NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, ATEKELEZA AHADI YA SERIKALI ALIYOITOA BUNGENI
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akikagua
eneo la mpaka katika Msitu wa Hifadhi wa Sayaka katika Kijiji cha
Bugatu, Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza hivi karibuni. Anayeongoza
utambuzi wa mpaka huo ni Afisa Misitu na Nyuki TFS Wilaya ya Magu, Ayoub
Mikae (wa tatu kulia). Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure
Kiswaga. Eng. Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya
maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini kwa ajili ya kutafutiwa
suluhu ya kudumu.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa sita kushoto) akiwa
na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Magu na baadhi ya
Wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka wakikagua
mpaka wa hifadhi hiyo hivi karibuni. Kinachoonekana mbele yao ni Kigingi
cha mpaka kinachodaiwa kusogezwa mbele na wananchi wa maeneo hayo kwa
ajili ya kumega eneo la Hifadhi.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na
wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka katika
Kijiji cha Bugatu Wilayani Magu Mkoani Mwanza hivi karibuni.
Aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi
yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.
Naibu
Waziri Maliasili , Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Bugatu, Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza hivi karibuni wakati
akikagua ramani ya Hifadhi ya Msitu wa Sayaka kubaini maeneo ya mpaka
yenye mgogoro. Eng. Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya
maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini kwa ajili ya kutafutiwa
suluhu ya kudumu. (P.T)
Mbunge wa
Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga (kulia) akizungumza na wananchi wa
Jimbo lake katika Kijiji cha Bugatu Wilayani Magu hivi karibuni.
Mwananchi
wa Kijiji cha Salama kilichopo kandokando ya Hifadhi ya Msitu wa Sayaka
Wilayani Magu, Charles Kassandiga (kushoto) akitoa ombi kwa niaba ya
wananchi wa kijiji hicho la kupatiwa maeneo ya kulima na kufuga kwa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia). Eng.
Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya
Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akiongoza
kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Magu alipotembelea
Wilayani humo hivi karibuni kuona eneo la mgogoro katika Hifadhi ya
Msitu wa Sayaka ambapo aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya
maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya
kudumu.
NA HAMZA TEMBA - WMU
Serikali
kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kupitia upya maeneo yote
ya Hifadhi nchini yenye migogoro ya ardhi kwa ajili ya kuyatafutia
suluhu ya kudumu kwa kutumia mbinu shirikishi.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Eng. Ramo Makani wakati akizungumza na Wananchi wa vijiji
vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka katika Kijiji cha Busega
Wilayani Magu Mkoani Mwanza.
Eng.
Makani alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano imekusudia kubadilisha
mfumo wa utendaji Serikali ambapo kwenye utatuzi wa migogoro iliyopo
kwenye maeneo ya hifadhi nchini itatatuliwa kwa kuwashirikisha wananchi
wa maeneo husika na kuweka kumbukumbu sahihi za makubaliano kufikia
suluhu ya kudumu.
“Maeneo
yote yenye migogoro tunaenda kuyapitia upya, tukija kwenye utatuzi
tutawashirikisha wananchi kupitia Serikali zao za Vijiji ambazo wajumbe
wake watahusika kwenye makubaliano kwa kuzingatia umuhimu na faida za
Uhifadhi lakini huku tukihakikisha tunajibu kero zinazowakabili”
Aliesema Eng. Makani.
Aliongeza
kuwa wakati wa kutatua migogoro hiyo yataainishwa maeneo kwa ajili ya
shughuli za ufugaji na kilimo kuepusha muingiliano kati ya wakulima na
wafugaji pamoja na kuepusha uvamizi kwenye maeneo ya Hifadhi
yaliyoainishwa, utaratibu huo utazingatia sheria, kanuni, taratibu na
miongozo mbalimbali ya Serikali.
Awali
akizungumzia mgogoro wa Hifadhi ya Msitu wa Sayaka, Eng. Makani alisema
kuwa, uamuzi wa kufika katika eneo hilo la mgogoro ni kuona uhalisia
kabla ya kuchukuliwa hatua za kumaliza mgogoro huo ikiwa ni utekelezaji
wa ahadi ya Serikali aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwa Mbunge wa Jimbo
la Magu, Boniventure Kiswaga.
Katika
mgogoro huo wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi hiyo walitoa
malalamiko yao kwa Naibu Waziri Makani kuwa maofisa wa TFS wamekuwa
wakisogeza vigingi vya mpaka wa eneo hilo kumega maeneo ya vijiji bila
kuwashirikisha. “Sio kwamba tunapinga Uhifadhi, lakini tunauliza kwanini
vigingi vinahama kila mwaka kusogelea maeneo yetu” Alihoji Mwanyekiti
wa Kijiji cha Bugatu, Charles Kusenza.
Akijibu
malalamiko hayo Afisa Misitu na Nyuki wa TFS Wilaya ya Magu, Ayoub Mikae
alisema kuwa, kilichokuwa kinafanyika sio kusogeza vigingi bali na
kuimarisha vigingi vilivyokuwepo ambapo utambuzi wake ulifanyika
kitaalam kwa kutumia GPS. Aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wasio
waadilifu walidaiwa kusogeza vigingi vya mpaka wa Hifadhi hiyo ili
wapate eneo la kulima jambo lililoleta taswira tofauti wakati wa kufanya
marekebisho sahihi kwa kutumia mtambo wa GPS uliosaidia kubaini mpaka
asilia.
Ayoub
alisema kuwa sababu ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Sayaka ilikuwa
ni kuhifadhi uoto wa asili, kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi samaki
wa Ziwa Victoria kwa kuwa mto uliopo katika hifadhi hiyo unapeleka maji
Ziwa Victoria.
Baada ya
kusikiliza hoja mbalimbali za wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi
hiyo katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Bugatu, Eng. Makani
alisema kuwa tatizo kubwa aliloliona katika mgogoro huo ni changamoto za
Uhifadhi ikiwemo uelewa hafifu wa baadhi ya wananchi juu ya umuhimu wa
uhifadhi, ushirikishwaji hafifu wa wananchi kwenye uwekaji wa vigingi na
baadhi ya wananchi kuchanganya vigingi vya hifadhi ya maji na hifadhi
ya Msitu, changamoto ambazo alisema zitazingatiwa kwa kina wakati wa
utatuzi wa mgogoro huo.
Alisema
kuwa “Tunahitaji uhifadhi endelevu, peke yetu bila wananchi hatuwezi,
tunahitaji uhifadhi rafiki, tukiwa na uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa
uhifadhi na tukajibu kero zenu mtatusaidia kulinda na kuhifadhi
Maliasili zetu”.
Kwa
upande wa Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo waliopewa
fursa ya kuchangia na kuuliza maswali kwenye mkutano huo walipaza sauti
zao kuiomba Serikali kupitia Naibu Waziri huyo kuwasaidia maeneo ya
kufuga na kulima kutokana na ufinyu wa maeneo uliosababishwa na ongezeko
kubwa la watu. Naibu Waziri Makani Aliahidi kwa niaba ya
Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi nchini yenye migogoro na
kuyatafutiwa suluhu ya kudumu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na
miongozo mbalimbali ya Serikali.
NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, ATEKELEZA AHADI YA SERIKALI ALIYOITOA BUNGENI
Reviewed by WANGOFIRA
on
23:16:00
Rating:
No comments: