Vinara wa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa Bariadi Kuwajibishwa

flu-shot
Kufuatia malalamiko ya wananchi ya muda mrefu kuhusiana na kukithiri kwa zisizofaa kwa wagonjwa zinazotolewa  na baadhi ya watumishi wa idara ya afya katika hospitali ya Somanda halmashauri ya mji wa bariadi, mganga mkuu ameagizwa kuwawajibisha  wanaodaiwa kuwa vinara wa lugha hizo pamoja na wale wasiozingatia maadili ya utumishi wao.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Bariadi festo kiswaga alipokutana na watumishi wa afya hospitalini hapo katika kikao cha pamoja ili kuwakumbusha wajibu na majukumu yao wanayopaswa kuyatekeleza wakiwa katika maeneo yao ya kazi ambapo  amesema ni lazima wawajibishwa wenye tabia hizo kwani kauli chafu dhidi ya wagonjwa zinawasababishia maumivu Zaidi wagonjwa .

Katika hatua nyingine ametoa wiki moja kuhakikisha hospitali hiyo iliyokithiri kwa uchafu ,mazingira yake yawe katika hali ya usafi ,ili kuepuka magonjwa ya milipuko.
Kwa upande wake mganga mkuu wa  halmashauri ya mji wa bariadi dkt akilimali mpozemenya  amesema kuwa maagizo aliyopewa atayafanyia kazi ,na tayari hatua zinaendelea kuchukuliwa.

Vinara wa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa Bariadi Kuwajibishwa Vinara wa Lugha Chafu Kwa Wagonjwa Bariadi Kuwajibishwa Reviewed by WANGOFIRA on 07:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.