hamna mwaya”

Nikanyanyuka kitandani huku nikiwa ninawenge la usingizi kidogo na nikaanza kuvinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo na kama kawaida ya wanaume wengi walio kamilika kimaumbile pale wanapo amka ni lazima koki zao husimama kuashiria ni siku mpya hii na ndivyo ilivyo kwangu jambo lililo mpelekea salome kuyagandisha macho yake kwenye koki yangu pasipo kuyapepesa hata kidogo.Nikawasha redio na kuifungulia sauti ya kawaida kisha nikarudi kukaa tena kitandani na salome akatoa simu yake aina ya samsung galax na kuanza kuiminya minya kisha akaiweka sikioni.

“jose jamani upo wapi?”
“sasa utarudi lini wakati mimi nipo kwako nilikuja kukufanyia supriz naona supriz yenyewe imeharibika”
“nimpe simu nani?”
“haya........Eddy ongea na jose simu ipo hewani”
“mmmm vipi kaka jose”
“safi.....Sasa huyo bibie ndio hivyo kaja bila taarifa”
“ndio”

“basi ninakuomba ukatafute hata sehemu ya kujishikiza kwa hizi siku ambazo nitakuwa sipo na yeye aishi ndani humo hadi nitakapo rejea”
“ahaaa powa kaka”
“hakikisha unafanya hivyo bwana....Huyo ni malkia wangu muache ajitanue ndani kwangu”
“sawa mzee......Chukua simu yako”
“eeehe baby”
“ahaa ataondoka eheee”
“haya kazi njema”
“I love too mwaaaaa”

Salome akakata simu na kuachia tabasamu pana ila kwa upande wangu nikajikuta roho yangu ikiwa inauma kupita maelezo kwani kitendo cha kuambiwa kuondoka kikabaki kikiniumiza na sikuwa na jinsi ya kufanya.Nikanyanyuka kiustaarababu na kuzitoa ndala chini ya uvungu nilizo kwenda kuogea jana usiku na kuzivaa vizuri na kusimama kwenye kioo kikubwa na kujitazama jinsi sura yangu ilivyo jaa ndevu zisizo na mpangilio na kunifanya nionekane kama mzee wa miaka 70 na zaidi kumbe ni kijana mdogo tu wa miaka ishirini naa.

“nawatakia maisha mema wewe na mchumba wako”
“eddy unakwenda wapi?”
“sijajua ila ngoja niondoke”
“eddy...”
“salome wewe tayari umesha mpenda mtu mwengine kuwa na mimi hilo litakuwa ni ngumu”
“powa nenda”

Salome akajibu kwa dharau na kunifanya nimtazame kwa muda huku machozi yakianza kunilenga lenga na kuyakumbuka mambo mema niliyo mfanyia salome kuanzia siku ninampa pesa ya matumizi kipindi tupo shule na alipo poteza pasa yake hadi siku ninamkuta na mkuu wa shule wakitoka kwenye mlango wa chumba cha hotel kisha taratibu nikashika kitasa cha mlango.

“salome naamini unaijua afya yako ila ni bora ukamueleza ukweli jose kuliko kumuua pasipo yeye kujua”
“nashukuru kwa ushauri wako ila ukweli ni kwamba sijaadhirika kama unavyo dhania”
“sawa kama ni hivyo”
“powa nenda usije ukanivunjia ndoa yangu na mume wangu mtarajiwa....Ila umeachwa nini na mpenzi wako mbona umechakaa hivyo kipindi kile nilivyokuwa nikikuomba msamaha ukawa unanidharau haya pole mwaya”

Maneno ya salome yakaniumiza kiasi kwamba nikajikuta nikitokwa na machozi kisha nikafungua mlango na kutoka nje na mtu wa kwanza kukutana naye ni yule mama wa jana aliye ninyang’anya maji yake na baada ya kuniona akaanza kucheka kwa kicheko cha kejeli

“heeeheee osama na wewe pia unalia makubwa haya”
Nikasimama na kumtazama kwa macho makali na akaendelea kujichekesha kitendo kilicho anza kunipandisha hasira na nikapiga hatua za haraka hadi alipo simama na sura yangu nikaisogeza karibu na sura yake huku ndevu zangu zikiwa zinamgusa kwenye mashavu yake na akakaaa kimya kiasi kwamba akaanza kutetemeka
“nitakuua”

Nilizungumza kwa hasira huku nikijitahidi kuizuia hasira yangu ambayo siku zote ni mbaya na taratibu nikageuka na kuondoka zangu.Na nikafika kwenye moja ya maskani na kuwasalimia watu wote nilio wakuta na mimi nikatafuta sehemu nikakaa huku nikiwasikiliza mabishano yao ya mpira dhidi ya timu za afrika zinavyo fanya vibaya kwenye kombe la dunia la mwaka huu na jinsi mabishano yao yanavyo endelea nikajikuta hasira yangu ikipungua
“alafu wewe jamaa ni mwera(polisi) nini?”
“kwa nini?”
“kwa maana umekuja hapa umesalimia na kuvamia vamia kijiwe cha watu usije ukawa unatuchunguza?”
“hapana jamani mimi mtu wa kawaida sana”
“sio kawaida usije ukasababisha pira(gari la polisi) likaja hapa ni kutunyanyua”

Jamaa mmoja aliye jazia kifua akanisogelea huku akiwa na kipisi cha bangi mkononi huku kikiwa kinawaka kisha akavuta fumba kubwa la moshi na kuinama na kunipulizia usoni jambo lililo nikasirisha sana na kujikuta nikinyanyuka na kumtandika kichwa cha pua na akayumba nyumba na kuwafanya wezake wapatao wanne kunivamia na kuniangusha chini na kuanza kunishambulia kwa mangumi na kujikuta nikimdaka mmoja sikio lake na kumng’ata kwa nguvu zangu na kumfanya atoe ukelele mkubwa huku akisema anakufa na nikamuachia kumng’ata na akanyanyuka huku damu zikiwa zinamwagika kwenye masikio yake na gafla vumbi jingi la gari lililo funga breki za gafla likasimama na watu walio nishambulia wote wakakimbia na kuniacha nikiugulia kwa maumivu.

Nikastukia askari wawili wakiwa wakininyanyua huku wakinipiga na virungu vya miguu na wakanisukumia kwenye gari lao walilo kuja nalo.Kwa wenge la maumivu sikujua ni wapi wananipeleka.Gari likasimama kwenye mtaa mwengine na kuwakuta askari wengine wapatao wanne wakiwa na bunduki mikononi wakiwaamrisha watu wapatao nane waliokuwa wamelala chini huku mikono yao wameiweka kichwani na wanavyo onekana ni wavuta bangi.Watu hao wakaamrishwa kuingi ndani ya gari hili la polisi na watu wengi tumezoea kuyaita ‘defendar’ na sote tukajikuta tukiwa tumetosha na askari wote wakapanda na likaondoa kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa tukawa tumesimama kwenye moja ya geti ambalo kwa haraka nikafahamu kuwa ni gereza la keko.

Gari ya polisi ikaingia ndani na sote tukaamrishwa kushuka na kupanga mastari mmoja huku tukiwa tumechuchumamaa na tukaanza kuhesabu namba huku na mimi nikiwa namba tano kati ya watu tisa tuliopo kwenye eneo hili na tukasimama huku mikono tukiwa tumewekeana kwenye mabega na kunyoosha mstari mmoja na tukaaza kutembea huku tukiongozwa na askari wa magereza hadi kwenye chumba kimoja cha mahabusu na sote tukaingia ndani na mlango wake ukafungwa.Nikatafuta sehemu yangu na kukaa huku nikijutia kitu kilicho nifanya nikae kwenye ile maskani ni nini.
“hata nikiwaambia kuwa mama yangu ni waziri haina tija”

Nilijisemea mwenyewe kimoyo moyo na sikuwa na uwezo huo kwa jinsi ninavyo wajua askari wangeniambia mambo ya dharau ambayo yangenikera zaidi na kunisababishia matatizo mengi zaidi.Hadi jioni inaingia sikujua ni kitu gani kinacho endelea juu ya chakula.Usiku mzima sikuweza kulala kutokana na baridi kali kwenye sakafu isitoshe tumbo langu tangu jana usiku halikuuingiza chakula cha aina yoyote.Mawazo ya jinsi nitampata mama yangu yakaanza kunitawala kichwani kwangu kwani kwa maelezo ya john aliniambia kuwa mama yangu yupo south africa akiwa anaumwa na amelazwa.

Hadi inatimu asububuhi sikuweza kupata usingizi na kengele kubwa likagongwa na milango ikafunguliwa na wezangu wakatoka kwa haraka na mimi ikanibidi nitoke kwa haraka na kuwafwata kwa nyuma na tukafika kwenye sehemu na kuwakuta wafungwa wengine walio valia sare wakinganyanyiana mabakuli yaliyo tengenezwa na alumuminiam na nimachafu ndani ya maji yaliopo kwenye karo na anayepata chombo chake anakimbilia kwenye sehemu unapotolewa uji.Nikabaki nikiwa nimesimama na kutokujua ni nini nifanye kwani nikahisi endapo nitakunywa uji wao ninaweza nikatapika kwani una harufu mbaya sana.
Watu wakakanywa uji kisha sisi tulio tolewa kwenye chumba tukaamrishwa kurudi kwenye chumba tulicho toka.

“oya wewe ni mtoto wa mama nini?”
Jamaa mmoja alizingumza na nikabaki nikiwa nimemtazama pasipo kukjibu kitu cha aina yoyote huku akininyooshea kidole
“oya wewe chok* si nanikuuliza wewe ni mtoto wa mama?”
“kwani wewe umezaliwa na mbwa?”
“ahaaa dharau sasa hizo”
“sio dharau unavyoniambia kuwa mimi ni mtoto wa mama ina maanisha wewe umazaliwa na mbwa tena mbwa koko”
“oya dogo inakuwaje anakuita mbwa koko alafu na wewe unakubali kirahisia rahisi”
“na wewe yasiyo kuhusu isiyaingilie ua na wewe unataka kuitwa mbwa koko?”

Jamaa aliye ingilia mada akanifwatwa huku kifua chake akiwa amekitunisha na mimi nikasimama kwa haraka na akanisukuma kidogo na kurudi nyuma na kwanguvu zangu zote nikamrukia kwa kutumia bega langu na likatua kwenye tombo lake na kumsukuma hadi ukutani na kuanza kumshindilia mangumi na kuwafanya watu wengine kushangilia kwa nguvu.Jamaa naye hakuwa nyuma katika kuyajibu mashambulizi yangu na kusema ukweli ngumi zake ni nzito kiasi kwamba nikaanza kuona nyota nyota na kwa bahati mbaya akanisukuma na kichwa changu kikagonga kwenye nondo ya mlango na kujikuta nikianguka kama mzigo na kupotaza fahamu
                                                    *****

Nikastuka na kujikuta nipo kwenye kitanda cha hospitalini huku mkono mmoja  nikiwa nimefungwa pingu na pembeni yangu amesimama askari wa magereza.Nikajishika kichwani kwangu na kukuta nikiwa nimefungwa na bandeji kubwa
“unajisikiaje?”

Askari aliniuliza na kunifanya nikae kimya nikiwa nikimtazama kwa macho ya unyonge.Askari akafungua mlango na kumuita nesi kisha na yeye akarudi kukaa kwenye sehemu aliyokuwa umekaa hapo awali.Nesi akaingia huku akiwa amebeba kisinia chenye vifaa vingi na kukiweka pembani kwenye meza iliyopo karibu na kitanda nilicho lala na kuanza kunitazama kwenye jeraha lililopo kichwani kwangu.

“amesha kula?”
“bado hajakula”
“ina bidi tuweze kumpatia chakula ili aweze kunywa dawa”
“hapa ni wapi kwenye kibanda ambacho ninaweza kumnunulia chakula?”
“ukitoka kwenye geti hapo utaweza kuona kibanda cha wauza chipsi na unaweza kumnunulia chakula”
“sawa”
“akimaliza kula ninaomba uniite”
“sawa”

Nesi akatoka na kukiacha kisinia chake na askari akanyanyuka na kutoka nje na nikapata wazo la haraka nikaanza kutafuta kifaa kidogo kinachoweza kuingia kwenye shimo la funguo la pingu na kuchukua kijikifaa kidogo kilichopo kwenye sinia na sikujua kina kazi gani na kuanza kuifungua pingu niliyo fungwa kwa utulivu wa hali ya juu na chakumshukuru mungu ikafunguka kisha nikashuka kitandani japo mwili umetawaliwa na maumivu makali ila nikajikaza na kuufwata mlango wa kutokea kwenye chumba nilichopo na kuwaona watu wakiwa wanaendelea na mishe zao.

Nikatoka ila kitu kilicho nichanganya sikujua askari ni wapi alipo elekea,nikaanza kutembea kwa umakini huku nikifwata sehemu yenye mlango wa kutokea na kwabahati nikamuona kwa mbali askari wa magereza akija kwa mwendo wa haraka huku mkononi mwake akiwa ameshika kifuko cheusi.Nikajibanza kwenye ukuta na akapita pasipo kuniona na kwaharaka nikatoka huku miguuni nikiwa sina hata kitu chohote,nikafanikiwa kuondoka eneo la hospitali na safari hii moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwetu.

Japo kuna umbali kidogo ila nikajikaza kutembea na nikafanikiwa kifika na kukuta geti likiwa limefungwa,nikakumbuka kwenye sehemu ya nyuma ya ukuta wetu kuna matofali yaliyo pagnwa ya mtu mwenye kiwanja chake aye taka kujenga.Nikazunguka na kuyakuta matofi kama nilivyo tarajia
“hivi mwenye haya matofali amefariki dunia au?”

Nilijisemea huku nikianza kuyapanga matofali karibu na ukuta wetu ambao ni mrefu kiasi kisha na kitu kingine kilicho niogopesha ni nyaya za umeme za ulinzi zilizo zungushiwa kwenye ukuta wa nyumba yetu sehemu ya juu.Ikanichukua kama dakika kumi na tano kutengeneza urefu wa ngazi za kuingilia kwenye nyumba yetu na nikafanikiwa kupanda ukutani huku kwa hahadhari kubwa nikizikwepa nyaya za umeme na nikafanikiwa kurukia kwa ndani na ukimya mwigi umetawala ndani ya nyumba,nikafika kwenye mlango wa mbele na kukuta umefungwa na kawaida mlango ukiwa umefungwa huwa funguo tunazificha kwenye vyungu vya udongo vyenye mau.Nikanza kutafuta kwenye chungu kimoja baada ya kingine wala sikuzikuta
“huyu shetani ameondoka na hizi funguo nini?”

Nikaendelea kutafuta na kwabahati nzuri nikaziona zikiwa nimefichwa kwenye kindoo kidogo chenye maua ambayo mama siku zote huwa huyapenda na kwamadai yake ameyanunulia nchini canada na aliyanunua kwa gharama kubwa kubwa sana.Nikafungua ndani na kukukuta vitu vikiwa vimeshanguliwa sana huku kukiwa na chupa nyingi za pombe zikiwa zimezagaa zagaa kwenye sakafu huku vijimito vidogo vya masofa vikiwa vimetupwa tupwa.Nikapanda ngazi hadi chumbani kwangu na kuingia bafuni na kuoga kisha nikapanda kitandani na kulala kutokana na uchovu mwingi sana.

Nikaamka mida ya saa mbili usiku huku niikiwa nimechoka nikaelekea jikoni na sikukuta kitu chochote cha kula hata mafriji yote hayakuwa na kitu chochote,nikakumbuka kwenye nyumba ya uwani kuna handaki ambalo mara nyingi nikiwa nipo likizo nilikuwa nikamuona mama akiingia na sikujua ni kitu gani anacho kifwata ndani ya handaki hilo.Nikaingia kwenye nyumba ya nyuma katika chumba ambacho kuna kitanda kimoja na kiti kisha nikasogeza pembeni kitanda na kulisogeza kapeti lilolopo ndani na kuukuta mlango wa chuma ambao ni mlango wa handaki.

Nikaufungua na kukuta ngazi za kushuka chini ambapo kunagiza la kutisha sana ikanibidi nirudi tena juu kutafuta tochi.Nikafanikiwa kuiona tochi yenye uwezo mkubwa wa wa mwanga.Nikaingia tena ndani ya handaki huku tochi ikiwa inawaka,nikaanza kuona picha nyingi za kutisha zikiwa zimebandikwa kwenye kuta za handaki hili huku kukiwa na vitu vichache sana ikiwemo majoho matatu moja likiwa jeusi la pili likiwa na rangi nyeupe na jengine ni la rangi nyeusi.Sikujua ni ya kazi gani nikakifwata kitabu kikubwa kilicho jaa vumbi nilicho kikuta na kukifungua na kukuta maandishi ambayo sikujua ni ya lugha gani iliyo andikwa ndani yake

Nikakiacha na kukiona kisanduku kidogo cha wastani kikiwa kimefungwa na kuwekwa kwenye kona ya handaki na nikakisogelea na kukifungua,sikuamini macho yangu baada ya kukuta cheni na pete za dhahabu pamoja na vipande vaya madini.Na nikaanza kuchangua changua na kukuta pete moja ya madini ya tanzanite ikiwa imetengenezwa kwa ustadi mkubwa huku kukiwa na vipande vingine vingi vya madini yenye dhamani kubwa na hata madini mengine sikuwahi kuyaona maishani mwangu.Nikakibeba kisanduku huki nikiwa nina furaa kubwa na nikaingia ndani ya chumba changu na kuvimwaga vitu vyote kitandani na furaha ikazidi kunitawala hata njaa sikuweza kuihisi tena na kujikuta nikiaanza kuimba nyimbo za aina mbali mbali huku nikicheza kiduku kisicho na mpangilio maalumu.

Nikazikusanya na kuziweka kwenye kisanduku chake kisha nikaviweka chini ya uvungu wangu wa kitanda na kwenda sebleni na kuwasha tv na kuangalia angalia miziki hadi usingizi ukanipitia.Cha kwanza baada ya kuamka asubuhi nikaoga na kuvaa nguo nyingine zilizo nipendeza na kuingia chumbani kwa mama na kuzikuta baadhi ya funguo za magari zinapo wekwa kwenye kabati na kuchukua moja kisha nikichukua dini moja la kuliweka mfukoni na kutoka nje na kuingia kwenye gari moja aina verosa ambayo mama aliinunu kipindi zinatoka.

Moja kwa moja nikaenda kwa sonara na kukutana na muhindi mmoja na tukakubaliana biashara na nikamuuzia kwa milioni kumi ambazo zinanitosha sana kwenye matumi ya kwenda nchini afrika kusini kumuona mama.Nikaingia saluni moja kiume na kunyolewa vizuri kisha moja kwa moja nikaelekea benki ya backrays kwenye akaunti yangu ambayo ni siku ningi niliifilisi hadi ikabaki kilinda akaunti na kukiweka kiasi cha milioni saba na kubaki na tatu na nikaanza mipango ya kutengenezewa hati yangu mpya ya kusafiri.

Na ndini ya masaa machache nikawa nimefanikiwa kutokana na kuhonga sana pesa kwa watu wanao husika na utengenezaji wa hati za kusafiria na hadi ninafanikiwa kuipata nikajikuta nikiwa nimebakiwa na laki tano na nusu nusu na nikakata tiketi ya ndege ya shirika la south africa aur ways.Na nikaelekea kwenye ofisi za wizara ya afya na kukutana na mmoja wa masekretari wa mama ambaye nina fahamiana naye vizuri na akaonekena kunishangaa.

“eddy si nimesikia umefariki wewe?”
“nani amekuambia?”
“eddy kila mtu anajua kuwa wewe umeuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu kitendo kilicho mpa mama yako mstuko na tumemkimbiza afrika kusini kwa matibabu zaidi”
“tena hilo ndilo nililokuwa nimekuja kulijua mama yangu amelazwa hospitali gani?”
“amelazwa hospital moja inaitwa louis pasteur ipo mji wa pestoria”

“ahaaa asante kwa hilo”
“ila eddy niambie ni kitu gani kilicho kupata hadi ukafufuka kwa maana mimi mwenye kwa macho yangu niliiona maiti yako ikiingizwa mochwari ila cha kustaajabu leo hii ninakuona hapa?”
“ni historia ndefu ila mungu akibariki nikipata nafasi nitakuja kukusimulia ila nashukuru kwa masaada wako”
“usijali nakutakia safari njema”

Kutokana tiketi ya ndege niliyo kata inaondoka saa mbili usiku ikanilazimu kurudi nyumbani na kubeba nguo kadhaa na kurudi uwanja wa ndege kwa kutumia taksi ya kukodi.Nikatafuta sehemu yenye mgahawa na kujipatia chakula cha kutosha kwani kutokea asubuhi sikuweza kuingiza chochote kutokana na mizunguko ya kuandaa safari.Imebaki lisaa limoja kabla ya safari nikaendelea kusubiri kwenye sehemu za abiria.
“samahani kaka hii sehemu kuna mtu?”
“hapana unaweza kukaa”

Dada mmoja aliye valia suruali ya kubana na kuyafanya makalio yake makuwa kujichora vizuri huku akiwa amejiremba na kuonekana mrembo zaidi alianiambia na baada ya kumjibu akakaa pembeni huku akiwa na pochi yake kubwa kiasi na kujikuta nikimtazama kwa jicho la kuiba.Nikaendelea kusoma gazeti hadi tulipo tangaziwa abiria shirila la ndege la south afrika air ways  tujiandae kwa safari na tukapanga foleni na kuanza kuingia sehemu maalumu ya kukaguliwa kisha nikaingia kwenye ndege na kutafuta sehemu ilipo siti yangu na kukaa baada ya mida kidogo akingia dada aliye niuliza kuhusiana na sehemu ya kukaa kisha na yeye akakaa siti ya pembeni yangu na baada ya muda safari ikaanza pasipo kusemeshana kitu cha iana yoyote hadi katikati ya safari ndipo akaanza kuniongelesha 

“samani kaka unaelekea wapi?”
“afrika kusini”
“ahaa mimi ninaitwa emmy”
“mimi ni eddy”
“ahaa nashukuru kukufahamu”
“na mimi pia”
“unakwenda south kufanya nini?”
“ninakwenda kumcheki bi mkubwa ni mgojwa”
“ahaa mimi kule ndio ninaishi ila mimi ni mtanzania
“kwa hiyo wewe ni mwenyeji kule”

“ndio....Mama yako amelazwa hospitali gani?”
“inaitwa louis pasteur”
“ahaa ndipo ninapo fanyia kazi na nidaktari pale”
“kweli?”
“ndio ila nilikuwa nipo likizo ndio ninarudi hivi nilikuja kuwaona wazazi mara moja”
“eheee asante mungu nimepata mwenyeji kwa maana hapa nilikuwa ninajiuliza ni jinsi gani ninaweza kumpata mama yangu”

Safari ikaendelea kwa masaa kadhaa huku nikiwa nina amani moyoni mwangu kwani nimempata mwenyeji wangu.Ndege ikatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa maputo.Emmy akaniomba kwanza niende kwake ili kukipambazuka vizuri tuweze kwenda hospitali kwani yeye amebakisha siku tano za kurudi kazini.Tukafika nyumbani kwake kwenye gorofa refu moja ambalo alinieleza kuwa watu wangi wamepanga na yeye sehemu yake ni gorofa ya saba kutoka chini.
“eddy karibu ndani?”
“asante”

Emmy akanikaribisha kwenye sehemu anayo ishi ambayo yenye vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu.Taratibu emmy akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine na kunifanya nibaki nikiwa nimemshangaa kwani sikujua ana maana gani na imekuwaje amevua nguo mbele yangu na kubakiwa na chupi wakati mimi na yeye hatuna mahusiano ya namna yoyote

 Itaendelea.... 

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 29 & 30 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 29 & 30 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 00:55:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.