RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 25 & 26 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia...
Nikambusu sheila mdomoni na kufungua mlango na kutoka na moja kwa moja nikashuka hadi kwenye chumba alicho nielekeza  sheila.Nikagonga mlango mara tatu na suti ya kike iliyopo ndani ya chumba hicho ikaniruhusu niingie.Nikafungua mlango na kuwakuta manesi watatu wakiwa wameshika mashavu yao huku wakionekana wanyongea na macho yao wameyaelekezea kwenye kioo cha tv iliyopo ndani ya chumba hicho.Na mimi ikanibidi ninagalie wanacho kitazama na kukuta mipigo ya moyo yakiende kwa kasi baada ya kuiona ndege kubwa ikiwa imeanguka huku inawaka moto na kutoa moshi mwingi na mweusi huku kikosi cha zima moto ambacho sikujua ni cha nchi gani wakijitahidi kuzima moto kwa kutumia magari yao maalumu ya kuzimia moto huku baadhi ya miili inayoonekana kuwa imefariki ikitolewa ndani ya ndege hiyo

Endelea...
“karibu kaka yangu tukusaidie nini?”
Nesi mmoja aliniuliza swali ila sikumjibu nikabaki nikiitazama taarifa inayorushwa kupitia kituo cha televishion ya sky news kinachopatikana nchini uingereza.Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio kana kwamba nimekimbia umbali mrefu pasipo kupumzika.Nikayasoma maandishi makubwa yaliopo ubavuni mwa ndege hiyo na kukuta yameandikwa emirates kiasi kwamba nikajikuta nikishusha pumzi taratibu na manesi wote wakabaki wakinitazama.

“kaka kaka”
“naam”
“mbona unashangaa?”
“ninatazama hiyo taarifa ya habari”
“inasikitisha sana kwa maana watu wote waliopo kwenye hiyo ndege wamefariki”
“imekuwaje hiyo ndege ikaanguka?”
“ilianguaka kipindi inapaa imesababishwa na hali ya hewa kutokuwa nzuri”
“imeangukia nchi gani?”
“imeangukia tailand”

Kidogo nafsi yangu ikapata unafuu na tabasanu likarudi usoni mwangu taratabu kwani nilidhani itakuwa ni ndege ambayo amepanda mama.Nikawaomba dawa za kutuliza maumivu ya kichwa wakanipatia pamoja na maji nikazinywa na kuwashukuru na kuondoka na kuwaacha wakiendelea na shughuli zao.Nikaenda kwenye maduka ya simu ambayo hayakuwa mbali sana na hopsitali na kununua simu kwa ajili ya sheila na kupitia kwenye sehemu wanapouza chipisi.Nikanunua chips za kutosha na kurudi hospitali na kumkuta sheila akizungumza na madaktari.

“hali yako inazidi kuridhisha na baada ya siku kadhaa tunaweza kukupa ruhusa ya kutoka hospitali”
“kwani hamuwezi kunipata hata leo?”
“kwa leo ni vigumu inabidi umalizie dozi yako ya vidonge na sindano za kukausha kidonda na baada ya hapo tutakuwa huru katika kukuruhusu.”
  
Tukakaa hospitalini siku mbili huku nikiendelea kumuuguza sheila na ndani ya siku mbili sikuweza kupata taarifa yoyote kuhusiana na mama juu ya kupatikana kwa ndege yao ambayo imetekwa na watu wasio julikana.Sheila akaruhusiwa kutoka hospitalini na akapewa vidonge ambavyo endapo atajisikia maumivu ameze.Nikapepeleka gari gereji kufanyiwa ukarabati wa vitu vidogo vidogo na kumuacha sheila akijiandaa kwa ajili ya safari ya kurudi dar es salaam.

“kaka hii gari umeinunua wapi?”
“kwa nini?”
“nina mwaka wa 21 tangu nianze kutengeneza magari ila sijawahi kuiona gari ya dizain hii kwa maana mmmm imekusanya mambo mengi”
“ahaaa hizi gari mbona zipo ukihitaji unazipata tuu”
“aise ila hii gari si chini ya milioni mia na kitu”
“imezidi zaidi ya hapo”

Niliendelea kuzungumza na fundi mkuu wa gareji ambayo nimeileta gari yangu,nikastukia nikiguswa bega kwa nyuma nikageuka na kukutana na sura ya madam rukia na kunifanya nistuke kiasi kwamba mapigo ya moyo yakaaza kunienda mbio.

“mbona unastuka eddy?”
“ha.....Pana nimeshangaa tu kukuona hapa”
“wife(mke) unajuananaye huyo kijana?”
Fundi gereji aliuliza swali na kujikuta nikizidi kupata kigugumizi chakuzumza kiasi kwamba nikaabaki nimekaa kimya
“ndio ni mwanafunzi wangu wa kidato cha tano,huyo ndio chanzo cha shele yetu kufungiwa”
“kaka sura yako inaonyesha mpole kumbe ni mkorofi kiasi hicho?”
“hapana mambo ya kawaida”

Nilizungumza huku nikibabaika kwani kila nikimtazama madam rukia ninakumbuka tukio lililotokea porini na jinsi nilivyo fanya naye mapenzi kwenye kichaka isitoshe nikakumbuka niliusikia mlio wa bunduki na kujua ni lazima atakuwa ameuawa na mkuu wa shule.

“ehee lete story edy ile siku ilikuwaje?”
Madam rukia aliniuliza swali baada ya mume wake kuondoka na kuingia kwenye moja ya chumba na kuanza kuzungumza  na wafanyakazi wake.Nikamuadisia madam rukia kuanzia tulipo achana hadi nikafika hopsitalini na yeye akaanza kuniadisia tangu tulipo achana.

“mimi ile siku bwana nilikutana na vijana ambao ni wanakijiji cha karibu kwenye ule msitu wenyewe walikuwa wanakwenda kuwinda.....Sasa pale ulipo niacha mkuu wa shule na wezake si wakawa wananifwata basi wale vijana wakatanda ile sehemu tuliyopo na kuanza kuwashambulia waalimu na kuwatoa mbio za kufa mtu basi ikawa ndio pona pona yangu”

“mbona nilisikia mlio wa bunduki alipigwa nani?”
“ahh mkuu wa shule si alikuwa anajifanya kidume anapiga bastola juu hewani ili kuwatisha wale vijana......Wee alipigwa gongo moja la pua hata sijui ile bastola aliitupia wapi nilisikia akitoa ukulele wa uwii na kuanza kukimbia....Sasa na ile miguu yake yenye matege ya kaekejea upande mmoja ungekuwepo ungecheka”

“mmmm sasa ulirudije mjini?”
“wale vijana wakaniazimisha simu na nikampigia my husband(mume wangu) nikamuelekeza nilipo akaja kunichukua na tukarudi mjini pamoja”

“ulimuambia jamaa kuhusiana na jinsi ulivyo fika porini?”
“ndio ila nilimuambia kuna majambazi ndio waliniteke...Ehee madam merry anaendelea vizuri amefanyiwa upasuaji na kizazi chake kimerekebishwa vizuri ila sasa hivi yupo powa”
Madam rukia alibadilisha mada baada ya mume wake kufika katika eneo tulilopo na sikuwa na haja ya kujiuliza ni kwanini amebadilisha mada nikajua moja kwa moja ahitaji mumu wake atambue kuwa mimi nilikuwa naye porini
“hivi wamesemaje kuhusiana na swala zima la shule kuendelea?”

“wamesema watatoa tangazo kwenye vyomba vya habari pele shule itakapo funguliwa ila kwa sasa wameunda tume ya madai yaliyopelekea shule kufungwa ambayo itachunguza kila kitu na wanafunzi walio kamatwa na polisi wapo wengine wanahojiwa”

“sasa hiyo tume watatumia muda gani kuchunguza hayo madai yato kwa maana siku zinakwenda mbele na masomo ndio hivyo yamesimama?”
“mimi wala sielewi ila kidato cha sita na cha nne wamesambazwa kwenye shule za jirani ili kuendelea na masomo hadi pale majengo yatakapo fanyiwa ukarabati nao ndio watarudi”
“ahaaa....”

“wewe sasa hivi unakwenda wapi dar au kwa marry?”
“huyo merry mimi wala sihiaji kumsikia kwa maana mume wake amenizingu sana majuzi”
“wee amekuonea wapi?”
“si nilikwenda kumcheki hospitalini sasa nikawakuta wana mazungumzo yao basi mimi ikanibidi niwaache niondoke zao basi jamaa akanifwata na kuanza kunipiga vibao mbele za watu na mimi nikampiga basi mambo yakaharibika pale hospitali nikaamua kumpotezea”

“ndio ukaumia hivyo?”
“hapa nilipata ajali ya gari ndio maana nikafungwa huu mbadeji”
“pole mwaya ila yule mume wa marry anajisikia sana”
“kwani anafanya kazi gani?”
“ni muwekezaji kwenye madini anasimamia kampuni ya baba yake kwenye kuchimba madini”

“tena nimekumbuka kuna kitu nahitaji unisaidie?”
“kitu gani?”
“si unamjua yule mdogo wa mke wa mwalimu nyange”
“yupi?”
“tuye mrefu refu kiasi na nimweupe”
“ahaaa unamzungumzia manka”
“ehee huyo huyo”
“mmmm yule mtoto wa watu anamatatizo sana kwani ni juzi juzi aliungua na maji ya moto usoni”
“kwa nini?”

“akili yake si imemruka yaani zinaingia na kutoka.Kuna kipindi akili yake inakuwa sawa na kuna kipindi akili yake inapote hii nikutokana na ajali iliyo mpata”
Nikaanza kujisikia vibaya moyoni mwangu kwa maana manka ni dada yangu japo nimefanya  naye mapenzi pasipo kujua ila bado ni dada yangu

“hivi kwenye ajali ndugu zake walisalimika?”
“yaaa dada yake alipona na shemeji yake siku ya ajali wao walibaki dar na kutokana na gari yao kujaa watu”
“mmmm.......Nasikia alikuwa na ujauzito?”
“ulitoka chezea ajali wewe ila mbona unaniuliza maswali mengi ambayo ni vigumu kwa mtu kama wewe kutambua hayo mambo?”
“kawaida tuu”

Madam rukia akaondoka na mume wake wakaniacha nikilisimamaia gari langu lioshwe na mafundi wasaidizi wa mume wa madam rukia.Wakamaliza kulisafisha gari langu nikawalipa pesa na kuingia kwenye ofisi waliyo ingia madam rukia na mumewe.

“jamani mimi ndio ninaondoka zangu hivi”
“bwaba mdogo karibu sana”
“asante na pesa ya matengenezo nimewalipa vijana wako”
“hakuna shida nakukaribisha tena na tena”
“asante madam mimi ngoja niamshe popo”
“eddy unakiswahili cha kihuni kuamsha popo ndio nini?”
“maana yake ni kuondoka”
“ahaa sasa hembu nianchie namba yako ya simu endapo kutatokea lolote nitakujulisha”
“sawa”

Nikamuandikia madam rukia namba yangu ya simu kwenye simu yake kisha na mimi nikajibipu na nikaisave namba yake nikaanachana nao na kurudi zangu hospitakini nikamkuta sheila akimaliza kuagana na manesi wake ambao alishaanza kuwazoena kama dada zake na kuwafanya baadhi ya manesi kumwagikwa na machozi haswa nesi aliyekuwa akimuhudumia sheila kwa karibu sana na ndio alikuwa akiitoa simu yake kwa ajili ya mawasiliano.Tukaondoka hospitalini na kurudi katika hoteli tuliyo fikizia na kuchukua mizigo yetu ambayo tulikuta imehifadhiwa kwenye sehemu malumu hii ni baada ya muda wetu wa vyumba tulivyo lipia ulikwisha.Safari ikaanza taratibu huku nikiendesha gari kwa umakini mkubwa kuepuka ajali zisizo na ulazima

“eddy nakupenda sana mume wangu”
“nakupenda pia mke wangu”
“yaani natamani hata tuishi pamoja kabisa”
“usijali mke wangu tutaishi pamoja”

Tukaendelea na safari huku ukimya ukiwa umetawala ndani ya gari,sheila akaweka vizuri siti yake aliyo kalia na kuanza kulala na kuniacha mimi nikiendelea kuendesha gari hadi tunafika mombo mida ya saa tisa alasiri nikamuamsha sheila na tukaingia kwenye hoteli ambayo ninapenda kuingia kwa kupata chakula nikiwa kwenye safari kati ya dar na arusha.Simu yangu ikaingia meseji na namba ngeni ambayo si yatanzania huku ujumbe wake ukiwa ni mfupi sana na kunistua kidogo.

‘nipigie’
Nikabaki nikiwa nimeutazama kwa muda huku nikiwa na maswali kichwani ni nani aliye nitumia ujumbe wa namna hiyo.Nikaingia kwenye akaunti yangu ya simu na kununua muda wa kutosha wa maongezi kisha nikaipiga namba ya simu.

“eddy mwangu hujambo”
Nikaisikia sauti ya mama na nikajikuta nikisimama kwa haraka na kuelekea kwenye vyoo kuzungumza na simu ambayo kwangu ni muhimu sana
“sijambo mama shikamoo”
“marahaba mwanangu sina muda wa kupoteza ila ninakuomba uje nchini iraq tupo kizuizini na hap.....”

Nikasikia mama akitoa kelele za kupigwa na watu ambao wanazungumza kiarabu ambacho sikuwa ninakielewa na baada ya muda kidogo simu ikakata na kujikuta nikianza kupandwa na hasira huku jasho likinimwagika.Nikatoka na kwabahi mbaya kwenye mlango wa kuingilia chooni nikagongana na jamaa anaye onekana ni sharobaro na kuifanya simu yake ya gharama aliyokuwa anaichezea kuanguka chini na kupasuka kioo,nikataka kuondoka jamaa akanishika mkono na kunivuta nirudi sehemu aliyo simama.

“wewe fala umeangusha simu yangu hata kuniomba msamaha unaondoka ondoka”
“fala mwenyewe kwanza niachie mkono wangu kati ya simu hako kakopo kako ndio unakaita ni simu”
“kwa hiyo mimi unaniita fala si ndio”

Jamaa alizungumza kwa hasira kiasi kwamba akanishika tisheti yangu kifuani na kuanza kuikinja huku akinivuta kiasi kwamba akazidi kunipandisha hasira.Nikaitoa mikono yake kwa nguvu kifuani kwangu na kumsukuma jamaa na akarudi nyuma kidogo na kuanza kunirushia ngumi ambazo zilinipata kifuani.Nikajirusha na bega langu kilampiga tumboni kwake kama wanavyofanya wacheza miyereka na nikamsukuma na sote tukajikuta tukiangukia mlango wa choo hadi ukavunjika.Nikanyanyuka haraka na kamkaba jamaa shingoni kwa muda na kuwafanya watu walio liona tukio kuja kutuamua.
  
“eddy mume wangu ni nini unacho kifanya”
Sheila alizunumza huku akinishika mkono akisaidiana na watu wanao amua ugomvi kuniondoa katika sehemu ya tukio
“wewe boya tuu kamlale mama yako ambaye ni malaya”

Jamaa alinitukana tusi lililoamsha hasira zangu upya na kujikuta nikiwazidi nguvu watu walio nishika na kwenda kumvaa jamaa na safari hii nikaanza kumshindilia ngumi za hasira kiasi kwamba jamaa akapasuka sehemu ya jicho lake na uso wake kujaa damu idadi ya watu ikazidi kuongezeka na kunitoa katika sehemu ya ugomvi na kuniingiza kwenye moja ya chumba kinachotumika kama ofisi ya eneo hili la hoteli.
“eddy mume wangu punguza hasira nakuomba tafadhali nipo chini ya miguu yako.Nakuomba baby”

Sheila akazidi kuendelea katika kunituliza kiasi kwamba nikabaki nimekaa kimya huku mwili ukiwa unanitetemeka kwa hasira huku meno yangu nikiwa nimeyakaza kwa kuyang’ata kwa uchungu na hasira kwani katika maisha yangu kitu ambacho kinanichukiza ni mtu kumsema mama yangu vibaya
“eddy wangu nakuomba uachene na wapumbavu mume wangu wasikupotezee muda wako...Ehhee tulia mume wangu sawa”

Sheila alizungumza huku akinikumbatia na kuanza kunifuta machozi yanayonitoka kwa hasira,wakaingia askari wawili na wakasimama mbele yetu huku wakijishauri kitu cha kuniuliza na mmoja wao nikamkumbuka haraka ni miongoni mwa askari walio nikamata siku manka na familia yake walipo pata ajali na wakanipeleka kituo cha polisi mimi na dereva wa mama
“kaka zangu niwasaidie nini?”
“ahaa tulikuja kumchukua jamaa akatoe maelezo kituoni kwa tukio zima lililo tokea”
“siendi kokote na ole wake mtu aniguse ninakufa naye”

Askri wakakaa kimya huku wakinitazama na kumfanya sheila awakonyeze kwa ishara ya kuniacha hadi hasira zipungue.Askari wakatoka na kuniacha na ndani ya lisaa hali yangu ikarudi kama awali hii ni baada ya sheila kunibembeleza kwa kila aina ya maneno mazuri ya kuvutia.Tukatoka ndani ya chumba tulichopo huku sheila akinipigisha stori za kunifurahisha na kunifanya nicheke,nikakutana na askari waliokuja kunikamata wakanifwata kiustaarabu na kuniomba niongozane nao hadi kwenye kituo chao na sikufanya ubishi.Tukaingia kwenye gari letu na kuongozana nao huku na wao wakiwa kwenye gari lao na haikichukua muda tukafika kwenye kituo cha polisi.

Nikakutana na baadhi ya wazee wapatao wanne wakiwa mamevalia mashati ya kijani sura zao zikiwa zimejikunja baada ya sisi kuingia na pembeni yao akiwa amekaa kijana niliye pigana naye na sura yake ikiwa na maplasta huku ikiwa imevilia damu.Wakaanza kuzungumza lugha ya kipare ambacho ninakielewa viruzi kwani walianza kumuuliza kijana wao ni nani aliye mpiga na akawajana kwa kuninyooshea kidole kuwa mimi ndio nilio mpiga hadi akaumia sura nzima
“mimi ni diwani kwani umepiga mwanangu”

Mzee mmoja mwenye kitambi cha wastani alizungumza kwa hasira na kabla sijamjiu sheila akanifinya mkononi na kunifanya nimtazame bila ya kumjibu chochote kwani nilipanga kupa tusi ambalo asinge nisahamu maishani mwake.

“mzee wangu ninakuomba umsamehe mume wangu kwani ni hasira tuu ndizo zilipelekea ugomvi kati yake na huyo mwenzake”
“wewe koma mwanamke malaya mkubwa usiye na haya wewe unaweza ukamuita huyu kapupwe wako mume ehee kwanza sijazungumza na wewe”

Mzee akazidi kuzungumza kwa hasira kiasi kwamba nikajikuta na mimi hasira zikaanza kunipanda taratibu na sheila akanishika kifuni ili jazba ishuke na sikuelewa ni kwanini askari wamekaa kimya mzee akiwa anazungumza
 “sawa mzee wangu ila ninakomba mumsamehe na kama kuna gharama zozote tupo tayari kuwalipa”
“wewe mwanamke huwezi kunilipa mimi....Uliza hapa mjini mzima wananijua mim ni nani?’

“mzee wangu naona ustaarabu umekushinda...Sijaja hapa kusikiliza kuwa wewe ni nani au unakazi gani.....Na nyinyi mumekuja kunichukua kule ili nije nikutane na wazee kama hawa wasio na aki.....”
Sheila akaniziba mdomo ili nisimalizie  nilichokuwa nikikizungumza kwani kingeamsha ugomvi upya
“mzee wangu tukauomba utusamehe kwa yaliyo jitokeza sema kama kuna kiasi chochote chapaesa ninaweza kukulipa”

Kuepusha shari nikatoka kwenye kituo cha polisi na kuingia ndani ya gari na kumsubiria sheila ambaye baada ya robo saa akatoka na kuingia ndani ya gari
“wamesemaje?”
“wametaka tuwalipe gharama za matibabu pamoja na gharama za vitu vilivyo haribika kwenye hoteli.Kumbe yule mzee ndio mmiliki wa hoteli na yule mwanaye alikuwa kama msimamizi pale”

“na wanataka kiasi gani cha pesa”
“milioni moja na nusu”
“waache upuuzi wao tuondoke watapewa na babu zao”
“eddy”
“tuondoke zetu wasilete uhuni yeye si amesema sisi hatuwezi kumlipa basi achana nao”
“edd achana kuwa mbishi mume wangu wameniomba nije kujadiliana na wewe ili tujue tunawalipa nini?

“ahaa basi majadiliano yetu mimi na wewe ni kwamba hakuna swala la kuwalipa cha msingi tuondoke zetu kwanza ninahitaji tufike dar leo hii kabla ya saa nne usiku na sasa hivi ni saa kumi na mbili jioni”
“eddy nakuomba tuwalipe mume wangu tuepushane na shari dhidi yao kwani watu wenyewe wanaonekana hivi hivi ni washirikina”
“funga mkanda wewe unaogopa wachawi?”
“ehhhee”
“na waturoge basi kama niwacawi kweli”

Nikawasha gari na kuondoka eneo la kituo cha polisi nakuendela na safari huku gari nikiizidisha mwendo na kumfanya sheila kuwa na wasiwasi na mwendo ninao tembea nao kwani ninatembea na zaidi ya spidi 220 ambacho ni kiwango cha juu na gari za kawaida za tanzania mwisho wa spidi yake ni 180.

“eddy punguza mwendo basi”
“ninaharaka mke wangu”
“jamani baba angu haraka ya wapi wakati tunaekelekea nyumbani”
“nataka niwahi kufika ili nipange safari ninahitaji kwenda iraq”
“eddy nimesikia vibaya au.....Unataka kwenda wapi?”
“iraq ndipo mama alipo kamatwa na hapa ninataka kwenda kutoa taarifa kwenye wizara ya mama wajue wananisaidiaje”
“mume wangu nitabaki na nini?”

“si nitarudi kwani ninakwenda kufa huko na hapa breki ya kwanza ni nyumbani kwetu”
“sawa mume wangu”
Tukafanikiwa kufika dar es salaam saa tano na robo usiku na moja kwa moja tukafikizia nyumbani na kupiga honi na akatoka askari huku akiwa ameishika bunduki yake kwa umakini na kuniomba nishuke kwenye gari kwani ninahisi hakujua kama ni mimi.

“eddy habari yako”
“salama vipi kaka”
“safi tuu nifungulie geti niingie”
“siwezi kufanya hivyo kwani bosi ameniambia nisimruhusu mtu yoyote kuingia ndani”
“bosi gani na wewe si unajua kuwa hapa ni kwetu sasa kwanini usiniruhusu?”
“baba yako ndio amesema nisiruhusu mtu yoyote kuingia ndani kwani anawageni humo ndani”
“amerudi lini?”
“anasiku nne tangu arudi hapa”
“na ha wageni ndio wamefungua mziki huo kwa sauti ya juu hivyo?”
“ndio”

Nikashuka ndani ya gari kufungua geti dogo na kuingia ndani huku sheila akinifwata kwanyuma kwa hatua za haraka,nikaufungua mlango na kukuta wasichana nane wakiwa wamevalia chupi huku wawili wakiw uchi kabisa wakikatika mauono mbele ya baba ambaye anaonekana amelewa huku akipiga kelele za kufurahia
“baba....Baba”

Baba akastuka na kuchukua rimoti ya redio na kuizima kisha akanyanyuka huku akiwa anayumba yumba na mkononi kwake akiwa ameshika chupa ya whyne na akaanza kupiga hatua za taratibbu kunifwata kwenye sehemu niliyo simama
“baba ni nini unacho kifanya ina maana wewe hujui kitu kilicho mpata mama na unakula raha na hawa machangudoa zako?”

Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakianza kunilenga lenga
“wee koma kwanza ni nani aliye kupa ruhusa ya kuingia humu ndani kwangu?”
“kwahiyo kwenye nyumba hii mimi sina ruhusa ya kuingia?”
Nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu na kunifanya niyumbe na sheila akanisaidia kisimama wima nisianguke chini

“huna mamlaka ya kuzungumza mbele yangu na kuanzia leo hii mama zako ni wale pale wanao cheza mbela yangu na mama yako kwanza hajui mapenzi kitandani.....Ni mzito hajui kukatika anakaa kama boga lililo ozeana”

Maneno ya baba yakazidi kunipandisha hasira na mbaya zaidi wasichana alio kuwa nao wakaanza kucheka kwa dharau huku wakinizomea na kuongea maneno ya kejeli.Baba akanitazama kwa macho yaliyo jaa pombe nyingi na kumfwata sheila na akatazama kwa muda na kumfanya sheila kuanza kutetemeka na gafla akamshika ziwa na kunifanya nishindwe kuvumilia.Nikamsukuma baba na akanguka chini na akanipiga teka la kustukiza na lililonifanya nianguke kama mzigo kisha akasimama na kuanza kuruka ruka kama wapiganaji wa kick boxre na kunifanyia kidole chake akiniomba ninyanyuke ili tupigane

“eddy usifanye”
Sheila akanishika mkono na kuninyanyua na kunivuta kwa nyuma huku akinizuia nisipigane na baba
“eddy twende zetu nyumbani”
“wewe malaya unataka kumpeleka wapi mwanangu”
“mimi sio mwanao na ninawapa hawa malaya zako dakika mbili watoke humu ndani la sivyo nitawaua”
“ohhh eddy hii ni nyumba yangu na kuhusu mama yako hawezi kurudi ndani ya hii nyumba tena kwani tayari ameshakufa”

Moyo ukaanza kuniuma baada ya kusikia mama kuwa amekufa,sheila akanishika kiuno na tukafungua mlango na kutoka nje huku machozi yakinimwagika na chuki zidi ya baba ikazidi kunipanda kiasi kwamba nilatamani kurudi na kupiga naye ila sheila akazidi kunionya nisifanye kitu cha namna hii.

“kuanzia leo hii mama zako ni wale pale wanao cheza mbela yangu na mama yako kwanza hajui mapenzi kitandani.....Ni mzito hajui kukatika anakaa kama boga lililo ozena”
Maneno ya baba ya baba yakezidi kujirudia kichwani mwangu na kuzidi kunichanganya na kuanza kupanga mipango ya kumuua baba pale nitakapo pata nafasi,sheila akaniingiza kwenya gari na akaingia upande wa dereva na tukaondoka katika eneno la nyumbani.

Ndani ya dakika ishirini tukafika nyumbabi kwake na tukashuka  kwenye gari akanifungulia mlango ni nakapitiliza mojakwa moja hadi ndani kwake na kujitupa kitandani na kumuacha akifunga miliango,sikutegemea ata siku moja baba yangu atakuja kinidhalilisha mbele za watu mbaya zaidi ananizalilisha kuhusia na mama yangu kipenzi.Sheila hakunisesha chochote zaidi ya kuvua nguo zake na kupanda kitandani na kukaa pembeni na akaanza kunivua nguo moja baada ya nyingine na kubakiwa na boxr.Kutokana na hasira na kuchoka usingizi mzito ukanipitia na kulala fofo
                                                            ***
“eddy baby kumepambazuka amka ukanywe chai”
“saa ngapi sasa hivi?”
“saa tatu”
Sheila akaninyanyua kitandani na kunivalisha ndala na kuniingiza bafuni na kila kitu anachonifanyia sheila sikuwahi kusanyiwa na mwanameke wa aina yoyote na taratibu nikajikuta upendo ukijijenga ndani ya moyo wangu na kujiapia kuto kumuacha sheila.Nikamaliza kuoga na kwenda moja kwa moja mezani na tukaanza kunywa chai kwa pamoja huku akiendelea kunifariji.

“sheila yale ndio maisha ambayo nilikuwa nikukuambia kuhusiana na baba yangu.....Na sijui ni kwanini anamfanyia mama vile na kitu kingine ambacho kinaniumiza roho ni jinsi baba alivyotembea na mfanyakazi wa ndani na kumpa mimba tena juu ya kitanda wanacholala  na mama”

“mmmm pole mume wangu ila hapa ninahisi kuna kitu tu kinachoendelea kwenye hili swala zima la kutekwa kwa mama na ninavyo kumbuka baba yako alisema kuwa mama amefariki.......Ina maana anajua mama kuwa ametekwa”
Nikakaa kimya na kunyanyuka kwenye kiti na kuingia ndani na kuvaa nguo kwa haraka na huku sheila akinitazama 
“baby unakwenda wapi?”

“nakwenda kutoa taari juu ya sehemu aliyopo mama kama jana alibvyo niambia kwenye simu”
“unaonaje tukaenda sisi wenyewe iraq kwa maana hapa ninahisia mbaya kuhusiana na lilicho yokea kwa mama mkwe”
“ila ngoja kwanza niende nikazungumze nao”
“eddy nisikilize mimi ninakuomba twende pasipo kuzungumza na mtu wa aina yoyote kwa maana hili swala lina mikono ya watu wazito na si bure”

Wazo la sheila nikalikubali na akaanza kuvaa nguo zake na kuchakua hati zake za kusafiria na ikatulazimu kwenda nyumbani kuchukua hati yangu ya kusafiria kwa maana nisingeweza kwenda sehemu yoyote pasipo hati hiyo.Tukakodi taksi hadi nyumbani kwetu nikamuomba dereva kusimamisha gari mbali kidogo na ilipo nyumba yetu na nikashuka na kutembea hatua chache hadi nyumbani na kugonga geti na akatoka askari.

“eddy umerudi tena mdogo wangu”
“huyu pimbi yupo humo ndani?”
“ametoka muda huu ameondoka na wale wadada wa jana usiku”
“powa naningia ndani dakika kadhaa tuu nitatoka”
“fanya fasta asije akakukuta”

Nikaingia ndani na moja kwa moja nikaingia ndani kwa mama na kufugua kwenye droo yake aliyo tengenezwa kwa chuma na kujengewa ukutani na nikaingiza namba za siri na ikafunguka na kukuta vitu maalumu ambavyo ni vya siri sana pamoja na pesa ya kutosha,nikachukua hati yangu ya kusafiria pamoja na pesa zote zipatazo dola za kimarekani laki moja na nusu ni sawa na milioni 24 za kitanzania na kuziweka kwenye begi la mgongoni na kabla sijakifunga ndipo nikaona katatasi zilizo ambatanishwa kwa pamoja zipatazo tano huku zikiwa na maandishi makubwa na nikaanza kuzisoma haraka haraka na kukuta ni maelezo ya mama 

“mimi grace j.Mapunda ninaandika nikiwa na akili zangu timamu pasipo kushauriwa na mtu wa aina yoyote.Mali zote ambazo ninazimiliki ni za mwanagu eddy godwin pale itakapotokea nimefariki yeye ndio atakuwa msimamizi na mmiliki mkuu wa mali zote ambazo ni

1.Nyumba ninayoishi yenye dhamani ya shilingi bilioni 1.5 za kitanzania pamoja na nyumba zangu tano za kifahari zinazopatikana arusha zipo mbili,mwanza moja na tanga moja”

2.Maduka nane.Hotel mbili zilizopo afrika kusini na vitega uchumi vilivyopo uingereza na marekani ikiwemo hisa asilimi 35 zilizopo kwenye kampuni ya utengenezaji wa magari nchini marekani”

3.Gari 8 za kifahari”
Sikutaka kuzisoma aina za magari ambayo mama ameyaorodhesha kwa maana ninayafahamu yote na kuachana na mambo mengi ambayo mama ameyaandika na nikajikuta nikistushwa na maneno yaliyopo karatasi ya mwisho.

“mume wangu asihusishwe kwenye chochote kilicho andikwa kwenye huu wosia wangu kwa maana hajahusika katika kupanda nilivyo navyo na si baba halisi wa eddy”
  
Nikahisi nguvu zikiniishia na swala zima la nani ni baba yangu liakaanza kunijia kichwani na nikazitoa karatasi zote zilizopo ndani ya kisanduku maalumu cha mama na nikafungua droo zake na kutoa cheni na pete zake za dhahabu na vitu vyenye dhamani na kuviingiza ndani ya begi na kabla sijatoka ndani kwake nikakumbuka kubeba albamu yenye picha zake na zangu kisha nikaridhika nafsini mwangu na kuufungua mlango na kutoka kabla sijashuka kwenye ngazi nikasikia mlango ukifunguliwa na nikaisikia sauti ya baba ikizungumza na watu wa wili nikachangulia nikawaona watu wawili wakiwa wamevalia nguo za jeshi huku wakiwa wameshika nyundo na sururu mikononi mwao.

“nimeshindwa kufungua kijidro kilichopo ukutani na huyu mwanamke amebadilisha namba za siri”
“kipo wapi mkuu tukushuhulikie?”
“kipo huku juu twendeni mukaking’oe”
Nikaingi jikoni na kujibanza kwenye mlango na wakapita bila kuniona na kuingia chumbani kwa mama na nikatoka na kushuka kwenye ngazi kwa haraka na kutoka nje na kuanza kukumbia na kabla sijafika getini nikaisikia sauti ya baba.

“wewe mpumbavu hapo getini mkamate huyo mshenzi”
Sikusimama na askari wa getini akanipisha na sote kwa pamoja tukatoka getina na tukaingia kwenye taksi na kumuomba dereva aondoke kwa kasi.
“mbona hujanikamata?”
“siwezi kufanya hivyo kwa maana mama yako amanisaidia kwenye mengi na nikifanya hivyo nahisi hata mbinguni sinto kanyaga”
“nashukuru ndugu yangu”

Nikafungua begi langu kutoa noti kumi za dola mia mia na kumpa askari wa getini akanishukuru kupita maelezo kwa muonekano wake tangu azaliwe hakuwahi kushika kiasi cha pesa nilicho mpatia kwa maana anaonekana kuzishangaa
“eddy kuna gari inatufwatwa kwa nyuma hembu iangalie sio ya baba yako?”

Sheila aliniambia na kunifanya nigeuke na mapigo ya moyo yakanza kunienda mbio baada ya kuiona gari ya baba ikija kwa kasi nyuma yetu na gafla dereva akafunga breki za kistukiza hii ni baada ya basi dogo aina ya dsm kujaribu kilipita lori lenye tela refu na kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya voxy iliyokuwa ikija kwa kasi kwenye upande na kusababisha ajali mbaya huku gari hizo zikiziba barabara nzima

                        *****sory madam*****(26)

Sheila aliniambia na kunifanya nigeuke na mapigo ya moyo yakanza kunienda mbio baada ya kuiona gari ya baba ikija kwa kasi nyuma yetu na gafla dereva akafunga breki za kistukiza hii ni baada ya basi dogo aina ya dsm kujaribu kilipita lori lenye tela refu na kugongana uso kwa uso na gari ndogo aina ya voxy iliyokuwa ikija kwa kasi kwenye upande na kusababisha ajali mbaya huku gari hizo zikiziba barabara nzima

Nikafungua  begi langu kwa haraka na kutoa noti mojaya dola mia na kumkabithi dereva taksi kisha sisi tukashuka ndani ya gari na kuanza kukimbia rukijichanganya na watu walio anza kukusanyika wakitoa misada kwa majeruhi wa gari mbili hizi.Mimi na sheila tukapanda bodaboda za pikipiki pasipo baba na watu wake kutuona na kuwaomba boda boda kutupreleka kiwanja cha ndege cha mwalimu julias kambarage nyerere pasipo baba na watu wake kujua ni wapi tulipo elekea.Tukaingia kwenye sehemu ya kutazama ratiba za ndege zilizopo kwa wakati huo na kukuta zimesalia dakika kuni na tano ndege ya shirika la qatar airways na nafasi za tiketi zilibakia tatu tu.Tukakata tikakata tiketi mbili na kuwa miongoni mwa abiria wa ndege hii itakayo ondoka ndani ya dakika kumi zijazo.Kwa haraka haraka tukapanda mstari na kuanza kukaguliwa na wakaguzi tulio wakuta kwenye uwanja wa ndege.
“wewe kijana kaa pembeni”

Askari aliye valia sare zake za kazi huku mwili wake ukiwa umepanda juu na kujazia kwa misuli mizito aliniambia huku akininyooshea mkono wake na kunifanya nianze kupata wasiwasi.Sheila akaruhusiwa kuingia upande wa pili ili kujumuika na abiri wengine wanao iwahi ndege.Nikamkonyeza sheila asiondoke na anisubiri kwani sikujua ni kitu gani kilicho mfanya askari huyo kuniambia nikae pembeni.Wakaja askari wengine wawili wakiwa na mbwa wakubwa na kusimama karibu yangu huku mbwa wao wakianza kunimusa nusa.

“kijana tunakuomba utufwate tunamazungumzo na wewe”
Askari aliye niambia nisimame pembeni alizungumza huku akiwa amelishika begi langu lenye pesa na vitu vyangu muhimu.Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kumfwata kwa nyuma askari hadi kwenye moja ya chumba na  kuingia naye na kukutana na askari wengine wawili wakiwa wamekaa kwenye moja ya meza moja kubwa na baada ya kumuonamwenzao wakampisha na kuanza kuuanali kwa macho ya dharau kuanzia chini hadi juu na kwaishara wakanionyesha sehemu ya kukaa na nikatii nikiwasubiria waniambie kitu ambacho wanataka kuniambia.Nikashangaa kumuona askar mmoja akilifungua begi langu na baada ya kuziona pesa zangu akaanza kushangilia kisha akavimwaga vitu vyote juu ya meza
“mbona munamwaga vitu vyangu?”
“tunakagua tunakuomba uwe mtulivu la sivyo hutotoka mikononi mwetu”

Ikanibidi nikae kimya huku mara kea mara nikiitazama saa ya ukutani na kuona dakika zikikatika taratibu huku zikiwa zimebakia dakika tano tuu ili ndege ifungwe na kuaondoka.Wakaanza kuchagua kitu kimoja baada ya kingine na kuanza kuzisoma baadhi ya karatasi za mama nilizo ziweka kwenye begi na askari mmoja akaanza kuipisha kila karatasi kwa wezake na wakaanza kuisoma taratibu huku wakinitazama usoni
“hii si nyaraka ya serkali?”
“ndio inabdidi atueleze vizzuri kuwa hizi karatasi za mikataba amezito wapi”

Askari wakaendelea kubishana wao kwa wao huku wakiendelea kuzitazama karatasia ambazo sikuzisoma na sikujua ni nyaraka gani wanazo zizungumzia.Ikanilazimu kuwaomna ili wanionyeshe karatasi hizo ila wakakataa
“wewe mikataba ya wizara ya afya umeitoa wapi?”
“ehee....”
“umelisikia vizuri swali langu sina haja ya kulirudia”
“mikataba hiyo ni ya mama yangu ambeye ni waziri wa hiyo sector”
“aaaa kumbe nyinyi ndio munaowapelekea wazazi wenu mikataba ili wakasaini ili kuidhulumu serikali yetu si ndio?”

“sikia mkuu mimi sio kwamba nimeichukua hiyo mikataba kwa ajili a kwenda kumpa mama yangu.....Nyote ninaamini kuwa mujua ya kwamba mama yangu pamoja na viongozi wengine wamekamatwa na sijui kuwa nyinyi muna kazi gani kwa maana hamuonyeshi juhudi zozote katika kuwakomboa viongozi hao”

Nilizungumza kwa hasira huku nikinyanyuka kwenye kiti na kuwafanya askari kuchomoa virungu vyao na kuanza kunisambulia kwa kunipiga sehemu mbali mbali za mwili huku nikimshuhudia mmoja waoa akiingiza pesa zangu kwenye mifuko yake ya suruali na kujikuta nikikasirika na kumsukuma na kuanza kuminyana naye kuzichomoa pesa zangu mifukoni mwake na kuzidi kuwongezea wezake hasira na kuzidi kunipiga virungu na mateke yaliyo tua tumboni na kifuani na kuuufanya mwili wangu kunifanya nianze kutokwa na damu za mdomoni na puani.

Gafla mlango ukafunguliwa na akaingia sheila akiwa ameongozana na waziri mkuu bi.Maimuna ramadhani na akaonekana kushanga na kuwafanya askari kuancha kitendo chao cha kunipiga.Nikabaki nikiwa nimejikunyata chini huku damu zikiwa zinaendelea kunimwagika huku mwili mzima ukiwa umetawaliwa na maumivu na uvimbe kwenye sehemu za kichwa chanu.Sheila akapiga magoti hukua akilia kwa uchungu na kutoa kitambaa chake na kuanza kunifuta damu zinazo nitoka.

“hii ndio kazi muliyo agizwa na serikali kuwapiga watu kiasi hichi?”
Swali la wa waziri mkuu likawafanya askari wote kukaa kimya na sikujua waziri mkuu imekuaje akaja katika chumba hichi ila uzuri ni kwamba ni rafiki wa mama na muda mwingi huwa wanashirikina sana katika maswala yao ya kina mama hususani katika uanzilishi wa mambo ya vikoba kwa wanamama wajasiriamali.

“eddy eddy”
“mmmmm”
Mdomo wangu haukuweza kufunguka kutokana na kuvimba kwa mdomo ambao pia umejeruhiwa kwa kupiwgwa na askari hawa ambao sasa hivi wamejikausha kama wamemwagiwa maji ya baridi.

“kwahiyo hamuna majibu ya kutoa”
Nikamnyooshea askari mmoja aliye chukua pesa zangu na kumf anya waziri mkuu kunimtazama huku akiwa haelewi ni nini kinachonifanya nimnyooshee mkono,nikajitahidi kunyanyuka kwa msaada wa sheila na akanikalisha kwenye kiti
“eddy mwanangu pole sana......”
Waziri mkuu akamnong’oneza sheila na kumfanaya sheila kutoka ndani ya chumba na baada ya muda akarudi akiwa ameongozaa na mlizi wa waziri mkuu.

“nipe simu”
Mlinzi wa waziri mkuu akatoa simu na kumkabidhi waziri mkuu na akaminya batani na kuiweka simu yake sikioni
“habari yako kaka”
“sasa kuna vijana wako wamemjeruhi kijana wangu pasipo kuwa na sababu ya msingi sasa ni hivi ninakuomba uwafute kazi mara moja”
“asante”
Waziri mkuu akampa mlinzi simu kisha akanisogelea na kunitazama kwa macho ya huruma
“mwanangu pole sana”
“asa...N.Te”
“ulikuwa unakwenda wapi?”

“tulikuwa tunakwenda iraq mama jana alimpigia simu eddy na kumuomba amfwate”
Sheila akajibu kwa niamba yangu kwani mdomo wangu ulivimba sana na kunifanya nishindwe kuzungumza vizuri na kumfanya waziri mkuu kuhamaki
“alisema you iraq sehemu gani?”
“hakusema kwani alipokonywa simu na watu walio wateka”
Waziri mkuu akaichukua simu yake na kupiga namba baadhi na kuisikiliazia simu yake na kukifanya chumba kizima kikiwa kimya tukimsikiliza.

“shikamoo muheshimiwa raisi”
“mimi nipo salama tu kuna taarifa hapa nimeipata kuwa viongozi wetu wapi iraq na ndipo walipo shikiliwa mateka”
“ndio taarifa nimeipata kwa mtoto wa grace na anadai jana alizungumza na mama yake”
“sawa mkuu nashukuru kwa ushirikiano wako”
Waziri mkuu akakata simu na kuwatazama askari walio nipiga na kumuagiza mlinzi wake awaandike majina yao pamoja na namba zao za kwenye mashati
“wa..Napes....A zan..Gu”

Nilizungumza kwa kujikaza japo ninapata maumivu makali ila ikanilazimu kufanya hivyo na sheila akasima na kumsogelea askari niliye mnyooshea mkono kwa mara ya kwanza na akanza kumpapasa mifukoni na kuzitoa pesa zangu na kumfanya waziri mkuu kuzidi kupandwa na hasira na kumpiga kibao askari huyo na kumfanya azidi kutetemeka
“pumbavu...Binti watazame na hao wengine”

Sheila akaanza kumpitia askari mmoja baada ya mwengine na kuzitoa wallet zao na kuchomo pesa zote walizo kuwa nazo na nyengine hazikuwa za kwangu ila sheila akazichukua.Akaingia mkuu wa usimamizi wa uwanja ambaye ni askari mkuu
“vijana wako hawa kuanzia sasa hivi sitaki kuwaona kazini.Sawa”
“sawa mkuu”

Tukatoka kwenye chumba huku sheila akinisaidi katika kutembea na baadhi ya watu wakaanza kutushangaa kila tunapopita.Tukaingia kwenye gari ya waziri mkuu na maja kwa moja wakanipeleka hospitali ya muhimbili na madaktari wakanipokea na kuanza kunifanyia huduma huku wakinichoma sindano za kupunguza maumivu.Waziri mkuu akatoa maagizo kwa madaktari nitibiwe katika uangalizi mzuri la sivyo watakiona cha moto kisha yeye akaondoka na kutuacha mimi na sheila.
Baada ya siku mbili nikapata uwezo wa kuzungumza vizuri kama awali japo kuna sehemu za mwili zina maumivu makali bado.

“sheila ile simu ilikuwaje wazari mkuu alikuja kwenye chumba tulichopo?”
“alikuwa kwenye dhiara pale uwanja wa ndee na ndio alikuwa anamaliza kuzunguka kwenye baadhi ya ofisi.Nikamfwata na kumuelezea na kwabati nzur nilivyomuelezea kuhusu wewe akanielewa ndio tukaja mule ndani”
“aaha nashukuru kwa hilo mke wangu”
“ila zile tiketi nimezirudisha na nimewaambia kuwa tumepata dharula ila hadi utakapo pona ndio tutakwenda iraq”
“sawa ila waziri mkuu hakukupigia siku mbili hizi?”

“alinipigia na nilimuwambia kuwa unaendelea vizuri na yeye akaniambia zoezi la kuwatafuta viongozi linaendelea vizuri hatuna haja ya sisi kwenda kwa iraq kwani itaongeza matatizo zaidi”
“sawa ila ndini ya mwili najisikia maumivu sana”
“sehemu gani?”
“hapa kwenye kifua kunaniuma sana nikihema hivi niihisi harufu ya damu”
“weee ngoja basi nimuite dakari”

Sheila akasimama na kwenda kumuita daktari aliye kabidhiwa kwa kuniangalia kwa ukaribu sana.Sheila akaanza kumuelezea dakatari hali ninayojisikia na kumfa ya daktari kutoa agazo kwa wezake wanifanyie uchunguzi zaidi.Wakanipeleka kwenye chumba cha x-reys na wakaniweka kwenye mashine kubwa iliyokaa kama mfumo wa jeneza na kunipitisha kwenye mitambo yao na kutokea upande wa pili wa sehemu hiyo na wakanitoa kwenye kifaa chao na kunirudisha wodini na kumuomba sheila kubaki na madaktari kwa mazungumzo zaidi.Baada ya muda sheila akaingia huku akiwa na sura ya unyonge iliyo anza kunipa wasiwasi kiasi kwamba nikajikuta ninaaza kupata wasiwasi na mimi.

“sheila wamekuambiaje?”
Badala ya sheila kunijibu akaanza kulia na kuzidi kunichanganya na sikujua ni nini kinacho mliza.
“eddy ninakupenda sana mume wangu”
“sawa hata kama unanipenda ila niambie kitu kinacho kuliza”
“eddy sitaki kukupoteza mume wangu bado hatujafikia malengo yetu”.

Sheila akazidi kunichanganya kiasi kwamba nikataka kunyanyuka ila kutokana na maumivu ya kifua changu nikajikuta nikurudisha kwichwa changu kwenye mto nilio uegemezea kichwa.
“eddy madaktari wanasema maisha yako yapo hatarini kupotea....Siku yoyote”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kiasi kwamba nikajikuta  ninazidi kuchananyikiwa huku jasho likinimwagika
“eddy kumbe ulisha wahi kupigwa risasi kwanini hukuniambia hadi leo madaktari wameniambia kuwa kidonda chako cha risasi hakikupona kikamilifu na jinsi askari waliyo kupiga imesababisha damu kuvilia kwenye mapafu na kuanza kujenga uzo kwenye moyo wako”

Nikazidi kuchanganyikiwa na kujikuta nikitokwa na machozi na kumzidisha sheila kulia kwa uchungu
“sheila kwahiyo mimi ndio nitakufa?”
“no eddy huwezi kufa mume wangu.....Usizungumze hivyo kumbuka wewe ndio mwanga wangu we....”
Kabla sheila hajamaliza kuzungumza akaiingia daktari mkuu na akasimama kwa muda akitutizama huku akwa ameshika kikaratasi mkononi mwake.

“binti umemuambia?”
Sheila akaitikia kwa kutingisha kichwa akimuashiria daktari kuwa ndio amenimbia
“binti nilikuambi usimuambie hii itamsababishia matatizo zaodi kwani moyo wake kwa sasa unaweza kushindwa kufanya kazi yake muda woote kuanzi sana na inaweza ikampelekea kifo”
Sikujua daktari kama akili zake zimekamilika vizuri au laa kwa maana kitu anacho kizungumza mbele yangu kikazidi kunichanganya zaidi ya alivyo niambia sheila na isitoshe amemkataza sheila kuniambia kiitu kama hicho na yeye ndio anakizungumza.

“sasa hapa kuna karatasi unatakiwa usaini ili tukamfanyie upasuaji mume wako”
“ngoja kwanza dokta ni nani munataka kumfanyia upasuaji?”
“ni wewe kwani maisha yako yapo hatarini”
“nyinyi si ndio wale mulio mpasua mgonjwa wa mguu kichwa na wakichwa mguu”
“hilo sio jukumu lako na mimi ni mgani.....Binti siani kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mume wako na kama upo tayari kumpoteza basi itakuwa hivyo”
Sheila alachukua katatasi mikononi mwa daktari na akaifungua na kabla hajaandika chpchote nikamuomba nanionyeshe ili nipitie na mimi.

“chochote kinaweza kutokea ikiwemo kifo”
Maandishi madogo yaliyomo kwenye karatasi yakanichanganya sana na kujikuta nikimtazama sheila ambaye amaeshika peni mkomoni kwa kusaini kwa niaba yangu.Sheila akasaini na kumkabidhi daktari karatasi yake na daktari akatoka kwenye chumba.

“eddy nakuomba ujikaze mume wangu”
“kwenye kufa sheila hakuna kujikaza hawa madaktari mimi sina imani nao kabisa”
“usijali kwa hilo mume wangu”
“kwani hiyo oparesheni ninafanyiwa lini?”
“leo hii mida na yamebaki masaa kama mawili”
“sasa imekuwaje na wewe ukasaini pasipo kuniambia kama ninafanyiwa leo kwa maana hapo kwenye hiyo karatasi kumeandikwa chochote kinaweza kutokea ikiwamo kifo sasa unaona ni haki kweli?”
“eddy acha kupanic”

“sio kupanic......Wewe kwanini usaini si uneniambia kuwa yamebaki masaa mawili nisinge kubali kufanyiwa ningesubiria hadi mama apatiakene ili hata nikifa nife vizuri”
“eddy usitake unilize sasa hivi mume wangu hembu tulia madaktari wanajua ni nini wanafanya”

Baada ya masaa wawili wakaingia amadaktari wawili akiwemo yule daktari wa familia akaonekana kushangaa kuniona ndani ya chumba,hakunisemesha akatoka ndani ya chumba na sikumfwatilia sana kwani manesi walianza kuniandaa kwa kunpeleke kwenye chumba cha upasuji huku wakinibadilisha nguo na kunivisha vazi maalumu kwa ajili ya upasuaji.Wakamaliza na kuniweka kwenye kitanda cha matairi na kuanza kukidukuma huku sheila akiwa pembeni yangu na machozi yakaanza kumwagika tena.

Nikastukia nikamuona daktri anaye sukuma kitanda akisukumwa na kuanguka chini na macho yangu yakakutana na macho ya baba yaliyojaa hasira hadi yakawa mekundu.Akanishika kifuani na kunivuta na kunitupa chini na kuanukia mgongo na kusababisha maumivu makali kuzidi kunitawala kwenye mwili wangu hususani kifuani mwangu.Madaktari wakataka kumsogelea baba ila akachomoa bastola yeka na kuwafanya madaktari kusita.Mguu wa baba ukatua kifuani kwangu huku ukiwa umevalia buti lake la jesi kisha bastola yake akaikoki tayari kwa kunifyatulia risasi....

 Itaendelea
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 25 & 26 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 25 & 26 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by Unknown on 00:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.